Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Kuna jamii na makabila yapo upande wa tanzania yalikuwa yanatumia ziwa nyasa kuvua zaidi ya miaka 1000+ kabla hata ya ukoloni leo unawaambia wasitumie kwa sababu ziwa ni la nchi ya malawi unadhani ina-make sense
 
Naamini huyu mpemba atakuwa ametumwa kupima upepo,namshukuru Mungu ameshauona upepo Upo vipi..
 
Ukweli usemwe na sio kupotoshwa.
Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kisheria, Tanzania mpaka leo tunaendelea kudai haki ya kudhurumiwa kupata sehemu ya ziwa. Hicho ndio google map wamefanya.
Wewe ndiyo ulikuwa unapinga serikali isisitishe mkataba wa songas eeeh ok
 
Wakati wa masika tenende yote Ile inafurika maji hadi inakuwa ngumu kupita kwenda Ipinda na kyela...maji yoote yanakwenda Sumbi...halafu mpemba mmoja anakuja kusema maji yakishaingia kwa Sumbi...yanakuwa siyo yetu tena,yanakuwa ya Malawi..
 
Hili jambo litaleta shida huko mbeleni. JPM angekuwa mtu sahihi wa kulimaliza.
Hakuna shida yoyote ...mpaka wakusadikika utakuwa huo wa mabeberu na mpaka halisi utakuwa katikati ya ziwa over ....wala msiwe na wasiwasi wowote kwenye jambo hilo
 
UMEMALIZA KILA KITU 🫡🤝
 

Kulingana na ramani uliyoiweka ndugu Zanzibar-ASP, ninkwamba ziwa hilo limegusa nchi tatu, Malawi, Mozambique na Tanzania.

Kulingana na ramani hiyo, kwenye nchi za Malawi na Tanzania, mpaka umepita kwenye ufukwe upande wa TZ. Lakini unapoambaa na mpaka huo mpaka nchini Mozambique, unagundua kwamba mpaka unarudi katikati ya ziwa, hapo mimi ndio sijaelewa aisee!!

Kwamba, kati ya Malawi na TZ mpaka upo ufukweni kwetu, ila kati ya Malawi na Mozambique mpaka upo katikati ya ziwa, inakuwaje hapo?

Pia ukiangalia mipaka kwenye maziwa mengine yanayounganisha nchi na nchi, mipaka inakuwa katikati ya ziwa!

Sasa kwanini kipande cha Tanzania na Malawi mpaka uwe ufukweni TZ ila kipande cha Malawi na Mozambique mpaka uwe katikati kama maziwa mengine?
 
Huyo Kikwete alishindwa vibaya mno alichofanya ni kumtishia Joyce Banda kwamba atapeleja jeshi
 
sheria za UN zinatamka wazi, mipaka ya kikoloni ya kisheria ndio mipaka rasmi baada ya uhuru. Mpaka wa kikoloni unatamka wazi kuwa Ziwa Nyasa lote ni mali ya Malawi
Naomba vifungu viwili tuu sehemu ilipoandikwa lake nyasa ni mali halali ya wamalawi
 
Angalau kuwa mzalendo; yanapotokea masuala ya kitaifa huwa haifai kuegemea upande wa pili.
Tupambane kwa jasho na damu tunufaike na ziwa nyasa, mipaka iliwekwa na mkoloni wala muafrika hakuweka mipaka.
Babu zetu walinufaika na ziwa nyasa miaka nenda rudi, iweje mkoloni atugawe?
Afrika mashariki yote Tanzania inanufaika na ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa na mito kama kagera na mto ruvuma ambayo imegawa Nchi, pamoja na hivyo tunanufaika na bahari pia.

Kumiliki nusu ya ziwa ni muhimu sana kwa masuala ya usalama wa nchi, leo ww unaleta ujinga wa kutetea malawi, WHY??
Wewe na Wamalawi acheni ubinafsi
 
Wewe ni under 18,ramani zote za vitabu vya zamani zinaonyesha mpaka upo kati kati ya ziwa lakini Kuna version mpya ya vitabu kuanzia miaka ya 2000 viliteta shida
 
Angalia mambo ya fursa na mipaka ya nyumba yako au familia yako,haya mambo ya kumsaidia Hangaya haya tusaidii chochote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…