Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati sokoine kwa vile alipo fariki nilikua bado sijazaliwa,nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;

1.ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine ilikua ya aina gani? kupinduka kwa gari,kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?

2.katika hiyo ajali hayati sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?

3.kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?

4.kama wakk hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?

4.Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?

5.Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?

6.Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?

7.KWA NINI HAKUNA SOKOINE DAY KWENYE KALENDA YA NCHI YETU KAMA ILIVYO NYERERE DAY NA KARUME DAY?

kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu.

Chinga 1.

kwa kifupi kifo cha Sokoine kilipangwa kitaalam kuliko wengi tujuavyo. Sokoine alipigwa lisasi kwanza ndo akagongwa na gari ili kupoteza ushahidi....hata uchunguzi wa dactari ulithibitisha kuwa mwili ulikuwa na tobo ya lisasi, na alivytaka kutoa taarifa akafungwa mdomo, vinginevyo na yeye angemalizwa. Hizi habari huwezi zipata kwa vitabu wala aticles
 
Taarifa za Polisi inaweza kuwa tofauti na hali halisi uliyopewa? Jaribu kuwasiliana n Polisi maana kuna mtu alikamatwa na kushtakiwa kwa kosa hilo.

Wataalam wa sheria nisaidieni hapa sheria inasemaje naweza kwenda polisi kufatilia taarifa za uchunguzi wa kifo cha sokoine?
 
Makubusho ya Taifa wanaweza kujibu baadhi ya unayoona ni utata kwako jaribu kuwaona wanaweza kukupa wapi pa kuanzia.

Nakumbuka Mwl katika hotuba yaker wakati wa mazishi alitamka kwamba MADAKTARI NA POLISI wamethibitisha kuwa Sokoine amefariki kwa ajali ya gari ,period
 
Official version ni kwamba Sokoine alifariki Aprili 12, 1984 Dumila, mkoani Morogoro, baada ya gari lake kugongana na Toyota Land Cruiser pickup (kama hiyo hapo chini) iliyokuwa ikiendeshwa na mkimbizi kutoka Afrika Kusini Dumisani Dube. Mwanachama huyo wa ANC alifikishwa mahakamani akikabiliwa na shtaka la kusababisha kifo kwa uendeshaji hatari, lakini baadae aliachiwa huru.

005.jpg

Mkuu mbona mnazidi kuleta majibu yenye utata. kwanza unasema gari iliyosababisha ajali ndio hii apo juu (Toyota Land Cruser) alafu ushaidi mwingine huu hapa chini unaonyesha gari ingine iliyosababisha ajali.

Pichani ni gari lililosababisha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Mhe:Edward Moringe Sokoine mnamo Tar 12 Mwezi 04 Mwaka 1984 wakati akitokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma kwenda jijini Dar – Es – Salaam

sokoine.jpg
 
Duh! komfyuzdi....!! ila mshua(dingi) aliwahi kunambia kwamba MORINGE(R.I.P) alkuwa siriasi mbayaaa na wezi wa mali ya NCHI hawakuwepo kipindi hicho... HATARI SANA..!!
enzi zake ilikuwepo sheria ya nguvu kazi(Human Resource Deployment Act).

Ole wako kijana ukutwe unazurulazurula mda wa kazi,wanakuweka ndani.kwawale wa rular area kuhudhuria kulima kwenye shamba la kijiji ilikua lazima sio ombi.
Walanguzi a.k.a wahujumu uchumi walikua wanatupa mafurushi ya pesa mitoni kukwepa kukamatwa uhujumu uchumi.
 
Mkuu mbona mnazidi kuleta majibu yenye utata. kwanza unasema gari iliyosababisha ajali ndio hii apo juu (Toyota Land Cruser) alafu ushaidi mwingine huu hapa chini unaonyesha gari ingine iliyosababisha ajali.

Pichani ni gari lililosababisha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Mhe:Edward Moringe Sokoine mnamo Tar 12 Mwezi 04 Mwaka 1984 wakati akitokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma kwenda jijini Dar – Es – Salaam

sokoine.jpg
hilo liloböndeka ndo lilikua la mkuru sokoine.
 
Ili iweje?
Vitu vingine ni state matters kwamba ajali yake ilipangwa ama ilikuwa ajali ya kawaida haibadilishi dhana kwamba alikufa!

Ni kweli mkuu sokoine amesha kufa ila yawezekana hujui umuhimu wa kuwa na taarifa kamili kwenye vifo vilivyoo jaa utata kwa maslahi binafsi ama ya umma, sometimes ni very risk kudadisi haya mambo but inabidi tu iwe hivyo kutokana na mambo kadha wa kadha.
 
