Utata kifo cha Afisa Usalama Kijitonyama

Utata kifo cha Afisa Usalama Kijitonyama

hata hayo majibu ya uchunguzi waliyoahidiwa 'yatatengenezwa ' , Ushahidi wangu wa kimazingira unaonyesha bila shaka yoyote kwamba 'ameshughulikiwa '! Pole Mama Mjane uliyeachwa .

kama wamemshughulikia waliomshughlikia watasema nini kwa mungu wao siku atakapowaita?au ukishakuwa tiss unnminishwa hakuna mungu.
 
wewe utakua huijui uwt machizi wa kiukweli wako kibao na system hiyo hiyo(kazi) ndo imewafanya wa creck

is that so?then tiss job is one of most difficcult jobs in the world.but is it supposed to be so?
 
pamoja na haya yote yanayosikika na kusomwa bado kuna wenzangu na mie wanalilia hii kazi mpaka kesho...si bure :der:
 
Ndio mambo ya watawala na watawaliwa! Kwani kumfukuza kazi au kumpotezea kama Balali hakutoshi mpaka auliwe? So sad!
 
Huo mwili wameukaguwa kucha na meno? sidhani hivyo viungo kama vilibakizwa mwilini mwake.
 
Mwisho wa maisha ni kufa. Hivyo siku yake ilifika. hakuna haja ya kutafuta mchawi
 
Wote tutakufa kufiiiii uwe na cheo usiwe nacho, uwe tajiri/masikini, uwe na akili, uwe na phd/hujasoma kabisa mavumbini tutarudi iwe kwa ajali/ugonjwa/kuuliwa/kuuwawa/kujiua...KWA yeYOte aliyeua/au kushiriki Kuua hata isipojulikana hadharani DHAMIRA YAKO HAITA KAAA iwe na utulivu Kamwe Hadi Utakapoonja mAUTI...Damu ya mwenzio itakulilia siku zote...RIP afisa usalama
 
SERIAL DEATHS OF SPIES IS NOT SOMETHING UN-USUAL ,ITS ONLY THIS WEEK THAT WE LEARNED THAT IT WAS IMRAN KOMBE INFACT WHO ORDERED MORINGE SOKOINE"S PERSONAL BODYGUARDS TO HEAD TOWARD MONDULI INSTEAD OF ACCOMPANY HE FORMER PREMIER TO ROAD TRIP TO DAR......FEW PEOPLE KNOW THAT WHEN IMRAN WAS KILLED HIM AND HIS WIFE WERE ON THE WAY TO FLEE THE COUNTRY TO CANADA AFTER SMELT FISH....ON HIS ROLE AHEAD OF 1995 ELECTIONS...
.....THE THEN DEATH OF ANOTHER SPY THIS WEEK IN THERE COMPOUND ...IS NOT SOMETHING NEW...TWO YEARS AGO FORMER CHIEF JUSTICE BOARDGUARD WAS FOUND DEAD ..IN SUSPECTIVE ENVIRONMENT..IT WAS QUICK COVERED ....
WE DONT KNOW THE REASON FOR YET AGAIN THIS LATEST ONE....ONE THING IS WE ARE NOT SUPPOSED TO WASTE OUR VOICES SINCE IN SPY PROFFESSION THERE IS A PRICE TO PAY WHEN YOU ARE CONSIDERED A THREAT A TRAITOR ....WHO KNOWS ...MAY BE THIS IS A MESSAGE TO SPIES INVOLVED IN RECENT LEAKAGES .....,
COMING ACROSS ANY TOP SECRET IS ANOTHER REASON TO DIE ..PASSIONATELY IF YOU ARE CONSIDERED NOT STRONG ENOUGH TO KEEP SECRET....

THEY WERE SWORN TO DIE THESE KIND OF DEATHS ....SO FOR LOVED ONE BURY YOUR DEAD ..YOU HAVE NOTHING TO ASK !!!!! LIFE GOES ON!!



and their rules states as follows:
Assume nothing.

Never go against your gut.

Everyone is potentially under opposition control.

Don't look back; you are never completely alone.

