Wakuu, wiki kadhaa zilizopita nilinunua kifaa kutoka nje ya nchi, nimetumiwa mzigo wangu kwa njia ya POSTA.
jana nimetumiwa sms kuwa kifaa changu kimefika, nimenunua kifaa kwa bei ya shilingi, aaah dola 100.
Sasa kabla sijaenda kuchukua kifaa changu nimefanya mawasiliano na mtoa huduma wa POSTA aliyenitumia sms. Mimi nipo nje ya mji, nilimuomba anisaidie kujua gharama za kodi ili nijue kiasi cha pesa nimachotakiwa kwenda nacho kabla sijafunga safari ya kufuata mzigo wangu.
Bila hiyana mtoa huduma amekubali.
MAJIBU SASA: Baada ya mtoa huduma wa POSTA kukubali kunisaidia kuuliza gharama za kodi ninazotakiwa kulipia, amekuja na jibu kwamba ninatakiwa kulipia pesa taslimu shilingi laki moja na thelathini (137000), hii ni pesa za Kitanzania.
Sasa hapa nimebaki najiuliza maswali, hivi ni kweli kitu nilichokinunua kwa dola 100 (sawa na shilingi za Kitanzania 272000) natakiwa kukilipia kodi ya shilingi za Kitanzania 137000?
Watanzania wenzangu, hivi hii ni kweli au kuna makosa sehemu?
Hivi ni kweli serikali yetu imewapa TRA mamlaka ya kututoza Watanzania kodi zaidi ya 50% ya bei tunayonunulia vitu.
Aione!
Chief-Mkwawa