Utaratibu wa kubadili majina ya mtoto shuleni ukoje??

Sijui kwa sasa ila zamani kulikuwa na fomu flani hivi ulikuwa unajaza kabla ya kufanya mtihani wa kidato cha nne,,na watu walikuwa wanabadili majina,,,
Huyo mtoto hahitaji fomu ya marekebisho ya majina (Query Circular Form) bali kuingia kwenye mfumo (PREM na kuedit tu.
 
Hii swala imekuwa changamoto,nami limenikuta kwa mtoto wa darasa la sita Mwalimu ameniambia haiwezekani chakunishauri nikwamba nikabadili jina RITA ili cheti chamtoto kiendane na jina lamtoto shuleni..mistek iliyotokea nikwamba mtototo anaitwa SUMA baba anaitwa BAHATI JUMA KINGAZI sasa shuleni aliandikwa kwa majina mawili SUMA BAHAT baadae kwene kuandika majina matatu jina latatu mtoto akawatajia jina la JUMA badala ya Jina la ukoo KINGAZI,kwaiyo shuleni anaitwa SUMA BAHAT JUMA badala ya SUMA BAHAT KINGAZI sasa kwene kulipachika jina la ukoo ndio imekuwa ishu ,tunapoelekea naona atatumia majina Manne kama anko Magu
Sio tatizo kivile mkuu. Kijana amefanya mtihani wa upimaji wa darasa la nne. Kubadili jina itabidi kubadili majina yake yaliyomo kwenye kanzi data ya matokeo yake NECTA ili taarifa ziwiane jambo ambalo ni ngumu.
 
Amesha kua mkubwa hapo ni deed poll, affidavit utapigwa tu lkn haitakubalika
 
Yani mimi nimehangaika sana sana lakini nimeshindwa. Kwasababu mtoto alishafanya darasa la nne,la saba na sasa form 2.
Kiukweli jina limeharibiwa kwa asilimia 95% la yule mtoto.
Nadhani cheti muhimu ni cha form 4,ungekuwepo utaratibu wa kufanya marekebisho ya majina haya kwani yanakosewa sana kusajiliwa na walimu hasa shule za msingi
 
Dah! Nami nahangaika na ishu hiyohiyo, maaana wkt Nesi aliekuwa anaandika jina baada ya Mtoto kuzaliwa alikuwa na tatizo la matamshi, baada ya kuandika Najmah yy akaandika Najimah, sasa ishu kuitoa hiyo i ndio shida na Dogo yupo darasa la3 na keshazoea kundika Najma
Kafanye marekebisho cheti cha kuzaliwa mtoto!, ukipata cheti nenda Shule.
 
Yani mimi nimehangaika sana sana lakini nimeshindwa. Kwasababu mtoto alishafanya darasa la nne,la saba na sasa form 2.
Kiukweli jina limeharibiwa kwa asilimia 95% la yule mtoto.
Nadhani cheti muhimu ni cha form 4,ungekuwepo utaratibu wa kufanya marekebisho ya majina haya kwani yanakosewa sana kusajiliwa na walimu hasa shule za msingi
kitu simple kama hiki nacho kinatushinda watanzania. ni hatari haya malalamiko yako mengi ila sioni tahadhari yeyote kutoka kwenye mamlaka
 
Dah! Nami nahangaika na ishu hiyohiyo, maaana wkt Nesi aliekuwa anaandika jina baada ya Mtoto kuzaliwa alikuwa na tatizo la matamshi, baada ya kuandika Najmah yy akaandika Najimah, sasa ishu kuitoa hiyo i ndio shida na Dogo yupo darasa la3 na keshazoea kundika Najma
ishu yako sio kubwa kihivyo,kama uko dar nenda RITA pale watakurekebishia
 
kitu simple kama hiki nacho kinatushinda watanzania. ni hatari haya malalamiko yako mengi ila sioni tahadhari yeyote kutoka kwenye mamlaka
Yani kitu kinachowezekana kabisaaa kimewekewa ugumu kama kipo kwa Mungu!Why this state aisee?

Waziri wa elimu,tamisemi na NECTA walifanyie kazi haraka.Wadau tuungane tuwafikie wizara husika.

Namna ya kuwasiliana nao mwenye access hata ya namba ya simu ya Profesa Mkenda tafadhari.
 
