Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Wakuu nimekiwa kwenye lindi la msongo wa mawazo mazito juu ya upatikanaji wa katiba ya umma,
Utata wa sheria ya katiba mpya.
Kwenye tafsiri ya kiswahili inatafsiriwa hivi:
1. Tafsiri ya kifungu cha 25 (2)cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba juu ya Majukumu ya Bunge la Katiba Mpya inasema hivi: "Bunge Maalumu la Katiba litakuwa na jukumu la kuijadili rasimu ya Katiba na kuipitisha tu"
Sheria hii ya mabadiliko ya Katiba inalifunga Bunge Maalumu la Katiba kuishia katika kujadili na kupitisha rasimu hiyo bila kuondoa neno wala kuongeza neno litakalobadili maana ya neo hilo.
Vivyo hivyo Bunge la katiba litafanya kazi ya kuboresha masharti ya Katiba yaliyomo ndani ya rasimu ya Katiba pasipo kuweka masharti mapya ambayo kwa taathira yatabadili ama kufifisha masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye Rasimu hii ya Katiba Mpya.
Lakini kwenye tafsiri ya sheria ile ya kiingereza kifungu hichohicho inatoa ruhusa kwa Bunge la katiba, kujadili, kuondoa kifungu, kutunga kifungu ama KUIONDOA/KUIFUTA kabisa rasimu ile ya Mzee Warioba ambayo ndio maoni ya umma na kuleta rasimu yao ya Lumumba,
Utata huo hauishii kwenye Sheria tu bali upo pia kwenye KANUNI za uendesha wa Bunge lenyewe la katiba,
Mathalani ukakasi wa kanuni ya 48 ya uendeshaji wa bunge la katiba unaosema kutakuwa na mambo ya faragha katika utungaji wa katiba hiyo,
Watanzania lazima tureje hata kwenye historia ya nchi yetu, Tujifunze huko ambapo tunaona wazi kuwa hata Lancaster House hapakuwa na faragha wakati Wazungu wakiandika katiba ya kwanza ya Tanganyika!
Katiba hutungwa na watu na bunge la katiba ni bunge la watu kwa niaba ya watanzania!
Watanzania tusimame tukatae uimla huu, sasa tuwaeleze hawa mabeberu wa ndani kuwa MAPINDUZI ya kiraia hayaepukiki ikiwa watafinyanga matakwa ya umma,
Jionee vifungu vyenye utata hapa chini.

Kwa mwendo huu katiba ni kiini macho chenya maslahi ya wavimbisha matumbo lakini si kwa maslahi ya nchi na watanzaia wenye dhamira ya kweli na nchi yao.
View attachment 141123View attachment 141124View attachment 141125View attachment 141126View attachment 141127View attachment 141128View attachment 141125View attachment 141129