Go with the flow, blend in.

Vary your pattern and stay within your cover.

Lull them into a sense of complacency.

Don't harass the opposition.

Pick the time and place for action.

Keep your options open.



 
hii kazi ni ya nidhamu ya hali ya juu, ila tukio kama hili la karibuni linatisha, hivi hii si inaleta uoga kwa wale watakaohitajika kufanya kazi huko na tunaweza badae tukakosa 'human resource'?
 
haya bwana mimi ngoja nijikunyate mikononi mwa MUNGU hakuna binadamu wa kulinda usalama wangu ,
 
kifo na uhai ni vitu visivyoweza kutenganishwa ukiwa jasusi. mengi yatasemwa sana lakini marehemu ndiye aliapa kufia huko. Ukishaingia huko ndugu hawana mamlaka ya kuihoji jamhuri na ndio maana ya kiapo. Huko unaweza kufa kwa kifo cha kawaida au kufa kiutata kama utakiuka kiapo. Jamaa yangu aliyeko huko anasema huyo jamaa alikuwa na matatizo ya akili na alikuwa kwenye matibabu kwa muda mrefu hata ndugu zake wanafahamu kuwa Idara hiyo ndio ilikuwa inamtibu tangu apate tatizo hili hadi kifo chake. Kifo hicho kinahusishwa na tatizo hilo. Na akasema ndio sababu marehemu alifia katika kisima cha hospitali akiwa katika mwendelezo wa matibabu.

Mkuu hata mimi nilikuwa nafikilia kwenye line hiyo hiyo, kwamba labda jamaa alikuwa matatizo ya akili; tukumbuke TISS ni ma-Prof, hawa wezi kufanya mambo yao ki-amateur namna ile.
 
Kazi ipo nchi inabidi ifumuliwe upya iundwe upya kuna ombwe kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
 
bADO WALE WALIOKUTWA KWENYE SIMU NA MAWASILIANO NA RWAKATARE WAKATI WA KUMKAMATA. KWELI HII KAZI SIO KABISAA!!! EEE MUNGU EPUSHIA MBALI!
 
Jason bouney jitokeze kwenye jukwaa, maana wasiwasi umeanza kuwaingia wanajukwa kuwa kuna uwezekano we ndo ukawa huyo afisa usalama, kwani mara ya mwisho kuingia humu ni tar 27.05.2013 siku ambayo afisa usalama alipotea. Tutoe waswas bro ingia jf
 
HIVI NDIVYO AFISA USALAMA WA TAIFA ALIVYOUWAWA KIKATILI NA KUZAMISHWA NDANI YA KISIMA CHA MAJI HUKO KIJITONYAMA...!!



Tuesday, June 4, 2013 | 12:18 PM






AFISA Usalama wa Taifa, Peter Patrick Tyenyi ,53, ambaye maiti yake ilikutwa Mei 27, mwaka huu katika kisima cha maji masafi kilichopo maeneo ya ofisini kwao, Kijitonyama Makumbusho jijini Dar, kifo chake kimetajwa kuwa ni cha kimafia.

Chanzo chetu makini ndani ya familia ya marehemu kimedai kuwa wao wanaamini kuwa ndugu yao hakufa kifo cha kawaida isipokuwa kuna mkono wa mtu.
Wanafamilia hao wanadai kuwa kifo hicho ni cha kimafia kwa sababu kisima kilichokutwa mwili huwa siyo rahisi mtu kuingia bila kuonekana.
Habari zinasema siku hiyo ya kutoweka kwake, asubuhi afisa huyo alitoka nyumbani kwake maeneo ya Kijitonyama akiwa na afya njema.
umafia.jpg

