Planet FSD
JF-Expert Member
- Oct 24, 2019
- 455
- 948
Wadau, leo kumesambaa taarifa kwenye vyombo vya habari kutoka kwa kamanda wa polisi Muliro akielezea sababu za kujiua katibu wa Feel Free Church kutokana na uchunguzi wa awali.
Maelezo ya kamanda yanapeleka kwenye hitimisho moja kuwa, Mama Mchungaji (Monica) na marehemu hawakuwa na mahusiano na kwamba katibu amejiua kwa kukataliwa baada ya kuwa akimtongoza Monica.
Inasemekana marehemu, alikuwa akimtumia jumbe za kimapenzi, jambo ambalo lilimfanya Monica akiwa na mama mtu mzima(hakutajwa jina) kufika nyumbani kwa marehemu siku moja kabla ya kifo chake kwa leo kumuhabarisha kuwa hataki kutumiwa jumbe hizo na wala hawezi kuwa nae kwa vile yeye ni mke wa mtu.
UTATA MTUPU…!
Kwa sisi wapenda documentaries za crime, hizi sababu zinaleta utata kuliko majibu. Katika matukio ya vifo kama hivi vinavyohusika mapenzi au fedha, lazima kitu kiitwacho MOTIVE kiwe established.
Katika wahusika wote watatu katika tukio hili, mtu mwenye motive kubwa ni Masanja. Haijalishi alikuwepo nchini au hakuwepo wakati tukio linatokea.
Ukifikiri kwa kina, haina maana ya mtu kujinyonga kisa kukataliwa, tena na mke wa mtu. Na ni mke wa mtu gani eti anakwenda nyumbani kwa anayemtongoza ili kumkataa? Kama amekuwa anamkataa siku zote, alishindwaje kumtaarifu mumewe kuwa katibu amevuka mstari? Badala yake akaenda na mama mtu mzima nyumbani kwa marehemu ili kumtaarifu juu ya kumkataa?
Je, ni kweli marehemu alijinyonga? Au amenyongwa halafu cover up imefanyika?
Je, inawezekana Masanja aligundua haya mahusiano na kutumia njia za kimafia kumueliminate marehemu huku yeye akiwa nje ya nchi ili kukwepa kushukiwa?( Mambo ya kawaida haya kwenye Investigation Discovery)
Uzuri kamanda amesema maelezo yake ya leo ni uchunguzi wa awali na bado wanaendelea. Naamini majibu yatapatikana tu, ila Masanja Mkandamizaji aangaliwe kwa ukaribu sana. Ndiye mtu pekee mwenye MOTIVE ya kuchezesha mambo. Simu za wahusika wote zikaguliwe kwa kina, na majibu yatakuwemo humo.