Wakuu,
Nina kiwanja ambacho hakijapimwa. Nani anaweza kunifahamisha kuhusu taratibu za kufuatilia hati katika mambo yafuatayo:
1. Taratibu za upimaji (surveying)
2. Makadirio ya muda, tangu umepima hadi kupata hati mkononi
3. Gharama za surveyor na nyingine zote ambazo zitahitajika kulipwa
Pia, kama wewe umeshawahi kupima hadi kupata hati ya kiwanja chako, ntashukuru kama unanishirikisha uzoefu wako.
Kiwanja kipo dar, maeneo ya Mbezi, Tangi Bovu.
Pia, kama unamfaham surveyor ambae sio longo longo (maana hii fani karibu wote ni longo longo), naomba unijulishe.
Natanguliza shukrani
Nyongeza: Kiwanya kina ukubwa wa 20m x 25m