Utaratibu wa kubadili majina ya mtoto shuleni ukoje??

Utaratibu wa kubadili majina ya mtoto shuleni ukoje??

kwani cheti cha kuzaliwa mtoto kinatolewa na nesi wa hospitali alyoyojifungulia mama au kinatolewa na RITA...ww mzazi mzembe mtoto hadi anaanza shule anafikisha miaka 9 upo tu...wakati ulikuwa na nafasi kurekebisha tangu mtoto akiwa na miezi sita..lakini mkuu bado una nafasi kurekebisha jina lake sasa hivi kabla hajafanya mtihani wa taifa wa darasa la nne maana majina yao bado hayajaingizwa kwenye mfumo wa mitihani NECTA na kupewa prem number..wahi
Kwahiyo Mkuu unanipa utaratibu na mshahara wa tusi kama nyongeza sio!? Haya Mkuu nimekusoma pia asante
 
Dah! Nami nahangaika na ishu hiyohiyo, maaana wkt Nesi aliekuwa anaandika jina baada ya Mtoto kuzaliwa alikuwa na tatizo la matamshi, baada ya kuandika Najmah yy akaandika Najimah, sasa ishu kuitoa hiyo i ndio shida na Dogo yupo darasa la3 na keshazoea kundika Najma
- Kwako inawezekana. Fuata taratibu, Watarekebisha walimu kwenye usajiri wa Mitihani ya Darasa la 4.
 
Dah! Nami nahangaika na ishu hiyohiyo, maaana wkt Nesi aliekuwa anaandika jina baada ya Mtoto kuzaliwa alikuwa na tatizo la matamshi, baada ya kuandika Najmah yy akaandika Najimah, sasa ishu kuitoa hiyo i ndio shida na Dogo yupo darasa la3 na keshazoea kundika Najma
Hii ya herufi NECTA wanafanya nenda pale ofisini kwao watakusaidia lkn jina jipya Hilo sahau
 
Hii swala imekuwa changamoto,nami limenikuta kwa mtoto wa darasa la sita Mwalimu ameniambia haiwezekani chakunishauri nikwamba nikabadili jina RITA ili cheti chamtoto kiendane na jina lamtoto shuleni..mistek iliyotokea nikwamba mtototo anaitwa SUMA baba anaitwa BAHATI JUMA KINGAZI sasa shuleni aliandikwa kwa majina mawili SUMA BAHAT baadae kwene kuandika majina matatu jina latatu mtoto akawatajia jina la JUMA badala ya Jina la ukoo KINGAZI,kwaiyo shuleni anaitwa SUMA BAHAT JUMA badala ya SUMA BAHAT KINGAZI sasa kwene kulipachika jina la ukoo ndio imekuwa ishu ,tunapoelekea naona atatumia majina Manne kama anko Magu
Kama yupo la Sita nenda ata Necta pale makao makuu waambie au nenda Kwa afisa elimu wilaya na IT wake fasta tu ila akifanya wa la Saba ndo basi
 
Haiwezekani hata iweje utabadilisha Kwa mambo mengine ila necta litatumika ilo ilo kiapo kitakusaidia kwenye mambo mengine Kam bima ya afya lakn necta haibadiliki mm nimetumia majina mawili tangu la kwanza had 4m 4 kuongeza jina tu imeshindikana
 
WKuu
Nina kijana yuko form 3 anaingia form four.
Sasa majina anayotumia jina la katikat siyo sahii nataka nibadili.Shuleni walidai haiwezekani.

Je utaratibu wa kisheria ukoje
Mtoto angekua shule ya Msingi ingekua rahisi, We waambie jina la kati limekosewa.
 
mm nahisi hawa wanaotaka kubadili majina watakuwa ni wale wanaume wakataa mimba au kutelekeza watoto na mwanamke akijifungua analea mwenyewe baada ya aliyemjaza mimba kuingia mitini huyu akija kumpa mtoto jina la ubini anapewa jina la babu au akitokea mwanaume mwingine akamsitiri huyo mwanamke na mtoto wake aliyetelelezwa basi mama mtoto anaweza kubadilisha jina la pili la mtoto akapewa la mwanaume mwingine ambae anamtunza baada ya baba halisi wa mtoto kumtelekeza...baada ya miaka ndio baba halisi anajitokeza anakuta mtoto anatumia jina la ubini usio wake ndio hawa wanaaanza kuhaha mtoto yupo kidato cha tatu eti ndio anajua jina la kati limekosewa yanataka kubadilishwa leo.! ndio najiuliza mtoto tangu anaanza darasa la kwanza hadi kidato cha tatu usione kasoro ya jina la baba kama ulikuwa ukiishi nae..maana yake ulimtelekeza au ulimkataa na sasa ndo umejirudi unataka mtoto awe na utambulisho wako
 
Back
Top Bottom