  • Kicheko
Reactions: Lax

malalamiko wanayo, ni kiburi tu
 
Dah! Nami nahangaika na ishu hiyohiyo, maaana wkt Nesi aliekuwa anaandika jina baada ya Mtoto kuzaliwa alikuwa na tatizo la matamshi, baada ya kuandika Najmah yy akaandika Najimah, sasa ishu kuitoa hiyo i ndio shida na Dogo yupo darasa la3 na keshazoea kundika Najma
Huyo kurekebisha jina inawezekana kabla ya kufanya mtihani wa darasa la nne kikubwa vizia mfumo wa PREM ukiruhusiwa nenda shule ufanye hayo mabadiliko..Akisajiliwa tu NECTA hapo ndiyo basi tena.
 
WKuu
Nina kijana yuko form 3 anaingia form four.
Sasa majina anayotumia jina la katikat siyo sahii nataka nibadili.Shuleni walidai haiwezekani.

Je utaratibu wa kisheria ukoje
Vyeti feki ndo nyie! Utaanzaje kubadili jina la mtoto? Tangu mtihani wa darasa la nne hukuona? Mtihani wa la saba hukuona? Mtihani wa kidato cha pili hukuona? RIP Magufuli
 
Dah! Nami nahangaika na ishu hiyohiyo, maaana wkt Nesi aliekuwa anaandika jina baada ya Mtoto kuzaliwa alikuwa na tatizo la matamshi, baada ya kuandika Najmah yy akaandika Najimah, sasa ishu kuitoa hiyo i ndio shida na Dogo yupo darasa la3 na keshazoea kundika Najma
Darasa la 3 wanabadili, nenda shuleni kwao watakupa maelekezo kabla hawajamsajili necta kwa mitihani ya Drs 4. Wakimsanili tu haubadilishi Tena.
 
Dah! Nami nahangaika na ishu hiyohiyo, maaana wkt Nesi aliekuwa anaandika jina baada ya Mtoto kuzaliwa alikuwa na tatizo la matamshi, baada ya kuandika Najmah yy akaandika Najimah, sasa ishu kuitoa hiyo i ndio shida na Dogo yupo darasa la3 na keshazoea kundika Najma
Cheti cha kuzaliwa ni rahisi kubadili jina RITA au mahakamani! Lakini sio necta!
 
Dah! Nami nahangaika na ishu hiyohiyo, maaana wkt Nesi aliekuwa anaandika jina baada ya Mtoto kuzaliwa alikuwa na tatizo la matamshi, baada ya kuandika Najmah yy akaandika Najimah, sasa ishu kuitoa hiyo i ndio shida na Dogo yupo darasa la3 na keshazoea kundika Najma
kwani cheti cha kuzaliwa mtoto kinatolewa na nesi wa hospitali alyoyojifungulia mama au kinatolewa na RITA...ww mzazi mzembe mtoto hadi anaanza shule anafikisha miaka 9 upo tu...wakati ulikuwa na nafasi kurekebisha tangu mtoto akiwa na miezi sita..lakini mkuu bado una nafasi kurekebisha jina lake sasa hivi kabla hajafanya mtihani wa taifa wa darasa la nne maana majina yao bado hayajaingizwa kwenye mfumo wa mitihani NECTA na kupewa prem number..wahi
 
Majina ya shule hayabadilishwi, usije ukaliwa tu hela zako. Labda kubadili chet cha kuzaliwa hyo inawezekana lkn majina ya shule hua yanabaki hvo hvo
 
Yani mimi nimehangaika sana sana lakini nimeshindwa. Kwasababu mtoto alishafanya darasa la nne,la saba na sasa form 2.
Kiukweli jina limeharibiwa kwa asilimia 95% la yule mtoto.
Nadhani cheti muhimu ni cha form 4,ungekuwepo utaratibu wa kufanya marekebisho ya majina haya kwani yanakosewa sana kusajiliwa na walimu hasa shule za msingi
Sijui kwa utaratibu wa sasa, ila zamani ilikuwa inaruhusiwa kubadili majina yako ifikapo kidato cha pili na kujiita vile wewe unaona inafaa.
Nakumbuka nilisoma na Wandengereko kadhaa waliokuwa na majina kama vile Chozi, Msiba, Matatizo na Shida walibadili na kujiita majina waliyoona wao yanawafaa
 
Back
Top Bottom