WALOLA VUNZYA
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 7,154
- 7,155
Sahihi kabisaNdio maana mipaka inatakiwa kuheshimiwa. Hakuna sehemu majirani awawezi eneo fulani ni lao. Halikadhalika Tanzania inaweza kuwa na claim hizo hizo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sahihi kabisaNdio maana mipaka inatakiwa kuheshimiwa. Hakuna sehemu majirani awawezi eneo fulani ni lao. Halikadhalika Tanzania inaweza kuwa na claim hizo hizo.
Na ndo wanaouza bàndari za tanganyika.
Inastahili kuwa hivyo.Au tulipiganie kama gaza?
Unadhani kwanini makambi ya wakimbizi ya Congo yapo Tanzania?Mbona na Tanganyika haiko kwetu pumbavu.
Hii ramani ya Ziwa uliyoweka umeitazama vizuri kweli? Mpaka wa Malawi na Msumbiji upo kati kati lakini wa Tanzania upo pembeni? Sasa kama maji yote ni ya Malawi, itabidi Malawi watulipe kila mili second ya muda maji hayo yatakapo kuwa yanagusa ardhi yetu, na bei ya gharama hiyo ni ardhi yote ya nchi kavu ya Malawi iwe sehemu ya nchi yetu !Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Haya sawa, sasa turudi Zanzibar, ni nchi au sio nchi?Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.
Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Tambua tu kwamba Tanzania kwa sasa ni mmiliki wa nusu ya Ziwa Nyasa, hizo documents zilitazamwa mwaka ule wakati kesi ikiendelea, Wanasheria wetu walikwenda Ujerumani kwa ajili ya kupata hizo taarifa.HUNA na hujawahi kuiona na hutakaa uione kwasababu hazipo Africa...
Mkuu umeongea hapo mwisho kwa uzalendo mkubwa sana tutafsirie tafadhali kwamba eti kibhoko nini?.Yaani masika nikiangalia mto kiwila na song we unavyoyamimima maji kwenda kwa Sumbi halafu eti Sumbi gwa kumalabhi....nakamo..
Atukuketa, kibhoko tukimenye atukukomana.
Mpaka upo katikati ya Ziwa kwa sasa, Wamalawi waliishindwa kesi wakaingia mitini.Upo sahihi.
Ila nafikiri maridhiano ya mipaka yalifanyika kati ya serikali ya wakoloni wa kiingereza (Malawi) na kireno (Msumbiji).
Wakati wanaelekea kutaka kuridhiana kati ya Uingereza (Malawi) na Germany (Tanganyika), WWI ikawa imetokea na baadaye Malawi na Tanganyika zote zikawa chini ya UK, huku mpaka wa mwanzo uliotambulika na Heligolqnd treaty ukiwa haujabadilika. Ni mpaka huo ndio uliendelea kurithishwa kwenye mataifa huru na ndio unaofuatwa na google.
Ni ukweli unaouma.
Kimantiki kila mtu anatamani mpaka uwe katikati.
Hebu onyesha mpaka wa Tanganyika au Tanzania ambao sio wa kikoloni unaanzia wapi na unaishia wapi na unatambuliwa na nani.Hamna mwenye haki ya umiliki wa hilo ziwa asilimia 100.
Mipaka ya kikoloni haiwezi kutuondolea haki yetu.
Takataka ninyi mikataba inapaswa kuwa wazi, ni mali ya wananchi.Siwezi kuweka humu masuala nyeti ya wizara ya katiba na sheria pamoja na mambo ya nje. Aliyeshughulikia suala hili na Tanzania ikashinda kesi kwa Malawi kuingia mitini ni Hamza Johari kwa sasa ni mwanasheria mkuu wa Tanzania AG.
Ofisi zake zipo pale pembeni ya mahakama kuu kama unaelekea wizara ya ardhi, ibuka tu na uombe hizo nyaraka naamini utapewa ingawa itabidi ueleze sababu haswa ya kuzihitaji ni ipi.
Mipaka ya Kiafrika haikugawanywa kwa kutumia sense. Kama ingekuwa hivyo, kusingekuwepo Wamasai pande za Tz na Kenya.Kuna jamii na makabila yapo upande wa tanzania yalikuwa yanatumia ziwa nyasa kuvua zaidi ya miaka 1000+ kabla hata ya ukoloni leo unawaambia wasitumie kwa sababu ziwa ni la nchi ya malawi unadhani ina-make sense
Sawa Ziwa Nyasa ni letuTambua tu kwamba Tanzania kwa sasa ni mmiliki wa nusu ya Ziwa Nyasa, hizo documents zilitazamwa mwaka ule wakati kesi ikiendelea, Wanasheria wetu walikwenda Ujerumani kwa ajili ya kupata hizo taarifa.
Kwani kesi ilifikishwa ICJ?Mpaka upo katikati ya Ziwa kwa sasa, Wamalawi waliishindwa kesi wakaingia mitini.
Wakamfufue Mwalimu Julius Nyerere na Kamuzu Banda kama mashahidi mahususi waliochukua nchi zetu kutoka kwa wakoloni ili kesi iishe,porojo porojo za google map hazitusaidii chochote zaidi ya magomvi.Unajua kwamba OAU walikubaliana kuwa mipaka ya kikoloni ndio iendelee kutumika baada ya uhuru?
Yani unataka kusema kwamba nchi za Afrika tuna busara sana kwahiyo tuanze kuchora upya mipaka. Unazijua akili za Mwafrika kweli mkuu?
Yani turudie kuchora, Uganda wapendekeze kupata Kagera salient, Kenya wapendekeze kupata mlima Kilimanjaro pale ambapo ramani ilipindishwa ili mlima uwe Tanzania, Zanzibar wadai pwani ya bara maana kuna Sultan aliwahi sema anaimiliki na akiwapa Wajerumani sijui, Tanzania tudai sehemu ya Masai Mara ya Kenya ili Wamasai wote wawe Tanzania, Kenya wapendekeze waongezewe sehemu ya ziwa Victoria wawe nayo nyingi maana Tanzania imechukua kipande kikubwa zaidi, Burundi nao waombe sehemu kubwa zaidi ya ziwa Tanganyika. Hapo ni sisi tu, bado sehemu nyingine za Afrika.
Kiuhalisia ukisoma Helligoland treaty na mkataba mwingine, hakuna ushahidi unaoonyesha Tanzania tunamiliki nusu ya ziwa Nyasa. Hata Wajerumani waliokuwa wanatawaka Tanganyika ramani yao inaonyesha Nyasa nzima ni ya Malawi.
Sisi Tanzania tunakuwa na claim kuwa wazungu walikubaliana kama kuna chanzo cha maji mpakani basi kigawanywe kila nchi inayopakana ipate kiasi chake. But that wasn't the case kwa ziwa Nyasa. Tukienda mahakama ya usuluhishi, zikaletwa mikataba na mashahidi wakoloni Tanzania tunashindwa asubuhi na mapema kabisa.
Mpaka ni katikati ya Ziwa Nyasa, hizi habari nyingine zipuuze tu.Takataka ninyi mikataba inapaswa kuwa wazi, ni mali ya wananchi.
Wanasheria wa Malawi waliikimbia kesi, haijalishi ilipelekwa mahakama ipi.Kwani kesi ilifikishwa ICJ?
Nusu yake ni sehemu ya Tanzania na nusu ni sehemu ya Malawi.Sawa Ziwa Nyasa ni letu