Utaratibu wa wafiwa kuwalisha waombolezaji wengine umerasimishwa Tanzania?

Utaratibu wa wafiwa kuwalisha waombolezaji wengine umerasimishwa Tanzania?

Kama hujalipenda jibu langu basi lifute ujiandikie jibu unalolipenda wewe halafu ufurahi!

Maana ni very corny mtu unapolazimisha watu watoe majibu unayotaka wewe

Kama majibu tayari unayo kichwani,ya nini umeleta uzi hapa?
Mkuu na wewe unataka ukiwa unaenda msibani unaenda kulishwa?
 
Unanifundisha jinsi ya kuelewa?

Wewe umeandika,kazi ya kuelewa ni yako au yetu?

Wewe nani anakwambia uingilie kazi isiyokuhusu?

Uandike wewe,uelewe wewe,ushurutishe watu wajibu unavyotaka,etc....who the fvck you mzee?
Kazi kweli kweli [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huku kwetu watu wanathamini Sana Kula ila uzuri ni kwamba wanajamii wanachangia Sisi kwetu msiba ulitokea ilibidi madume wachinjwe na ukikaa vibaya unaweza kubakiwa na madeni Kwa sababu mchango wa jamii unaweza usitoshe Kwa sababu watu wanathamini Kula.
 
Huku kwetu watu wanathamini Sana Kula ila uzuri ni kwamba wanajamii wanachangia Sisi kwetu msiba ulitokea ilibidi madume wachinjwe na ukikaa vibaya unaweza kubakiwa na madeni Kwa sababu mchango wa jamii unaweza usitoshe Kwa sababu watu wanathamini Kula.
Yes!,kuchangia ni utaratibu mzuri sana lakini si kwamba familia ya wafiwa ndiyo ibebe mzigo
 
Sisi kabila yetu gharama za hivo vyakula vinatoka kwa majirani wanaokuzunguka ,Kijiji kizima inachanga na usipochanga siku na wewe ukipata shida unatengwa ,hata utaratibu wa kula wale wa mbali ndo wanatangulia ili hata msosi ukiisha wale majirani siyo ishu
 
Utakuta mtu anakuja msibani na rambirambi ya buku lakina anataka buffet ya kuku na mazagazaga mengine.
Misiba inatumika kama sehemu ya kubadilisha diet.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Habari za leo wanajamvi? bila shaka mapambano yanaendelea kama kawaida!
Tuendelee kupambana sana na kusaka michuzi kwa udi na uvumba kana kwamba hatufi, na tuendelee kumuomba na kumwabudu Mungu kana kwamba tunakufa kesho!

Kwanza kabisa napenda kutoa masikitiko yangu kama mwananzengo kwa sintofahamu ambayo imeendelea kuikumba jamii ya kitanzania kwa sehemu kubwa kama si yote.

UMUGHAKA nimekuwa nikijiuliza huu utaratibu wa kipumbavu ni nani/akina nani waliyo urasimisha? Kumekuwa na kasumba ambayo sidhani kama nikiita ni upumbavu/ushenzi kama nitakuwa nakosea.

Misiba mingi kama si yote niliyowahi kuhudhuria, nimekua nikiona utaratibu wa wale waliofikwa na msiba ndiyo ambao wanahaha kuwalisha watu ambao wamekuja msibani kutoa pole/kufariji.

Na lazima niwe mkweli ya kwamba,hata sisi kwetu pia tumepata misiba mingi tu ya ndugu zangu na utaratibu huwa ni huo huo!,hili suala limekaaje wapendwa? Yaani unakuta waliofikwa na msiba ndiyo wanaumiza vichwa namna ya kuwalisha wanaokuja kuwafariji badala ya waliokuja kuwafariji wenye matatizo wao ndiyo ilipaswa wakae wakusanyane wananzengo ili kuwalisha waliofikwa na msiba!

Huu utaratibu ni mbovu sana na siungi mkono kabisa! Ni kwanini tusiwe na utaratibu tunapoenda misibani kuwafariji wafiwa kusiwe na utaratibu wa kuwalisha wafiwa pamoja na watakao hudhuria msibani? Yaani unakutwa watu wengi wanaoenda misibani ni kupiga soga tu na kusubiri kunawishwa wakati wa kula huku wanafurahia maisha kana kwamba ni sherehe.

Watu wengi wanaenda misibani si kufariji bali kupiga soga na kula!,huu ndiyo ukweli ukubali au ukatae!

Yaani mtu amefiwa na mpendwa wake halafu bado aumize na kichwa namna ya kuwalisha wananzengo!,hii kitu iko sawa kweli?,hivi hizi nguvu unadhani atakuwa nazo?,hii imepelekea hasa watu wenye kipato cha chini wanabaki kusimangwa na wananzengo hata bila aibu!,unakuta kabisa majirani wanaongea " Msiba wenyewe hata vyakula hauna,naona watu wamechungulia tu wamesusa",kabisa?

Lakini misiba ya watu wenye uwezo utasikia "Jamaa wanapika vyakula vizuri asikwambie mtu,unakula mpaka unasaza".

Hata kama mfiwa anao uwezo,ndiyo alishe wananzengo badala ya wananzengo kumlisha yeye?.

JE,huu utaratibu ni nani aliyeuanzisha?

Je,makabila yote ya Tanzania hufanya hivi?

Wenzetu mliotembea tembea huko ughaibuni,je hali huwa iko hivi kama huku kwetu.

Unakuta "Mijitu" inaenda misibani kwa ajili ya kula tu,ikishakula hiyoooooo inalala mbele!,hata aibu haioni!,unakuta jitu badala liende hata ndani kusalimia wafiwa lenyewe linakomea getini linapiga msosi halafu linalala mbele!!

HUU UTARATIBU HAUKUBALIKI

#USIPOBADILIKATUTAKUBADILISHA
#TIGHABHATEMWE

Huo ni utaratibu mbovu sana. Ila taratibu ya ukweli ni kila mgeni mwenye uwezo kunakuwa na daftari unachangia kiasi unachoweza kutokana na uwezo wako.

Huko nyuma wengine walileta magari, yao, nyama, ngombe, wapikaji, mchele, Waimbaji (wafariji), wachimbaji wa kaburi nk.
 
Kwa waislamu swala la ndowa na mazishi dini yao imewapa maekekezo mazuri sana.

Hizi shida waachieni wakristo lakini kwa mwislamu kupata shida hizi ni kujitakia.

Dini ya kiislamu inaelekeza mtu akifa azikwe haraka.

Familia haiwezi kuumia kwa kuwapikia uji na sukari inatosha kabisa, mambo ya catering waachieni wakristo.
Shida misiba ya kariakoo wanafunga mtaa na biliani ya kufa MTU tena basmat kabisa afu ikafuatia mitaa ya Ilala, magomeni na Sasa hadi Tandale humnywishi MTU ule uji wa mchele kwenye kifuu.
Jingine wameiga hadi mambo ya sare misibani
 
Umefiwa unaulizwa kuni ziko wapi *****,wakat wa kuuguza ulkuwa peke yako na unakuta umetumia gharama kbao,dunia haiko fair
 
Back
Top Bottom