Utata kifo cha Afisa Usalama Kijitonyama

Utata kifo cha Afisa Usalama Kijitonyama

mungu aiweke roho yake peponi...hii taarifa ipo hapa wiki sasa kwa thred tofauti tofauti au kuna kitu kinatafutwa???
kila jukwaa ukienda ipo
 
icon1.png
Mbeya: Ofisa Usalama auawa kinyama!

MMOJA wa wasisi wa idara ya usalama wa taifa enzi za ukurugenzi wa hayati Emil Mzena, mzee Joseph Mwasokwa ameuawa kwa kuchinjwa usiku wa kuamkia leo jijini Mbeya.

Chanzo hakijajulikana.

Hayati mzee Mwasokwa atakumbukwa kwa uchapa kazi wake mahiri, wakati huo akiwa na akina mzee Kayugwa, mzee kiliwa mzee Adam Kilumbi, Mzee Shekalage, Mzee Lymo, Marehemu Amir Koyamba, Mzee Kashinde, Mzee Kisesa, Mzee Said Mawele, marehemu Mzee Mahmood Issa, marehemu mzee Ijagala, Mzee Bwimbo [upande wa PSU], mzee Kalumanga NA WENGINE WENGI.

BWANA AMETOA BWANA AMETWAA

*************
More details:

- Mwili wa marehemu ulikutwa getini kwake, maeneo ya Block T jijini Mbeya.
- Marehemu alikuwa ameenda jirani kuangalia mechi ya mpira
- Marehemu alikutwa na $200 na TShs 100,000 hivi na vitu kama saa, simu n.k ambavyo havikuchukuliwa
- Hakuna uhakika kama aliuliwa palepale getini kwake au aliuawa mbali na mwili kutupwa getini kwake

Habari imeandikwa kwa kirefu zaidi hapa - Ofisa Usalama wa Taifa auwawa kwa kuchinjwa kinyama Mbeya | Fikra Pevu

one of his post..
 
Ukiua kwa panga na wewe utauawa kwa upanga, huwa wanajisahau wanapopata nafasi.
 
Poleeni kwa wote na wanafamiliya wapate farji na subira kuhimili msiba huu wa kusikitisha.

Siye niviumbe tumekuja na tutarudi kwa Mwenyeezzi Mungu.
rambirambi zetu.
 
Huu uandishi wa kizuzu-magic bwana. Hayo ni maelezo mbona ni mtiririko wa mambo yalivyokenda na hayana uhusiano wowote na kichwa cha habari!
 
Inside job.... useremala wa taifa at their best..
 
wakiambiwa idara imechafuka wameasi,hawaaminiani,kuna mamafia na wafia nchi kati yao Zoka huwa anakataa aseme sasa manake hatusikii polisi wanafuatilia au nani na nani anahojiwa au usalama wa taifa kufa kwa kubinywa kwenye visima vya maji ni halali yake duh nchi hii
 
Mwili huo ulifanyiwa uchunguzi (post mortem) na wanandugu waliruhusiwa kuuchukua tayari kwa mazishi.................................... lakini majibu ya uchunguzi hayajapatikana

Hadithi za usalama wa Taifa zinanichefua sana, unaweza kukuta na yeye ni mmoja wa wanausalama ambao inadaiwa wamechoshwa na jinsi usalama wa Taifa unavyo fanya kazi zake hivyo kudaiwa kuanza kutoa siri za Serikali kama zinavyoibuka hizi siri za Youtubes ya lwakatare, kuforward ma e-mail ya akina michuzi n.k
 
Ni Mtu MJINGA tu ndiye anaweza kuua kwa njia hiyo halafu akajindanganya ameficha ushahidi. Kujua hilo kwa kufanya post motern ni rahisi sana hata kwa MD 4.

Mtu aliyekufa kwa kutumbukia kwenye maji ukimfanyia post moterm mapafu yake yanakuwa yamejaa maji.

Mtu aliyeuawa (akiwa hayuko majini) halafu akatumbukizwa majini (kisima) baada ya kuuawa mapafu yake yanakuwa hayana maji.
 
Huyo atakuwa walimpeleka quater guard au torture chamber ..kutakuwa kuna kosa alifanya ....la kiutendaji....huenda hawakuwa na nia afe ..labda gwaride likawa gumu!!Nashangaa kwa nini wakakubali kuonesha amefia kisimani ...inaonekana sikuhizi TISS hakuna smooth operators ......la sivyo angetakiwa tu akutwe Mortuary...na msg tu kuwa aliokotwa barabarani ....Taarifa kama hizi kwa kipindi hiki sio nzuri zinaleta tension bure bungeni ..... unless alikuwa anauza siri na wametaka kutuma message kwa waliokuwa wakimtuma na wengine wenye tabia kama zake
mzee unaonyesha ww nimtaalamu, hizo mbinu ulizotoa hapo hauko mbali na hao jamaa.
 
Mtume Lasul! Hakyanani sikujua kama jf kuna mainteligencia kiasi hiki! kila wazo linalotolewa humu kuhusiana na tukio ni sahii kabisa!


...usiogope hawa vijana woote wamefuzu intelijensia shirikishi,so kukusanya udaku sio ishu sana kwao....
 
...usiogope hawa vijana woote wamefuzu intelijensia shirikishi,so kukusanya udaku sio ishu sana kwao....
Manake mimi nilidhani wanaishia kwenye polisi ya kijamii tu, kumbe mpaka huku ushirikishwaji upo?!
 
Back
Top Bottom