Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Swala ni haijulikani waliomchukua na ingefahamika tungejua aliko kama ilivyokua kwa Nay istoshe haieleweki sababu ya kuchukuliwa

Ndio maana wameenda kutoa taarifa polisi,polisi ndio watatueleza ni nani aliewachukua.
 
Magufuri umepewa ridhaa ya kuongoza nchi. ......sio fikra za watu na uhuru wao.
 
Kwani huyo Roma ndio nani? na anajishughulisha na nini? mbona mnapenda kutafuta Kiki kwa Serikali kibwege bwege hivi. leteni vitu vya msingi watu wamchukue Roma waende nae wapi? kama ndieyule mwanamuzi anaeimba nyimbo zinazokaa wiki moja watu hawazikumbuki tena, kama kuimba kuna watu waliimba wa bongo flava mpaka leo nyimbo ikipigwa bado inamaana ije kuwa nyimbo zenu kama pipi ukimung'unya inakwisha.
Haters waga awakos
 
Sakata linguine, kazi kweli kweli
 
Kama kazi waliyobakiza ni kamatakamata na kauli tata viwanda tusahau kabisa, mwenye nia ya kuleta maendeleo hawezi kudeal na vitu vidogo kama hivyo. Yesu aliponya vipofu, viwete hadi akafufua wafu lakini walimkosoa. Sembuse binadamu?!...
 
  • Thanks
Reactions: y-n
wanataka wasikosolewe iwe kama bendi za zaman walivyokua wakiwapamba viongozi,nchi, Radio Tanzania na mikoa....leo Roma akae aimbe kama zile za eti,jamani Morogoro morogoro hooh,.Ile ni enzi zile TV anamiliki mukulu pekee sasa hivi njia za kujua madudu ziko nyingi.
 
Naona watoa comments Karibu wote tuna mawazo kuwa Roma na wenzako wamechukuliwa na Serikali kitu ambacho ni hisia tu kisa Roma ana nyimbo za kuikosoa Serikali.

Jamani tuache huu mzaha ktk maisha ya watu kwani kuna wahalifu wanaweza kutake advantage ya UJINGA wetu kila anayepotea au kutekwa kufikiria ni Serikali wakati huna hata ushahidi wowote then wakafanya mengi mabaya kwa faida zao.

Hili tuliachie mamlaka husika watupe nini kilitokea na juhudi ni zipo za kuwatafuta.
 
Wakitoka kwa wasanii wanaenda wapi sasa? maana huku walisha pita
-Wafanyabiashara
-Vyombo vya habari
-Upinzani
-
-
-
Bado ww Na mwenye nyumba hamuishi kihalali![emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hivi kura tuliwapigia kwa amani mbona malipo ndio haya jamani hayo mambo tulizoea kuyaona kwa wasomali huko na alshabaab yao miungu watu tutakufa sote ni swala la mda tu watangulizeni wenzenu zamu yenu yaja kutwa makanisani kumbe mbwa mwitu wakubwa [HASHTAG]#free[/HASHTAG] roma
 
Habari wakuu nimekuta bandiko katika ukurasa wa Prof. Jay kuhusu kukamatwa kwa msanii ROMA na kuchukuliwa kwa baadhi ya vitu vya studio ya Tongwe record sijui ni kiki au kweli? Mwenye kujua kinachoendelea

=======

View attachment 491832
Baada ya kuzagaa kwa taarifa kuhusu kukamatwa kwa Msanii Roma Mkatoliki akiwa studio na kupelekwa kusiko julikana, Muungwana Blog imefika katika studio za Tongwe Records jijini Dar es salaam ambapo mkasa mzima ulikuwa hivi...

Kwa mujibu wa Mashuhuda (Majina yanahifadhiwa) walio ambao pia wanaishi katika nyumba ambayo inapatikana studio ya Tongwe, wameijuza Muungwana kuwa April 5, 2017 ambayo ilikuwa ni jana, katika majira ya Saa moja jioni ilionekana gari aina ya Noah nyeusi nje ya studio hizo, ambapo walishuka watu zaidi ya Watano na kuingia ndani ya studio hizo.

Watu hao bila ya kujitambulisha walitamka kuwa wanamuhitaji Roma na mwenzake ambapo walimchukua na kutoka nae nje, na baada ya muda kidogo walirejea ndani na kuwachukua wengine watano akiwemo na Prodyuza wa studio hiyo Anayeitwa Moni.

Mbali na kuwachukua watu hao pia mashuhuda hao wemeeleza baadhi ya vifaa vya studio hiyo pia vimebebwa ikiwemo TV, na Computer.

Kwa Mujibu wa Mwanasheria wa Studio hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Edin ameiambia Muungwana Blog kuwa nikweli tukio hilo limetokea na mpaka sasa hawajui Roma na wenzake wamepelekwa wapi na hivyo hawezi kuelezea zaidi mpaka atakapojua walipo wakina Roma, ambapo aliongeza kuwa anakwenda kuripoti katika kituo cha polisi cha Oysterbay Jijini humo.

Chanzo: Blogs
Unapeleka kesi ya nyani kula mahindi kwa tumbili. Unategemea nini
 
Back
Top Bottom