Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
Ni kweli kwenye heligoland treaty muingereza alitumia influence yake kupata ziwa upande wa Tanganyika na kwa sababu inasemekana mjerumani hakuwa na interest kwenye water bodies. Wala hakujali ndio maana pande zote zingine kama msumbiji walipewa haki za mipaka yaoUnajua kwamba OAU walikubaliana kuwa mipaka ya kikoloni ndio iendelee kutumika baada ya uhuru?
Yani unataka kusema kwamba nchi za Afrika tuna busara sana kwahiyo tuanze kuchora upya mipaka. Unazijua akili za Mwafrika kweli mkuu?
Yani turudie kuchora, Uganda wapendekeze kupata Kagera salient, Kenya wapendekeze kupata mlima Kilimanjaro pale ambapo ramani ilipindishwa ili mlima uwe Tanzania, Zanzibar wadai pwani ya bara maana kuna Sultan aliwahi sema anaimiliki na akiwapa Wajerumani sijui, Tanzania tudai sehemu ya Masai Mara ya Kenya ili Wamasai wote wawe Tanzania, Kenya wapendekeze waongezewe sehemu ya ziwa Victoria wawe nayo nyingi maana Tanzania imechukua kipande kikubwa zaidi, Burundi nao waombe sehemu kubwa zaidi ya ziwa Tanganyika. Hapo ni sisi tu, bado sehemu nyingine za Afrika.
Kiuhalisia ukisoma Helligoland treaty na mkataba mwingine, hakuna ushahidi unaoonyesha Tanzania tunamiliki nusu ya ziwa Nyasa. Hata Wajerumani waliokuwa wanatawaka Tanganyika ramani yao inaonyesha Nyasa nzima ni ya Malawi.
Sisi Tanzania tunakuwa na claim kuwa wazungu walikubaliana kama kuna chanzo cha maji mpakani basi kigawanywe kila nchi inayopakana ipate kiasi chake. But that wasn't the case kwa ziwa Nyasa. Tukienda mahakama ya usuluhishi, zikaletwa mikataba na mashahidi wakoloni Tanzania tunashindwa asubuhi na mapema kabisa.
Ubaya zaidi tanganyika na malawi zilikuja kusimamiwa na muingereza kwa muda mrefu zaidi. Kwa hiyo kusingekuwa na njia ya yeye kugawa hilo eneo
Ila ukifuatilia vigezo vilivyotumika Berlin kugawa maeneo, natural geographical bodies kama maziwa, milima na mito ndivyo vilitumika kupima mipaka. Ukianzia ziwa Victoria, tanganyika hadi mto kagera.. Hiyo ndio ilikuwa criteria ya ugawsji Ila neglection ya mjerumani kutojali maziwa ndio ilisababisha yote hayo
Na ndio maana sheria ya mipaka hadi leo bado inatambua hizi geographical structures kama mpaka sahihi.. Kingine ukisema malawi wamiliki ziwa lote, utakuwa na assurance gani kwamba hawatokuja kudai na pwani
Shida ni hiyo mkuu neglection ya mjerumani na muingereza kutofuata vigezo vya ugawaji mipaka ndio chanzo cha yote