Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

producer anaitwa bin laden wasanii ni Roma na monii.....point of correction monii sio producer
 
Ukiingia YouTube kuna ngoma inaitwa utawala wa kimabavu, haujulikani umeimbwa na Nani. Mwenye kujua anijuze
 
Mambo ya Bashite. Ccm wanahaha.
Ndiyo madhara ya kutaga hayo. Nay wameanza kumtishia maisha naye
 
Naona wamesikitika kuwa walimchelewa "WAPO" na sasa wanashindwa kuizuia.Wanavyomjua Roma,bhasi wameamua heri Shari Kamili kuliko nusu shari. Mkono wa Fe5+ huo!!
 
Tulikuwa tunayasikia Cuba, Russia, China Turkey, North Korea sasa yapo mlangoni mwetu. Jiandae, kaa chonjo wa kutafuta hifadhi anza sasa hujachelewa, wakuingia kwingine mtajiju. Mliyataka wenyewe na mlimchagua wenyewe. Waliomchagua lakini wapo na raha wanapewa ukatibu mkuu na wengine ubunge na u DC na u RC. Je ndugu zao wanafaidi nao kama wao? Tafakari na hao wanaoandika kila siku mitandaoni eti huyu ndo anafaa, kweli? kufunga watu midomo. Wacha watu waropoke wakichoka si wanalala?
 
Habari wakuu nimekuta bandiko katika ukurasa wa Prof. Jay kuhusu kukamatwa kwa msanii ROMA na kuchukuliwa kwa baadhi ya vitu vya studio ya Tongwe record sijui ni kiki au kweli? Mwenye kujua kinachoendelea

=======

View attachment 491832
Baada ya kuzagaa kwa taarifa kuhusu kukamatwa kwa Msanii Roma Mkatoliki akiwa studio na kupelekwa kusiko julikana, Muungwana Blog imefika katika studio za Tongwe Records jijini Dar es salaam ambapo mkasa mzima ulikuwa hivi...

Kwa mujibu wa Mashuhuda (Majina yanahifadhiwa) walio ambao pia wanaishi katika nyumba ambayo inapatikana studio ya Tongwe, wameijuza Muungwana kuwa April 5, 2017 ambayo ilikuwa ni jana, katika majira ya Saa moja jioni ilionekana gari aina ya Noah nyeusi nje ya studio hizo, ambapo walishuka watu zaidi ya Watano na kuingia ndani ya studio hizo.

Watu hao bila ya kujitambulisha walitamka kuwa wanamuhitaji Roma na mwenzake ambapo walimchukua na kutoka nae nje, na baada ya muda kidogo walirejea ndani na kuwachukua wengine watano akiwemo na Prodyuza wa studio hiyo Anayeitwa Moni.

Mbali na kuwachukua watu hao pia mashuhuda hao wemeeleza baadhi ya vifaa vya studio hiyo pia vimebebwa ikiwemo TV, na Computer.

Kwa Mujibu wa Mwanasheria wa Studio hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Edin ameiambia Muungwana Blog kuwa nikweli tukio hilo limetokea na mpaka sasa hawajui Roma na wenzake wamepelekwa wapi na hivyo hawezi kuelezea zaidi mpaka atakapojua walipo wakina Roma, ambapo aliongeza kuwa anakwenda kuripoti katika kituo cha polisi cha Oysterbay Jijini humo.

Chanzo: Blogs
tatizo nini jaman
 
Itakuwa kuna ngoma mpya iliyokuwa inarecordiwa iliyolenga kumkosoa mtu "fulani"!
Ngastuka.
 
Hii ya mbona mimi naona kama imekaa kiki kiki hivi au wadau mnaonaje maana haieleweki ''''''Wasanii watatu ambao ni Roma, Monii Central Zone, Bin Laden pamoja na Imma ambaye ni mfanyakazi wa Mama mzazi wa mmiliki wa studio za Tongwe Records J Murder, mpaka muda huu hawajaweza kupatikana na haifahamiki wapi walipo baada ya kuvamiwa studio na kuchukuliwa na watu wasiojulikana.'''''

sasa mmiliki anachosema'''''
Muda mchache, J Murder ameeleza kiundani juu ya tukio hilo ambalo binafsi anadai limemshtua sana, wakati akihojiwa na watangazaji Chris Bee na Fredoo kupitia kipindi cha The Splash kinachoruka redio Ebony FM.


“Sijui kisa ni nini kusema ukweli kwa sababu mimi studio sikuwepo ila kitu ninachojua mimi ni kwamba walikuja watu pale na gari aina ya Noah wakamhoji Roma baada ya hapo wakawahoji na watu wengine halafu nasikia wakaingia studio nakujukua baadhi ya vifaa” amesema J Murder.


“Baada ya hapo wakaondoka na wasanii wangu, amechukuliwa Roma, Monii, Bin Laden pamoja na mfanyakazi wa mama angu anaitwa Imma, mpaka sasa hivi hatujui wako wapi namba zao zinaita lakini hazipokelewi wakati wakivamiwa kulikuwa hakuna ulinzi walikuwepo wasanii hao na majirani ambao ni mashabiki wa studio,” ameongeza J Murder.


Mapema leo Mmiliki hiyo wa Tongwe Records alifika kituo cha Polisi Osterbay na anaendelea kutujuza kilichomfikisha pale. “Jana usiku baada ya kutokea tukio nilienda kutoa ripoti pale polisi Osterbay kwahiyo leo nilichoenda pale ni kujua mpelelezi wa kesi yangu ni nani nimpe maelekezo wa vitu gani vime-happen pale studio.”


“Nachowaambia mashabiki wa Tongwe, kwamba tuwaombee ndogu zetu akina Roma, Monii, Bin Laden na mfanyakazi wetu Imma wawe salama maana hatujui wako wapi, mali si tatizo tatizo ni watu wangu kwanza mali zinanunuliwa lakini huwezi kununua roho ya mtu,” amesisitiza J Murder.


sasa hapa ndio ninapoona ni kiki maana obey hawapo by tha way ni mawazo yangu tu aisee ila kama kweli basi NCHI IMEFIKIA KUBAYA NA KUNA KINOAH HAPO KATIKA MAELEZO NA STORY ZA NOAH BANA...........
 
Back
Top Bottom