Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkubwa nakwambia umenikumbusha kitu gani tena? Usinilize Mkubwa! Nakumbuka kabisa mvua kubwa ilinyesha pasipo kukatika takrban masaa 7 na RTD enzi hiyo ambayo leo ndiyo TBC ikitangaza moja kwa moja mazishi yake!
Nilikuwa mdogo sana kwani nilikuwa darasa la kwanza ila nilikuja barabarani kuomboleza kifo ya shujaa huyo wa Tanzania mzalendo wa Nchi yetu!
Nakumbuka kabisa wanakijiji wote wababa kwa wamama walijitokeza barabarani na huku vijana karibu wengi wa kabla lake (Maasai) Morani wakiumiza miili yao kwa mori siku hiyo ya mazishi nilikuwa mdogo lakini sitokaa nikasahau msiba huu mchungu kwa Watanzania walio wengi kwa JEMBE huyo Marehemu Edward Moringe Sokoine.
Mwenyenzi MUNGU mwingi wa Rehema na ampe pumziko la milele shambani mwake Bwana wetu!
Ameeen!
Niwakumbushe kitu. Wakati Sokoine akiwa Waziri Mkuu, Msaidizi wake alikuwa Horace Kolimba. Inatosha kusema hivyo!
Nakumbuka ilikuwa ni jumapili ya tarehe 15 April 1984 nikiwa Arusha. tulikuwa kanisani kwenye ibada ya jumapili katika kanisa lilo kando ya barabara ya uhuru ( kwasasa karibu na shoprite) waumini wote tulitoka nje ya kanisa kuangalia mwili wa Sokoine ukipitishwa kuelekea Munduli kwa Maziko, nakumbuka jinsi watu walivyokuwa na simanzi wakati huo
hapana haikuvunjika, ilikuwa ni mchana ibada imekwishaUnamaanisha ibada ilivunjika ili mumuone Sokoine?