Utaratibu wa kodi baada ya kupokea mzigo Posta ukoje?

Mkuu, nimeagiza kwa kutumia taarifa za mkoa wangu, mkoa wa Pwani, lakini mzigo umezuiliwa Dar.
Wanakuonea, posta wanabanwa na sheria za kimataifa, kama pwan ofisi haina Tra hilo sio kosa lako
 
Mimi nilishangaa siku wananitumia sms nifuate mzigo wangu Dar.
 
Mkuu, nimeagiza kwa kutumia taarifa za mkoa wangu, mkoa wa Pwani, lakini mzigo umezuiliwa Dar.
Du! Hilo sasa kazi mkuu, kuna jamaa ananjaa hapo ndo anataka kukuliza, ukifika lia sana muelewane unaweza toa hata 50K, watanzania kila kitu kinazungumzika ila Pole sana.
Watafanya tushindwe kua tuna agiza online kwa mambo haya.
 
Hiyo pesa ya nauli ambayo nitatumia ilikuwa ndio itumike kwenye kulipia kodi.
Watumishi wa umma wa nchi yetu ni pasua kichwa.
 
Kwahiyo hapo nafanyaje mkuu, kuna ushauri?
Nenda posta yako dai mzigo wako kwa anuani yako ulipo, kama Tra waje hapo pwani,
Kwa sheria za posta ni makosa kuchukua mzigo ulio nje ya anuani yako.
 
Bro upo mkoa gani.. ila huo nenda na 30k
Watoe hapo upewe mzigo wako
Usipende kuwa straight sana utaumia
 
Kuna tatizo katika utaratibu au kanuni ya kukokotoa kodi.
 
Nenda posta yako dai mzigo wako kwa anuani yako ulipo, kama Tra waje hapo pwani,
Kwa sheria za posta ni makosa kuchukua mzigo ulio nje ya anuani yako.
Kwahiyo niende POSTA iliyopo eneo langu, wao watafanya mawasiliano na POSTA ya Dar ili mzigo wangu utumwe?
 
Wangekuchaji kodi elfu30 au 40 ndio ilibidi ushangae, tz ni nchi ya makodi makubwa
 
Kwahiyo niende POSTA iliyopo eneo langu, wao watafanya mawasiliano na POSTA ya Dar ili mzigo wangu utumwe?
Utalipa tena hela ya usafiri, kwani wewe adress uliandika wapi?
 
W
Wanakomoa wanataka..uagize kupitia makampuni Yao binafs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…