Utaratibu na gharama za kupata hatimiliki ya nyumba/kiwanja

Utaratibu na gharama za kupata hatimiliki ya nyumba/kiwanja

Jodoki Kalimilo

Asante kwa taarifa hizi.

Ombi la ziada kama unauzoefu na hii. Je una info yoyote kuhusiana na gharama za uwekaji wa mawe baada ya hatua ya kuwa Ramani ya eneo husika imepitishwa pale Ardhi.
 
Mikael P Aweda

Maelezo yako yote ni mazuri na yametoa mchanganuo mzuri ila hapo nilipo bold inategemea eneo lako kama lilikuwa limepimwa au la, lakini kiujumla kama umepata Offer toka kwa halmashauri ya wilaya au manispaa ukienda kwa kamishina wa ardhi kufuatilia hati yako ni bure kwa kuwa gharama zote zimekuwa covered wakati unanunua kiwanja na zipo indicated kwenye letter of offer, sana sana ni gharama kidogo kwa mwanasheria kama witness nayo ni fedha kidogo ambayo haizidi hata 50,000/=

Unayosema wewe ni ile kama una eneo lako alafu ukaanzisha mchakato wa kulipimisha hapo ndio mchakato unakuwa mrefu maana wajanja watataka kula chao but kama umebahatisha kununua kilichopimwa hati utaipata ndani ya miezi mitatu tu kikubwa ukubali kupigwa kalenda

Mie sina connection lakini nilipata ndani ya huo muda na wengi tu nimewaona, tatizo linakuja kwa vile viwanja ambavyo vimepimwa

Nakuunga mkono hapo kwenye blue ili mambo yawe wazi zaidi na ikiwezekana ndani ya mwezi unapata na kama isipopatikana kuwe na sehemu ya kukimbilia
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa taarifa hizi.
Ombi la ziada kama unauzoefu na hii.Je una info yoyote kuhusiana na gharama za uwekaji wa mawe baada ya hatua ya kuwa Ramani ya eneo husika imepitishwa pale Ardhi.


Mkuu sina uzoefu ila kwa logic tu kama umepimiwa mwenye jukumu la kuweka becon ni yule aliepima maana becon zina namba ambazo wao wanazijua ni zinasaidia kutambua viwanja mbalimbali vilivyopo eneo lako mfano kama kuna becon ipo kwenye kiwanja chako ni rahisi kwa wao kutambua kutoka pale becon ilipo kuna kiwanja / viwanja vingapi vipoIla kuna becon zingine za kienyeji unaweza kuweka maana wakati mwingine kuna weza kuwa na becon 2 katika kila kona alafu zingine unaweza kuweka wewe mwenyewe kama alama zao maana huwa watu wa manispaa wanapokuonyesha eneo lako wanakuja na ramani ya eneo husika na tape measure yao kwa kufuata mwongozo wa zile becon zenye namba hivyo pale ambapo hakuna becon unaweza weka za kwako
 
Zina risiti? Manake aridhi napo naona wamejazana watu kibao sijui wanafanya nini kazi utapeli tu, hata kakitu kadogo utasikia sio chini ya laki, na kazi ya siku inaweza chukua miezi au zaidi ya mwaka. Aridhi kwenye Manispaa na Wizarani ni zaidi ya janga la kitaifa!

Mkuu unalalamika tu,mambo ya ardhi yana misingi yake inayopelekea na kuamua gharama zote za shughuli nzima ya upimaji na ugawaji wa ardhi,jaribu kujifunza vitu sio kutoa lawama moja kwa moja
 
nami napenda kuuliza,mfano mtu amekushikia hati yako kwa sababu mbalimbali anaweza kwenda kwa kamishina kubadili umiliki wa hati yako kwenda kwake bila wewe kuwepo ?
 
Jodoki Kalimilo;

Mkuu nashukuru kwa Maelezo yako mwanana.Mimi nataka kubadili jina kwenye OFFER na nimefata taratibu zote pale Ardhi Ilala baadaye nikaelekezwa niende TRA ambapo kwa Eneo langu la kama robo heka nikaambiwa nitalipia zaidi ya Milioni Moja kwa mahesabu ya harakaharaka.

Naomba mwenye kuelewa na hili anijuze maana mimi sikuelewa. Eneo lenyewe lipo nje kidogo ya jiji.
 
Jodoki Kalimilo

Umetapika yote yanayotakiwa sina cha kuongeza.

Angalisho jaribu kwenda ofisi za mahakama kwa ajili ya suala la kisheria maana ukienda kwa hawa wanasheria wa kujitegemea wana mkono mrefu kukuchomoa mfukoni.
 
Nimepewa uwanja na rafiki yangu(kiroho safi
Twataka tubadili jina kuja kwangu,
Nahitaji taarifa/document zipi? Kufuatilia zoezi hili?
 
