Mipaka yote ya bara la Afrika iliwekwa na wakoloni, na hiyo ndio tuliweza kurithi baada ya uhuru na sheria za UN zinatamka wazi, mipaka ya kikoloni ya kisheria ndio mipaka rasmi baada ya uhuru. Mpaka wa kikoloni unatamka wazi kuwa Ziwa Nyasa lote ni mali ya Malawi japokuwa lilikuwa linapakana na nchi tatu (Malawi, Tanzania, Msumbiji), leo hii Msumbiji ana umiliki pia wa sehemu ya ziwa Nyasa baada ya kuridhiana na Malawi kumpa sehemu ya ardhi yake yenye milima ili yeye (Msumbiji) apate sehemu ya ziwa hivyo mpaka wa Malawi na Msumbiji ukabadilishwa kisheria. Tanzania tumekataa kuridhiana na Malawi ili nasi tupate sehemu ya ziwa kisheria.
Hoja ya Tanzania ni moja tu, mkataba wa kikoloni ulioipa Malawi umiliki wote wa Ziwa haukuwa wa haki, hivyo haupaswi kurithiwa, upigwe chini. Hayo sasa ndio mambo ya kisheria, siku moja tutajadili upya hapa JF japokuwa ilishajadiliwa sana humu.