Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Huyu dogo ipo siku Moja atatamani asingeandika haya time will tell thread zake zinafuatiliwa kiumakini sana
 
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Hii ramani ya Ziwa uliyoweka umeitazama vizuri kweli? Mpaka wa Malawi na Msumbiji upo kati kati lakini wa Tanzania upo pembeni? Sasa kama maji yote ni ya Malawi, itabidi Malawi watulipe kila mili second ya muda maji hayo yatakapo kuwa yanagusa ardhi yetu, na bei ya gharama hiyo ni ardhi yote ya nchi kavu ya Malawi iwe sehemu ya nchi yetu !
 
Haya sawa, sasa turudi Zanzibar, ni nchi au sio nchi?
 
Mpaka upo katikati ya Ziwa kwa sasa, Wamalawi waliishindwa kesi wakaingia mitini.
 
Hamna mwenye haki ya umiliki wa hilo ziwa asilimia 100.

Mipaka ya kikoloni haiwezi kutuondolea haki yetu.
Hebu onyesha mpaka wa Tanganyika au Tanzania ambao sio wa kikoloni unaanzia wapi na unaishia wapi na unatambuliwa na nani.
 
Takataka ninyi mikataba inapaswa kuwa wazi, ni mali ya wananchi.
 
Kuna jamii na makabila yapo upande wa tanzania yalikuwa yanatumia ziwa nyasa kuvua zaidi ya miaka 1000+ kabla hata ya ukoloni leo unawaambia wasitumie kwa sababu ziwa ni la nchi ya malawi unadhani ina-make sense
Mipaka ya Kiafrika haikugawanywa kwa kutumia sense. Kama ingekuwa hivyo, kusingekuwepo Wamasai pande za Tz na Kenya.

Kwa kutumia sense, Wahaya wangekuwa sehemu ya Uganda maana lugha yao inasikilizana na Kiganda na Kinyankole kuliko Kiha au Kisukuma lugha za jirani kwa huku Tanzania.

Tukipeleka sense mahakama ya kimataifa Malawi wakapeleka mikataba na wakaita wakoloni walioisaini then hapo tutaambulia sifuri. Tutaambiwa Tanganyika tulipata uhuru mwaka 1961, aliyekabidhi uhuru alikabidhi ziwa likiwa Malawi.
Kama tunabisha basi na kwanini mfano Karagwe isiwe sehemu ya Rwanda na wao wakiamua kutumia sense ya kwamba Wanyambo na Rwandese wanasikilizana.
 
Wakamfufue Mwalimu Julius Nyerere na Kamuzu Banda kama mashahidi mahususi waliochukua nchi zetu kutoka kwa wakoloni ili kesi iishe,porojo porojo za google map hazitusaidii chochote zaidi ya magomvi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…