Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Naona issue ya Roma macho yote ni Serikali tu wakati hakuna mwenye chembe ya ushahidi hata mmoja ktk comments zote.

Kwanza kilichowafanya Roma na kundi lake kutii amri za kupanda Noah nyeusi toka kwa watu waliovaa kiraia na kubeba vifaa vyenu vya kazi nini??

Hawakutakiwa kutii amri toka kwa raia usiowajua kupakia vifaa na kuondoka nao gari za kiraia kama umechukiliwa na Serikali kweli!!

Walikuwa zaidi ya watu 4 studio walikuwa na uwezo wa kupiga kelele kuwa wamevamiwa na kila mmoja kukimbia upande tofauti kwa Mara moja na naimani hiyo gari isingeondoka hapo.

Watu wange iblock tu,sasa wote sijui wa 4 sijui 5 mnakubali tu kirahisi kubeba vifaa kweli kirahisi tu kienyeji tu hivyo.

Mimi haiingii akilini sana Hapa kuna michezo tu ya kihuni inaendelea kwa kuchezea akili za watu. Ili tuamini kuwa Serikali unafanya harassment kwa watu wake.Hii syndicate haitakubalika.

Kazi ya msingi Serikali ni kulinda RAIA wake na si kuangamiza raia wake.

Mkuu unamaanisha kuna shoo wameenda kupiga mahali?

Kama kamanda kasema hawalijui hilo na hakuna jitihada za kiserikali zinazochukuliwa hadi sasa, naamini ni maombi tu yatakayowaokoa vijana hao na genge hilo la wahalifu kwani sitegemei wala kuamini kuwa watarudi salama kutokana na kuwa na siri nyingi za huko walipo. Eeh Mwenyezi Mungu tufunulie tuyajue yaliyijificha ktk matukio haya.
 
Kuna mambo hayajakaa sawa ktk hii habari:
  1. Roma hajatoa wimbo wowote wenye kukashfu serikali au viongozi wake hivi karibuni. Nyimbo zilizopo ni za wakati wa Kikwete na hakuchukuliwa hatua zozote.
  2. Waliomkamata wameenda na Noah nyeusi. Polisi hawana magari dizain ya Noah. Watu waliokuwa hapo walipaswa kuwatilia shaka kama kweli hao ni polisi.
  3. Polisi wamechukua kompyuta na TV. Hapo ndipo penye utata zaidi. Kwanin polisi wachukue TV? Kwa ajili ya upelelezi, polisi hahitaji hata monitor (screen) ya PC. Anahitaji System Unit tu. Hili jambo lilipaswa liwashtue wanaokamatwa na kuwahoji askari vitambulisho vyao na kituo wanachotaka kuwapeleka. Pia watu waliokuwa karibu wangeweza kustuka kutokana na hili.
Kwa maoni yangu, suala la kukamatwa kwa Roma halijakaa kipolisi kabisa. Inawezekana ni vyombo vingine vya dola au ni kiki inatengenezwa. Hoja ya kiki hata mimi sijapenda kuiibua, lakini kama Ney kasamehewa ambaye wimbo wake uliilenga serikali moja kwa moja, kwanini serikali itake kushughulika na Roma? Kama management ya Roma inatengeneza kiki, basi wanafanya makosa makubwa sana maana kuna watu kama Ben Saanane ambaye hajulikani aliko na pia Ulimboka ambaye alipotezwa halafu akapatikana akiwa na hali mbaya sana. Hatutakiwi kujenga dhana kwamba 'kupotea na kutopatikana hata ktk vyombo vya dola ni kawaida'.
Hakuna taarifa iliyosema kakamatwa na polisi na ingekua polisi tungejua yupo kituoni
 
Hapo usalama wanahusika vizuri sanaaa na hii movie inaonekana itakuwa tamu sanaa kama police wenyewe hawajui chochote ina maana hao watu watajitokeza na hawa jamaa watakuwa hai kweli??
 
sooth kiki inajulikana tu sema hii ya roma imejaa maswali mengi sana
inawezekana hata maadui wake wa zamani wametake advantage due to current situation in tz
Tumuombe Mwenyezi Mungu apatikane salama
 
Tukio lolote la kiusalama kwa mwanainchi likitokea kuna mamlaka husika za kutoa taarifa kwa utaratibu wa Serikali.

