Pichani ni gari lililosababisha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Mhe:Edward Moringe Sokoine mnamo Tar 12 Mwezi 04 Mwaka 1984 wakati akitokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma kwenda jijini Dar Es Salaam
Picha hapo chini ikimuonyesha Baba wa Taifa ambaye naye ni marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa aliyekuwa rafiki yake kipenzi Waziri Edward Sokoine ukiwa umelala milele.
Sokoine alifariki kwa ajali ya gari Jumatano ya Aprili 12, 1984 saa 11:30 jioni wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam
Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha!
Hayo mengine ni maswali ya hisia tu ambayo kila mwenye hisia zake moyoni hana budi kujiuliza bt all in all apumzike kwa amani milele!