Hakukuwa na utata wowote kwenye ajali ya Sokoine. Wakati ule tulikuwa na vyombo vizuri sana vya DOLA. Ile ilikuwa ni ajali. Sema tu ajali haikustahili kumpata Sokoine wetu ambaye kwa kweli alikuwa ni MJAMAA zaidi hata ya Mwalimu.
 
kwa kifupi kifo cha Sokoine kilipangwa kitaalam kuliko wengi tujuavyo. Sokoine alipigwa lisasi kwanza ndo akagongwa na gari ili kupoteza ushahidi....hata uchunguzi wa dactari ulithibitisha kuwa mwili ulikuwa na tobo ya lisasi, na alivytaka kutoa taarifa akafungwa mdomo, vinginevyo na yeye angemalizwa. Hizi habari huwezi zipata kwa vitabu wala aticles

Kitu kinazidi kunichanganya ni kua safari za kiongozi kama waziri mkuu kunakua na msafara wa magari kibao yakiwamo ya polisi na TISS unakuta magari mengine yanazuiwa barabarani kupisha msafara sasa kwa huyu sokoine ilikuaje hiyo gark ilimgonga sokoine isizuiliwe kupisha msafara wa mkubwa waziri? au enzi hizo safari za viongozi hazikua na ving'ora? kichwa kinauma.
 
kwa kifupi kifo cha Sokoine kilipangwa kitaalam kuliko wengi tujuavyo. Sokoine alipigwa lisasi kwanza ndo akagongwa na gari ili kupoteza ushahidi....hata uchunguzi wa dactari ulithibitisha kuwa mwili ulikuwa na tobo ya lisasi, na alivytaka kutoa taarifa akafungwa mdomo, vinginevyo na yeye angemalizwa. Hizi habari huwezi zipata kwa vitabu wala aticles

Kitu kinacho zidi kunichanganya ni kua safari za kiongozi kama waziri mkuu kunakua na msafara wa magari kibao yakiwamo ya polisi na TISS unakuta magari mengine yanazuiwa barabarani kupisha msafara sasa kwa huyu sokoine ilikuaje hiyo gark ilimgonga sokoine isizuiliwe kupisha msafara wa mkubwa waziri? au enzi hizo safari za viongozi hazikua na ving'ora? kichwa kinauma.
 
Hakukuwa na utata wowote kwenye ajali ya Sokoine. Wakati ule tulikuwa na vyombo vizuri sana vya DOLA. Ile ilikuwa ni ajali. Sema tu ajali haikustahili kumpata Sokoine wetu ambaye kwa kweli alikuwa ni MJAMAA zaidi hata ya Mwalimu.

Bado sijakuelewa vizuri, kwa hiyo ulitaka impate hiyo ajali?
 
Nasikia aliwashiwa taa apaki pembeni eti hakuelewa na nadhani magari yalikua speed kabla ya hili wala lile akalivaa gari la Pm ,wakati huo magari mengine yalishampita,ni kama vile alikua anaitarget gari ya pm.
 
Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati sokoine kwa vile alipo fariki nilikua bado sijazaliwa,nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;
Chinga 1.

Unahangaika na kifo cha Sokoine kilichotokea wakati ukiwa mdogo wakati kuna kifo cha Balali kimetokea ukiwa na akili timamu na ungeweza kufanya utafiti wako ukaja na majibu. Maswali yako huenda yakawa na maana ila afadhali mwili wa Sokoine ulionekana, Balali hata mwili wake haukuonekana. Anzia utafiti wako hapo.
 
Naunga hoja yako mkono IKINGO. Hili ccm ilihusika moja kwa moja.

Ni swali. Mwaka huo 1984 Edward Lowassa alikuwa wapi ndani ya serikali hii?

Miaka ya 1977 hadi 1989, Mhe Lowassa alikuwa akifanya kazi kama mwajiriwa wa chama cha TANU na baadaye CCM, alikuwa Kada wa Chama. Mwaka 1984 wakati Sokoine anafariki Mhe Lowassa alikuwa Uingereza akichukua Masters ya Development Studies, University of BATH.
 
Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati sokoine kwa vile alipo fariki nilikua bado sijazaliwa,nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;

1.ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine ilikua ya aina gani? kupinduka kwa gari,kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?

2.katika hiyo ajali hayati sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?

3.kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?

4.kama wakk hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?

4.Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?

5.Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?

6.Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?

7.KWA NINI HAKUNA SOKOINE DAY KWENYE KALENDA YA NCHI YETU KAMA ILIVYO NYERERE DAY NA KARUME DAY?

kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu.

Chinga 1.

Nakujibu kwa Ufupi Sokoine kwa Taarifa juu ya Uchunguzi wa maiti yake (Postmoterm) kama baadhi ya watu walivyomnukuu Prof. Shaba enzi zile ni kuwa alipigwa risasi maeneo ya kifuani, na yule Prof kutokana na ulevi wake aliweza kutoa siri hii bila kujua.
 
Back
Top Bottom