Sasa ukiniuliza mpaka lini hilo Mimi sio msemaji wao.

Lakini hujazuiwa kupiga kelele
Kumbuka kuna la Ben ziliachiwa mamlaka hadi leo halina majibu
 
Naona issue ya Roma macho yote ni Serikali tu wakati hakuna mwenye chembe ya ushahidi hata mmoja ktk comments zote.

Kwanza kilichowafanya Roma na kundi lake kutii amri za kupanda Noah nyeusi toka kwa watu waliovaa kiraia na kubeba vifaa vyenu vya kazi nini??

Hawakutakiwa kutii amri toka kwa raia usiowajua kupakia vifaa na kuondoka nao gari za kiraia kama umechukiliwa na Serikali kweli!!

Walikuwa zaidi ya watu 4 studio walikuwa na uwezo wa kupiga kelele kuwa wamevamiwa na kila mmoja kukimbia upande tofauti kwa Mara moja na naimani hiyo gari isingeondoka hapo.

Watu wange iblock tu,sasa wote sijui wa 4 sijui 5 mnakubali tu kirahisi kubeba vifaa kweli kirahisi tu kienyeji tu hivyo.

Mimi haiingii akilini sana Hapa kuna michezo tu ya kihuni inaendelea kwa kuchezea akili za watu. Ili tuamini kuwa Serikali unafanya harassment kwa watu wake.Hii syndicate haitakubalika.

Kazi ya msingi Serikali ni kulinda RAIA wake na si kuangamiza raia wake.
Ushawahi kutekwa na ukafanya unayoyaongea? Hujawahi ona taarifa za magari kadhaa kutekwa na watu wakachukuliwa vitu vyao? Unafikiri wao hawakufikiria kufanya unachodhani wangefanya?
 
Kitendo cha polisi kukana kuhusika ndiko kunawaweka ktk hali isiyosalama zaid
 
Kuna wakati najiwazia hivi hii ndo Tanzania yetu ya cku zote ama ? Kila iitwapo leo ukiamka unakutana na jipya, vijana wa watu wanatafuta riziki zao ila wanaishiwa kukamatwa tunaenda wapi
Halaf kumbe jamaa alijidai kumwachia Ney ili tuone n mwema
Ila watz tuungane jaman tupige makelele yasije tokea kama ya Ben tena
Mungu awatie nguvu familia zao
 
Ushawahi kutekwa na ukafanya unayoyaongea? Hujawahi ona taarifa za magari kadhaa kutekwa na watu wakachukuliwa vitu vyao? Unafikiri wao hawakufikiria kufanya unachodhani wangefanya?
Nadhani jamaa ni miongoni mwa waliohusika kumteka Roma na wenzake, hapa analeta hoja za kutuvuruga tu.
 
Kumbuka kuna la Ben ziliachiwa mamlaka hadi leo halina majibu
Ndiyo mamlaka zinaendelea sasa kelele zetu za mitandaoni zinabadili nini kama yuko hai yuko hai na yuko ktk mikono salama yuko hai na yuko ktk mikononi salama lakini kama alifariki ktk mikononi michafu ndiyo amekufa ktk mikono michafu na hatuwezi kumpata akiwa hai zaidi kuwasaka hao wahalifu.

Na mamlaka haziwezi kutoa taarifa just wewe uridhike tu wakati si kweli,wakiwa na taarifa za kweli wanatoa taarifa kamili.

Nakupa tu mfano kuna jamaa aliua ndugu zake kama watano Mbeya miaka ya nyuma sana then akatoweka kabisa yule bwana alitafutwa na Jamhuri na makachero toka Mbeya zaidi ya 8 maana alikuwa amejificha vijijini kabisa na mwisho alikuwa mbeba mizigo Ubungo stand na makachero nao walibeba naye mizigo Ubungo kwa muda wa miezi 6 ndiyo walipothibitisha kuwa ni yeye.

Basi sisi watu wakabipigwa pingu wabeba mizigo na makachero ndani ya pingu mpaka polisi mchujo mchujo basi yeye akabaki safari Mbeya na sasa anasubiri kitanzi.
 
Back
Top Bottom