Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Huyu dogo ipo siku Moja atatamani asingeandika haya time will tell thread zake zinafuatiliwa kiumakini sana
 
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Hii ramani ya Ziwa uliyoweka umeitazama vizuri kweli? Mpaka wa Malawi na Msumbiji upo kati kati lakini wa Tanzania upo pembeni? Sasa kama maji yote ni ya Malawi, itabidi Malawi watulipe kila mili second ya muda maji hayo yatakapo kuwa yanagusa ardhi yetu, na bei ya gharama hiyo ni ardhi yote ya nchi kavu ya Malawi iwe sehemu ya nchi yetu !
 
Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.

Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.

Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Haya sawa, sasa turudi Zanzibar, ni nchi au sio nchi?
 
Upo sahihi.
Ila nafikiri maridhiano ya mipaka yalifanyika kati ya serikali ya wakoloni wa kiingereza (Malawi) na kireno (Msumbiji).

Wakati wanaelekea kutaka kuridhiana kati ya Uingereza (Malawi) na Germany (Tanganyika), WWI ikawa imetokea na baadaye Malawi na Tanganyika zote zikawa chini ya UK, huku mpaka wa mwanzo uliotambulika na Heligolqnd treaty ukiwa haujabadilika. Ni mpaka huo ndio uliendelea kurithishwa kwenye mataifa huru na ndio unaofuatwa na google.

Ni ukweli unaouma.

Kimantiki kila mtu anatamani mpaka uwe katikati.
Mpaka upo katikati ya Ziwa kwa sasa, Wamalawi waliishindwa kesi wakaingia mitini.
 
Hamna mwenye haki ya umiliki wa hilo ziwa asilimia 100.

Mipaka ya kikoloni haiwezi kutuondolea haki yetu.
Hebu onyesha mpaka wa Tanganyika au Tanzania ambao sio wa kikoloni unaanzia wapi na unaishia wapi na unatambuliwa na nani.
 
Siwezi kuweka humu masuala nyeti ya wizara ya katiba na sheria pamoja na mambo ya nje. Aliyeshughulikia suala hili na Tanzania ikashinda kesi kwa Malawi kuingia mitini ni Hamza Johari kwa sasa ni mwanasheria mkuu wa Tanzania AG.

Ofisi zake zipo pale pembeni ya mahakama kuu kama unaelekea wizara ya ardhi, ibuka tu na uombe hizo nyaraka naamini utapewa ingawa itabidi ueleze sababu haswa ya kuzihitaji ni ipi.
Takataka ninyi mikataba inapaswa kuwa wazi, ni mali ya wananchi.
 
Kuna jamii na makabila yapo upande wa tanzania yalikuwa yanatumia ziwa nyasa kuvua zaidi ya miaka 1000+ kabla hata ya ukoloni leo unawaambia wasitumie kwa sababu ziwa ni la nchi ya malawi unadhani ina-make sense
Mipaka ya Kiafrika haikugawanywa kwa kutumia sense. Kama ingekuwa hivyo, kusingekuwepo Wamasai pande za Tz na Kenya.

Kwa kutumia sense, Wahaya wangekuwa sehemu ya Uganda maana lugha yao inasikilizana na Kiganda na Kinyankole kuliko Kiha au Kisukuma lugha za jirani kwa huku Tanzania.

Tukipeleka sense mahakama ya kimataifa Malawi wakapeleka mikataba na wakaita wakoloni walioisaini then hapo tutaambulia sifuri. Tutaambiwa Tanganyika tulipata uhuru mwaka 1961, aliyekabidhi uhuru alikabidhi ziwa likiwa Malawi.
Kama tunabisha basi na kwanini mfano Karagwe isiwe sehemu ya Rwanda na wao wakiamua kutumia sense ya kwamba Wanyambo na Rwandese wanasikilizana.
 
Unajua kwamba OAU walikubaliana kuwa mipaka ya kikoloni ndio iendelee kutumika baada ya uhuru?

Yani unataka kusema kwamba nchi za Afrika tuna busara sana kwahiyo tuanze kuchora upya mipaka. Unazijua akili za Mwafrika kweli mkuu?

Yani turudie kuchora, Uganda wapendekeze kupata Kagera salient, Kenya wapendekeze kupata mlima Kilimanjaro pale ambapo ramani ilipindishwa ili mlima uwe Tanzania, Zanzibar wadai pwani ya bara maana kuna Sultan aliwahi sema anaimiliki na akiwapa Wajerumani sijui, Tanzania tudai sehemu ya Masai Mara ya Kenya ili Wamasai wote wawe Tanzania, Kenya wapendekeze waongezewe sehemu ya ziwa Victoria wawe nayo nyingi maana Tanzania imechukua kipande kikubwa zaidi, Burundi nao waombe sehemu kubwa zaidi ya ziwa Tanganyika. Hapo ni sisi tu, bado sehemu nyingine za Afrika.

Kiuhalisia ukisoma Helligoland treaty na mkataba mwingine, hakuna ushahidi unaoonyesha Tanzania tunamiliki nusu ya ziwa Nyasa. Hata Wajerumani waliokuwa wanatawaka Tanganyika ramani yao inaonyesha Nyasa nzima ni ya Malawi.

Sisi Tanzania tunakuwa na claim kuwa wazungu walikubaliana kama kuna chanzo cha maji mpakani basi kigawanywe kila nchi inayopakana ipate kiasi chake. But that wasn't the case kwa ziwa Nyasa. Tukienda mahakama ya usuluhishi, zikaletwa mikataba na mashahidi wakoloni Tanzania tunashindwa asubuhi na mapema kabisa.
Wakamfufue Mwalimu Julius Nyerere na Kamuzu Banda kama mashahidi mahususi waliochukua nchi zetu kutoka kwa wakoloni ili kesi iishe,porojo porojo za google map hazitusaidii chochote zaidi ya magomvi.
 
Back
Top Bottom