Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara



Rapa Roma Mkatoliki ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Usimsahau mchizi' amekamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana.

Katika taarifa iliyotolewa na msanii Prof. Jay ambay pia ni mbunge wa Mikumi inasema msanii huyo alikamatwa jana akiwa studio.

Prof. Jay ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa jana wakiwa studio za Tongwe Records.

"Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua computer ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi"aliandika Prof. Jay

Mpaka sasa bado hajafahamika wasanii hao wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi.

Lakini watu kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.
 
Ma RPC wote wamesema hawana habari za Kukamatwa kwa msanii Roma Habari hizi zilitolewa na Msanii Joseph Haule Zilisema ROMA alikamatwa katika studio Tongwe hizi huwa zipo Dar es Salaam.

Usimsahau Mchizi ROMA na Ben Saanane.
 
Huyu Nae baada ya Ney kuhit vyombo vya habari na yeye anajaribu kete yake [emoji23]
 
Inaonekana hyo project aliotaka kuitoa roma ingeua hahahahahha wameshtuka mapema stupid
 
Mmmmh nilikuwa na singo yangu ila ngoja nishushe pumzi.
 
Kitengo baada ya kutfta mafisadi na kufufua uchumu wa kitelegensia wanahangaika na wabana pua stupid
 
Ma RPC wote wamesema hawana habari za Kukamatwa kwa msanii Roma Habari hizi zilitolewa na Msanii Joseph Haule Zilisema ROMA alikamatwa katika studio Tongwe hizi huwa zipo Dar es Salaam.

Usimsahau Mchizi ROMA
bashite in action
clauds
nape
wapo
roma ........................


endeleeni kumchekea naona anazidi kuota mapembe
 
Itakuwa wamekamatwa kwa maagizo ya mvamizi Daudi Bashite. Asije tu akawaweka jela miezi sita bila kwenda mahakamani kama alivyowatisha vijana wa Clouds
 
Huyo amejiteka tuu kutafuta kiki...ROMA anatekwa kwa sababu gani hasa? ana nini cha kumtisha mtu yeyote nchi hii?
Ni nani aliona Roma akikamatwa? Ni nani aliona Roma akitekwa?
Huu ni uzushi tuu....
 
Back
Top Bottom