Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Ni kweli kwenye heligoland treaty muingereza alitumia influence yake kupata ziwa upande wa Tanganyika na kwa sababu inasemekana mjerumani hakuwa na interest kwenye water bodies. Wala hakujali ndio maana pande zote zingine kama msumbiji walipewa haki za mipaka yao

Ubaya zaidi tanganyika na malawi zilikuja kusimamiwa na muingereza kwa muda mrefu zaidi. Kwa hiyo kusingekuwa na njia ya yeye kugawa hilo eneo

Ila ukifuatilia vigezo vilivyotumika Berlin kugawa maeneo, natural geographical bodies kama maziwa, milima na mito ndivyo vilitumika kupima mipaka. Ukianzia ziwa Victoria, tanganyika hadi mto kagera.. Hiyo ndio ilikuwa criteria ya ugawsji Ila neglection ya mjerumani kutojali maziwa ndio ilisababisha yote hayo

Na ndio maana sheria ya mipaka hadi leo bado inatambua hizi geographical structures kama mpaka sahihi.. Kingine ukisema malawi wamiliki ziwa lote, utakuwa na assurance gani kwamba hawatokuja kudai na pwani

Shida ni hiyo mkuu neglection ya mjerumani na muingereza kutofuata vigezo vya ugawaji mipaka ndio chanzo cha yote
 
We jamaa unataka kusema pale Liuli,,Mbamba bay.. Maatema beach na Kyela ni Malawi??
 

Lengo la mada hii ni nini? Kwa kuwa ulitaka kudai pwani za Tanzania Bara ndiyo isababishe kuleta suala la ziwa Nyasa? Wewe ni mtanzania kweli? Umevuka mipaka
 
Kwanini Liwe la Malawi peke yao?

1. Upande wa Msumbiji mpaka upo katikati ya Ziwa, ukija Tanzania uende Pwani WTF?!!
2. MSUMBIJI wanaliita Ziwa Niasa, sisi tunalazimishwa tuite lake Malawi!

Wajua hata wao Malawians hawapo serious kulidai wanajua madhara yake, hence preservation of the status quo!
 
Usiwe zezeta kiasi hicho lile eneo ni huruma za Nyerere kuwapa wachambawima kwa ajili ya mifugo lakini serikali inaweza kubadilisha matumizi yake muda wowote ikitaka na usichojua ni kwamba wanachi wanazidi kujenga kwenye hilo eneo kwa kadri wanavyoweza, tuliza kinyesi hicho tahira usie na kisogo shenzi
 
Wewe ni mpuuzi kabisa ona bichwa lake
 

Usijali hadi zile mile kumi za sultani kutokea pwani ya kenya hadi tanganyika mnaweza kuzidai na mkazipata.

Hivi kwa nini wazanzbari mna chuki kali dhidi ya wabara
 
Hujui hata Makubaliano ya Berlin Conference 1884-85.

Let alone ushenzi wa Leopard II aliuofanya huko Congo (enhe sikia tu) hadithi za kugawa hiyo mipaka na ushenzi wa wazungu.

Unazungumza habari za UN, clear hujui historia ya Africa.

What do they teach you

Ningekuwa na nafasi serikalini ningesema usakwe unyofolewe walau kucha, ujinga mwingine sio wa kuvumiliwa.

Yaani kabisa unachezea mipaka ya nchi na kuna mataahira yanakuunga mkono.
 
Then tunarudi palepale, mikataba ya kikoloni inaipa Malawi ziwa Nyasa lote.
Hizi waligawa mkuu. Maandishi yapo na mkataba upo, sio maneno ya mdomoni. Kwahiyo ukienda mahakamani Malawi wakaleta Heligoland treaty, Mtanzania ukaleta maneno ya mdomoni ya "ni kwa sababu Ujerumani ilineglect vyanzo vya maji" unapigwa za uso asubuhi na mapema.
Na ndio maana sheria ya mipaka hadi leo bado inatambua hizi geographical structures kama mpaka sahihi.. Kingine ukisema malawi wamiliki ziwa lote, utakuwa na assurance gani kwamba hawatokuja kudai na pwani
Malawi hawawezi dai Pwani, watadai kwa claim ipi? Wanadai ziwa Nyasa kwa claim ya kimkataba wa wakoloni ambao ndio tunatumia kudai mpaka fulani uko wapi. Kama hatukubaliani na mpaka ule, vipi Kenya nao wakisema hawakubaliani na Kilimanjaro kuwa Tanzania? Na wao tuwakubalie.
Shida ni hiyo mkuu neglection ya mjerumani na muingereza kutofuata vigezo vya ugawaji mipaka ndio chanzo cha yote
Sasa hii kisheria ndio imeishakuwa hivyo. Hata Kaprivi strip kule Namibia inaheshimiwa na majirani. Haya mambo ya wakoloni walikosea yataleta shida kwenye akili za kipuuzi za Mwafrika.
Iddi Amin naye alisema wakoloni walikosea kutoipa bandari Uganda, pia walikosea kuiweka Kagera salient Tanzania. Ethiopia inasikitika sana kutokuwa na access na bandari.
 
Hivi mwendawazimu gani anaweza kukubali kuwa mpaka wa nchi ni mawimbi ya maji?.

Sisi tunachojua ni kwamba maji lazima yawe shared kwa watu wote wanaohabit hilo ziwa. Haki aliyotoa Mungu haiwezi kugawiwa vinginevyo na mkoloni.

Anayeleta habari za mkataba wa kikoloni aende akabaki na ukoloni wake, sisi ni watu huru na maji tuliyonayo tutayatumia bila kujali mikataba feki.
 
Miaka ya nyuma hili jambo lilileta shida sana. Ikabidi tupeleke baadhi ya maafisa wa jeshi letu kushughulikia lakini bado hali ni tete. Malawi wameshikilia msimamo Ziwa nyasa lote ni lao kitu ambacho si sahihi
 
nilende kukupinga. mipaka inapoangukia kwenye maj.bas lazma iwe nusu kwa nusu. kwa raman hio kipi kijustify malawa aje mpaka tanzania? bas kama ndio hivyo hata tanganyika uwaambie ko ngo kuwa ziwa ni lettu lote .hapa umepotosha
Kama hoja ni kugawana sawa sawa, inakuwaje Ziwa Victoria Tanzania tuna umiliki wa zaidi ya 60% wakati huo huo Kenya na Uganda wamepata jumla ya chini ya 35% ya ziwa Victoria?
 
Hilo ziwa haiwezekani nchi moja kujimilikisha lote ilihali na raia wetu wanalitumia kwa sababu za kiuchumi na kimaisha...eti kisa mkataba wa mkoloni....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…