Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati Sokoine kwa vile alipofariki nilikua bado sijazaliwa, nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;

1. Ajali iliyosababisha kifo cha Sokoine ilikuwa ya aina gani? Kupinduka kwa gari, kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?

2. Katika hiyo ajali hayati Sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?

3. Kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?

4. Kama wako hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?

4. Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?

5. Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?

6. Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?

7. KWANINI HAKUNA SOKOINE DAY KWENYE KALENDA YA NCHI YETU KAMA ILIVYO NYERERE DAY NA KARUME DAY?

Kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu.

Chinga 1.
 
Makubusho ya Taifa wanaweza kujibu baadhi ya unayoona ni utata kwako jaribu kuwaona wanaweza kukupa wapi pa kuanzia.
 

Je ulipitia uandishi wa magazeti ya udaku?
 

unaonekana kuwa na fununu!
 
Sasa kumbe wakati wa tukio ulikua mdogo, huyo aliekuambia Sokoine alikufa kwa ajali kwa asikuele na hayo yote unayotaka kuyajua. Alafu mpaka sasa hunau nahokijua kifo chake, lakini umeshajaji eti utata. Alafu bila aibu unaweka sahihi eti CHINGA 1 aah toa mi nakukataa.
 

Mmh kaka umenishtua kidogo, inaonekana kuna kitu unakijua hebu funguka kidogo na wengine tupate kujua.
 

Soma vizuri nilicho kiandika, hakuna alie niambia bali nimejua kupitia maandiko kadhaa ambayo bado yanaacha maswali hayo niliyo yaweka hapo juu...
 
Pichani ni gari lililosababisha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Mhe:Edward Moringe Sokoine mnamo Tar 12 Mwezi 04 Mwaka 1984 wakati akitokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma kwenda jijini Dar – Es – Salaam



Picha hapo chini ikimuonyesha Baba wa Taifa ambaye naye ni marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa aliyekuwa rafiki yake kipenzi Waziri Edward Sokoine ukiwa umelala milele.



Sokoine alifariki kwa ajali ya gari Jumatano ya Aprili 12, 1984 saa 11:30 jioni wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam
Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha!
Hayo mengine ni maswali ya hisia tu ambayo kila mwenye hisia zake moyoni hana budi kujiuliza bt all in all apumzike kwa amani milele!
 

7) tutakuwa na siku nyingi jamani taifa changa kama hili ni lazima tuache kushadadia masikuku ya aina hii
 

Asante kwa picha lakini bado hizo picha hazijibu maswali mengi,ukiangalia vizuri hayo maswali yote yame base kwenye kupata reality kwa mfano taarifa ya polisi inasemaje? lazima kulifanyika uxhunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajali hiyo kama unafanywa uchunguzi kwa ajali za watu wa kawaida itakua kwa waziri mkuu?
 
Official version ni kwamba Sokoine alifariki Aprili 12, 1984 Dumila, mkoani Morogoro, baada ya gari lake kugongana na Toyota Land Cruiser pickup (kama hiyo hapo chini) iliyokuwa ikiendeshwa na mkimbizi kutoka Afrika Kusini Dumisani Dube. Mwanachama huyo wa ANC alifikishwa mahakamani akikabiliwa na shtaka la kusababisha kifo kwa uendeshaji hatari, lakini baadae aliachiwa huru.

 
Nakumbuka ilikuwa ni jumapili ya tarehe 15 April 1984 nikiwa Arusha. tulikuwa kanisani kwenye ibada ya jumapili katika kanisa lilo kando ya barabara ya uhuru ( kwasasa karibu na shoprite) waumini wote tulitoka nje ya kanisa kuangalia mwili wa Sokoine ukipitishwa kuelekea Munduli kwa Maziko, nakumbuka jinsi watu walivyokuwa na simanzi wakati huo
 
Harooo usin'tanie!! Ina maana Mzee Kizota long time alikuwa Mjeda yule? Sa' yale manyama manyama aliyonayo na mengine yaliyojazana sehemu ya kukalia yametoka wapi yale? Au anaumwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…