Chinga one mimi nakumegea yale ambayo ninayafahamu. Sokoine alikuwa anatokea Dodoma kurejea Dar baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge. Msafara wake ulipofika eneo la Wami Sokoine mkoani Morogoro, jirani na palipojengwa makao makuu ya sasa ya Wilaya ya Mvomero, gari yake ilipata ajali kwa kugongwa na gari L/cruiser iliyokuwa inaendeshwa na Mkimbizi raia wa Afrika ya kusini anaitwa Dumisani Dube aliyekuwa anaishi kwenye Kambi ya wanachama wa ANC hapo Dakawa. Dumisani alishitakiwa mahakamani lakini ninadhani kwa sababu za kisiasa zaidi, mahakama ilimwachia na alirudishwa kwao Afrika ya Kusini. Ajali hiyo ilitokea mchana na Sokoine alipofikishwa Hospitali ya mkoa wa Morogoro, madaktari walithibitisha kifo chake. Miaka kumi baada ya kifo chache, Daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Sokoine baada ya kifo, aliweka wazi taarifa ya chanzo cha kifo chake. Sehemu ya taarifa hiyo ilisema kuwa baada ya ajali, Sokoine alivunjika shingo ambayo ilisababisha kubana mshipa wa fahamu (spinal cord) ambayo ilikata mawasiliano kati ya ubongo na sehemu nyingine za mwili. Kumbuka Nyerere na Karume walikuwa maraisi wa nchi, Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, pia waasisi wa mataifa haya, hivyo tunawaenzi kwa sababu hizo kuu tofauti na Sokoine aliyekuwa Waziri mkuu. Mahali alipopatia ajali Sokoine pamejengwa mnara wa kumbukumbu. NINAWASILISHA.