Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Si tuliwasikia Mwakyemb na Magu wakiruhusu wimbo wa Ney wa Mitego, huku wakibainisha kuwa wasanii wako huru kuonyesha feeling zao kupitia tungo zao?

Sasa imekuwaje tena mbona kwa Roma Mkatoliki wanafanya vice versa?
 
Upumbavu na ujinga ukizidi , sasa inakuwa ni ukichaaa!
 
watakuwa walipata tetesi kuwa Roma yupo jikoni anapika bonge la jiwe wakaona isiwe tabu kwanini wasubiri kuumbuliwa wakati issue yenyewe wanaweza kuistop so easy

Haisadiii, si madini anayo moyoni na Kichwani!!!
Serikali dhaifu ni ile; inayopambana kuwazima watu wake, badala ya kuwaletea maendeleo na kutatua kero za matatizo yao.
 
Msanii wa mziki Ibrahim Mussa maarufu kama Roma mkatoliki na msanii mwezake Moni pamoja na kijana mwingine ,wamekamatwa jana majira ya saa moja usiku wakiwa studio za TONGWE Records na watu wanaosadikiwa kuwa ni jeshi la polisi.Wakamataji hao walio ondoka pia na Computer pamoja na Tv flat za Studioni hapo.
Chanzo cha kukamatwa kwao na mahala walipopelekwa bado haijajulikana.

Source.Joseph haule tweet.


Tukio hilo linajiri ikiwa limepita takribani juma moja tangu msanii mwingine wa mziki Emmanueli Elibariki maarufu Ney wa mitego aliyekuwa amekamatwa na jeshi la polisi kuachiliwa huru kwa order ya rais kupitia kwa waziri Mwakyembe.Msanii Ney wa mitego alikamatwa akiwa mkoani morogoro kwa kile kinacho daiwa ni kutunga wimbo wakichochezi alioupa jina la "wapo" ambao baadaye ulipewa ruhusa ya kusikika kwenye vituo vyote vya redio na serikali.
 

Attachments

  • Screenshot_2017-04-06-06-49-10.png
    96.9 KB · Views: 51
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…