Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Acheni lawama za kpuuzi kwan kuna watanzania wwngap wanakamatwa mnanyamaza? au mnasema kwa wale ambao mna maslah nao....
 
Mkuu Malawi hawawezi kuyapiga haya majambazi sugu, labda uwepo msaada mkubwa Sana wa taifa kubwa ndo Tunaweza kukombolewa.

Mhm, ,,,kweli watu mmechoka aisee,,,nimeamini mara zote watawala ndio huwa wanasababisha wasaliti wa nchi zao,,,,ila tuombe yasifikie hayo, ,, Mi naamini haya yanayotokea M/mungu anataka kuleta kudra zake,,,,,hata Firauni na kaumu yake walitesa sana wana wa Israel hadi kufikia kuwachinja wana wao wakiume, ,,,,LAKINI mwisho wa siku Firauni aliangamia na majeshi yake,,,,,,UNAWEZA ukachukia jambo kumbe lina kheri ndani yake,,,na unaweza ukalipenda jambo kumbe lina Shari kubwa,,,,; Iko siku M/mungu atawaondolea utawala dhalimu wale wanaokandamizwa
 
Hatuna taaarifa kama n police na kama ni police huyo roma.n kama mtanzania yeyote yule anayekamatwa na kuhojiwq so sion tatzo lolote mbona weng kitaaa wanakamatwa mbona hamsemi? hao huyo roma ndo ana roho wengne hawana??
 
imefikia hatua sisi wabongo tunaona ni kawaida mtu akitoweka ghafla/ kupotea au kukamatwa na watu wasio julikana, tunaona ni kawaida tu wakati zamani mfano mzuri huko vijijini watu walikuwa wana organize na kuanza kumtafuta huyo mtu kila kona. Tubadilike jamani kama police wamekana hawajahusika kumkamata Roma na Wenzake basi tutumie mtindo kama nilivyo eleza hapo juu.
Mkuu Swizzy umeandika kiurahisi rahisi lakini kuna hoja kubwa sana hapa.
Niliona clip ya Mh. Tundu Lissu (MB) pale Kisutu akimwelezwa askari kuwa huna haki ya kumkamata mtu mpaka uwe na taarifa (RB) inayoonyesha ni kwa nini unamkata yaani kosa lake.
Tukiruhusu hii hali ya mtu kuvamia na kumkamata yoyote na kumpeleka kusikojulikana bila mjumbe wa mtaa kujua au familia mwisho wake tutakuwa na watu wengi waliopotea kama Ben Saanane. God forbid!
 
Kakamatwa na nani? Jeshi la polisi au jeshi la bashite?
Hii haileti taswira nzuri kwa raia wapenda haki. Iwapo Jeshi la Polisi limemkata mtu lazima watoe taarifa haraka ili kujiepusha na shutuma zisizo na ulazima
 
aibu tubu kwakweli,
Sisi tunaokwenda nchi za jirani ndio inakuwa tabu hata kujitambulisha unatokea Tz,
Zamani ilikuwa ni ufahari kusema wewe ni Mtanzania,
Lakini skuhizi aibu tupu.
 
Kutoka kwenye Facebook wall ya Professor Jay................

"Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONY @moni_ centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana.

Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!"



View attachment 491654

Baada ya uvamizi kwenye kituo cha louds Tv/Radio ,kukamata msanii Ney,na sasa uvamizi kwenye Studio ya Kurekodia muziki.movie inaendelea na jitihada za kunyamazishana.
 
Wamekamatwa au wametekwa? Mwenye Dar yake naye ana tatizo la sleep walking akitoka kwake anavamia studio yoyote iliyo wazi usiku. Ila huwa anakuwa usingizini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sifuri sifuri zikikuandama inaleta hamu za kuvamia studios
 
upload_2017-4-6_13-29-42.jpeg



Rapa Roma Mkatoliki ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Usimsahau mchizi' amekamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana.

Katika taarifa iliyotolewa na msanii Prof. Jay ambay pia ni mbunge wa Mikumi inasema msanii huyo alikamatwa jana akiwa studio.

Prof. Jay ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa jana wakiwa studio za Tongwe Records.

"Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua computer ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi" aliandika Prof. Jay

Mpaka sasa bado hajafahamika wasanii hao wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi.

Lakini watu kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.
 
Back
Top Bottom