Kiliendelea kusema kwamba mara baada ya afisa huyo kufika ofisini, walikaa kikao cha kazini na mara baada ya kumalizika hakuonekana tena.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa ofisa huyo alitafutwa kwa njia ya simu baada ya kutoonekana ofisini kwa saa kadhaa lakini zote zikawa hazipatikani.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wafanyakazi wenzake waliingiwa na hofu kwa vile haikuwa kawaida yake kuondoka ofisini bila kuaga na hakuwa na tabia ya kuzima simu zake zote.
Habari zaidi zinaeleza kuwa kutoonekana kwa marehemu kwa saa kadhaa, kuliwafanya ndugu zake wapigiwe simu na maofisa wa idara ya usalama wa taifa kuulizwa na ikabidi wafike ofisini kwake ili kupata taarifa kamili.
UMAFIA3.jpg


Inasemekana kuwa mara baada ya ndugu hao kupewa taarifa hizo waliingiwa hofu, hali iliyowafanya waanze kutembelea baadhi ya hospitali za hapa Dar lakini hawakufanikiwa kupata taarifa zozote kuhusu ndugu yao huyo.
Wakati ndugu zake wanaendelea kumtafuta kwa siku za Jumanne na Jumatano, zikapatikana taarifa kuwa kuna mwili umeonekana katika kisima cha maji masafi kilichopo maeneo ya ofisini kwake.
Imedaiwa kuwa siku ya Alhamisi ambayo mwili ulionekana, maji yalikuwa yamekatika na mmoja wa wafanyakazi wa idara hiyo alikwenda kwenye kisima hicho ndipo alipouona mwili na kutoa taarifa kwa uongozi.
UMAFIA4.jpg


Imeelezwa kuwa baada ya uongozi kupata taarifa hizo, walienda kushuhudia na kuutambua kuwa ni wa Tyenyi.
Mwili huo ulikutwa ukiwa umeharibika na ulichukuliwa hadi Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania, Lugalo.
"Ndugu wa marehemu ilibidi wapewe taarifa ambapo walifika alipokua akifanyia kazi kisha kwenda Lugalo na kuutambua mwili," kilisema chanzo hicho.
Mwili huo ulifanyiwa uchunguzi (post mortem) na wanandugu waliruhusiwa kuuchukua tayari kwa mazishi.
Muda wote kabla mwili haujasafirishwa kwenda Musoma kwa mazishi, msiba ulikuwa kwa mdogo wake aitwaye Julius Patrick, Kigamboni.
Kwa mujibu wa familia kupitia kwa Julius, mwili ulisafirishwa kwa ndege Jumamosi asubuhi ya wiki iliyopita na kuzikwa siku hiyohiyo jioni lakini majibu ya uchunguzi hayajapatikana.
UMAFIA5.jpg

Marehemu ameacha watoto watatu na maofisa wa polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini wakasema msemaji ni mkuu wao, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela.
UMAFIA6.jpg

ACP Kenyela alipopigiwa simu alithibitisha kutokea tukio hilo.
"Ni kweli mwili wa marehemu ulikutwa kwenye kisima chao lakini upelelezi bado unaendelea," alisema Kenyela.




Read more: HIVI NDIVYO AFISA USALAMA WA TAIFA ALIVYOUWAWA KIKATILI NA KUZAMISHWA NDANI YA KISIMA CHA MAJI HUKO KIJITONYAMA...!! - GUMZO LA JIJI
 
Jason bouney jitokeze kwenye jukwaa, maana wasiwasi umeanza kuwaingia wanajukwa kuwa kuna uwezekano we ndo ukawa huyo afisa usalama, kwani mara ya mwisho kuingia humu ni tar 27.05.2013 siku ambayo afisa usalama alipotea. Tutoe waswas bro ingia jf

Wakuuu Kama Jason hatajitokeza hadi Ijumaaa.....tuanze kuwa na mashaka kuwa huyu ndie Mpiganaji Peter Tyenyi.........
katika hali ya kawaida huyu jamaa Angesha update ziara ya Rais Singapore inayoanza Kesho......

Naomba wote tuendelee kumfuatilia isije Ikawa tumepoteza member.....

Still.....searching .......>>>>>>>>>>>

Wenye taarifa Zaidi waziwekee.....ili Kama yupo ajitokeze...

What a coincidence jamaa alipotea na kufa Muda unaoendana na wa huyu jamaa kuonekana hapa..????
 
Back
Top Bottom