Umetapika yote yanayotakiwa sina cha kuongeza.

Angalisho jaribu kwenda ofisi za mahakama kwa ajili ya suala la kisheria maana ukienda kwa hawa wanasheria wa kujitegemea wana mkono mrefu kukuchomoa mfukoni.

Ni kweli mkuu walinichomoa buku tano kwa ajili ya mhuri, tatizo na wanasheria nao wa serikali wanajiweka mbali na wananchi kiaina
 
nami napenda kuuliza,mfano mtu amekushikia hati yako kwa sababu mbalimbali anaweza kwenda kwa kamishina kubadili umiliki wa hati yako kwenda kwake bila wewe kuwepo ?

Mkuu ni vizuri hivi vitu kumwachia mtu unaemwamini maana kwa Tanzania kila kitu kinawezakana kutokea though kuna utaratibu wa kuhifadhi hizi document muhimu kama vile katika mabenki na taasisi zingine ambazo mwananchi anaweza kuhifadhi document yaani the same procedure kama mtu anapoandika wosia na kuuhifadhi kwenye ofisi ya serikali (ila sina uhakika sana ila kuna mtu aliniambia utaratibu huu labda ambao wapo aware wanaweza kufunguka kwa kutusaidia)
 
Nimepewa uwanja na rafiki yangu(kiroho safi
Twataka tubadili jina kuja kwangu,
Nahitaji taarifa/document zipi? Kufuatilia zoezi hili?

Ukitaka kukwepa mizunguko mingi, nenda serikali za mitaa katika eneo la kiwanja chako, kisha watakupa maelekezo, hiyo ni kazi yao, na watakuambia taratibu zote za kufanya na hatua za kufuata. Ndivyo nilivyofanya mimi na sikupata matatizo ye yote. Serikali za mitaa wana daftari la ramani na majina ya wamiliki, iwapo kama kuna utapeli watakuambia mmiliki ni mwenyewe au la.

Angalisho:
  1. Unaponunua kiwanja kwa mtu, hakikisha kwanza unaonana na maofisa wa serikali za mitaa kufanya uhakiki wa kiwanja kabla ya taratibu nyingine za malipo na makabidhiano ili kujihakikishia uhalali.
  2. Hali kadhalika malipo ni bora kwenda mahakamani kwenye ushahidi wa kisheria badala ya kukabidhiana wawili au bila jopo la kisheria linalotambulika kisheria.
  3. Kabla ya kwenda mahakamani kwa ajili ya utaratibu wa kisheria wa malipo kwa mhusika na makabidhiano ya hati, serikali ya mtaa katika eneo husika watakupa barua ya kisheria ambayo utaipeleka mahakamani au kwa mwanasheria wako kwani bila barua ya serikali ya mitaa hakuna kitakachofanyika na utarudishwa huko kuanza upya zoezi hilo.
  4. Hatua zaidi za kubadilisha hati miliki na certificate ya kutamalaki lazima upate barua toka kwa mtendaji wa serikali za mitaa.

Unaona ukweli serikali ya mtaa ndio wenye kukuongoza na kukupa maelekezo yote nini kinatakiwa na hatua zipi zinatakiwa kufuatwa hadi uweze kukamilisha umiliki wa kiwanja chako.
 
Mkuu unalalamika tu,mambo ya ardhi yana misingi yake inayopelekea na kuamua gharama zote za shughuli nzima ya upimaji na ugawaji wa ardhi,jaribu kujifunza vitu sio kutoa lawama moja kwa moja

Asante kwa maelekezo. Gharama mbalimbali zinaeleweka na taratibu zake za ukiritimba fulani pia! Lakini zaidi yawezekana umechomwa na ukweli kuhusu wizi, uzembe, ulaghai, rusha kwa watumishi wa aridhi. Pole mkuu hata sisi wakulima tukichemka huwa tunakaangwa. Nakutakia utumishi mwema
 
Ni kweli mkuu walinichomoa buku tano kwa ajili ya mhuri, tatizo na wanasheria nao wa serikali wanajiweka mbali na wananchi kiaina

Mkuu Habari za kazi

Mie nilinunua Shamba mwaka juzi ......last year nimeenda kupeleka watu wa kuli survey ili mchakato mwingine ufate...jamaa kuchukua coordinates wakaenda plot wakasaema eneo lote ni la NBC. Wana project yao wanata kufanya sasa sijui lini.

Ila eneo watu wameshajenga na kuweka uwekezaji mwingine...Je nikiwekea na mie nyumba itakuwa ni mbaya? Je ntalipwa kama fidia mwisho wa siku kwa uwekezaji niliofanya pale?

Utaratibu ukoje kuhusu mambo hii?

Natanguliza shukrani.
 
Binafsi nakubaliana na maelezo ya mh.kingkong pia niwakumbushe kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya mwaka 2008 ya sheria ya ardhi no.4 ya 1999 barua ya toleo (letter of offer) imefutwa na badala yake ukishalipia umilikaji kiwanja unapewa uthibitisho wa kupokelewa malipo yaani acknowledgement of payment ambayo kimsingi inakusukuma kufuatilia kuandaliwa hati ya kiwanja chako.

Tofauti na zamani amabapo offer ilikua na nguvu ya kisheria hali iliyopelekea watu wakipata offa wanaridhika na hivyo hawafatilii hati zao na matokeo yake mauziano na mimala mingine inakwama. kwa sasa sheria inaelekeza ndani ya siku 90 ukishalipia unastahili kupatiwa hati yako.

kuhusu hati ya kiwanja na nyumba kimsingi sheria inatambua nyumba kuwa sehemu ya ardhi hivyo inatambulishwa kwa hati ya kumiliki ardhi lakini kama ambavyo uhalali wa umiliki wa kiwanja unatambulishwa na hati (certificate of Title) pia uhalali wa jengo juu ya kiwanja unatambulishwa na kibali cha ujenzi (building permit) hivyo kwa mujibu washeria hati ya nyumba ni muungano wa certificate of title na building permit.

kwa maoni yangu suala la rushwa ni cancer inayotafuna nchi na siyo Wizara ya ardhi peke yao, angalia polisi angalia uhamiaji , cheki tra na bunge letu yaani siyo harufu bali ni uozo wa rushwa.
 
Mkuu!
Bila shaka umekuja vema kbs!

Lakini Mi ckujuaga kama nyumba haina hati. Nashukuru kwa kutujuza hili
kwn wengine tulikuwa giza bado.

kulingana na sheria ya unit tittles sehemu ya nyumba pia ina weza
kupata Tittle, mathalan kila floor kwenye flat ikawa na tittle yake, gharama za kupata hati kwa kiasi kikubwa zina varry kutokana na ukubwa wa eneo na eneo ardhi hiyo ilipo
 
Na wakishachukua GPS kabla ya kupima wanaangalia kwenye ramani ya eneo hilo kama kiwanja chako kipo kwenye maeneo ambayo siyo ya makazi mfano kama kipo kwenye eneo lililotengwa kwa ajili ya hospitali, soko, viwanja vya michezo, nyumba za ibada nk ujue hawatakupimia hiyo imekula kwako.

Nashauri pia wadau wakati wa kununua kiwanja nenda ofisi za ardhi kwanza ili ujue kama hilo eneo ni halali au la! kuna kipindi nilitaka kununua eneo kule gongo la mboto nikamleta jamaa wa ardhi akachukua GPS alipoangalia ramani akakuta ni eneo la soko basi ikawa salama yangu maana nilikuwa na hela zangu kwenye mfuko wa rambo duh..

Mjini kweli shule
 
Wadau naomba mnielimishe utaratibu na gharama za kupata title ya kiwanja kwa maeneo ya Mbezi-Msakuzi(Mpigi Magoye road) na Kitunda kivule...Nasikia ni shughuli pevu lakini kuna haja ya ku accomplish hili, tafadhali nahitaji idea how to start the process and how much should I have in hand for the process..
 
Utaratibu

1. Pata barua ya utambulisho toka kwa mjumbe wako wa shina.

2. Andika barua kwa mkurugenzi wa Halmashauri kumuomba kibali cha kupimiwa (survey) eneo lako. Barua hiyo inatakiwa kupitia ofisi ya serikali ya mtaa na ofisi ya afisa mtendaji kata.

2. Fikisha barua hiyo pamoja na vithibitisho vya umiliki wa kiwanja chako (makubaliano ya mauzo au urithi) kwenye ofisi ya Serikali ya Mtaa pamoja na barua ya kuomba kupimiwa eneo. Serikali ya Mtaa itakukata kodi ambayo ni asilimia 10 ya thamani ya kiwanja. Serikali ya Mtaa itakutengenezea hati ya umili na kukupa ndamba ya kiwanja. Hati hii unaweza kuitumia kulipa kodi ya ardhi kila mwaka.

3. Pitisha barua hiyo ngazi ya kata. Hata hakuna makato zaidi ya "kamchango" kadogo ka ofisi kama sh. elfu 5 hivi. Huwa kuna michango ya shuguli za maendeleo etc kupitia huduma kama hizi.

4. Peleka barua hiyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri. Mkurugenzi atasubiri Baraza la madiwani likae ili kupitisha ombi lako iwapo eneo hilo halipo katika mpango wa matumizi mengine zaidi ya residency etc.

5. Baada ya kupata kibali toka kwa Mkurugenzi, tafuta kampuni ya survey wakupimie na kampuni hiyo itawasilisha ombi la title deed wizara ya ardhi kupitia kwa mkurugenzi.

6. Wizara ya ardhi itakukabidhi title deed iliyokamilika.
 
Back
Top Bottom