Utata wa Sheria na Kanuni hizi za Bunge la Katiba utazaa Katiba ya mtaa wa Lumumba

Utata wa Sheria na Kanuni hizi za Bunge la Katiba utazaa Katiba ya mtaa wa Lumumba

Kwa Hiyo unamaanisha Wakuu wa Upinzani walikosea Kwenda Ikulu?
MissM4C, hawakukosea kwenda Ikulu, bali kuna kitu Chadema ilipaswa kufanya mule bungeni, haikufanya, badala yake, wakasusa, wakatoka nje, sheria ikapitishwa bila wao, ndipo wakaitwa ikulu kubembelezewa juice, chai na vitafunwa!.

Kosa lilifanyika mwanzo na haya ni matokeo tuu!, tangu mwanzo tumepiga kele Chadema i deal na chanzo, na sasa haya ni matokeo tuu!. Kama ulishindwa kuzuia chanzo, ukafurahia juice na chai, unashangaa nini kwa matokeo haya?.
Kanisome hapa labda utanielewa Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!
Pasco.
 
kwa akili yako suala la kupatikana katiba bora anayewajibika ni CDM?????????????
Kama taifa litaendelea kubaki na watu wenye mawazo mgando kama wewe basi tumekwisha!!!!
Mkuu Shingwe,
Mchakato huu ni process, ulianzia Bungeni, Chadema kikiwa ni chama kikuu cha Upinzani, kuna kitu hapa Chadema kilipaswa kufanya tangu mwanzo, hakikufanya na haya sasa ndio matokeo!.

Jee kitu ambacho Chadema walipaswa kufanya ni nini?, kwa nini hawakufanya?, na badala yake walifanya nini?.
Soma hapa Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!
Pasco
 
Katiba mpya ilikuwa ni sera ya Chadema, haikuwahi kuwa sera ya CCM!.

Tangu mchakato unaanzishwa na CCM tuliwaonya Chadema beware of the phase "I fear the Greeks especially when they bring gifts!", Chadema hakusikia, CCM walipouleta ule muswada, tukiwategemea Chadema wangeusimamisa mchakato by doing the right thing at the right time and doing it right!, Chadema hakufanya walichopaswa kufanya!, na badala yake wakakimbilia juice, chai na vitafunwa vya Ikulu!, haps tulipofikia unadhani ndio tunaweza kufanya nini?!.

Dawa ni kwa Chadema na wengine wote kutulia tuu kama wananyolewa!, tuipate hiyo "bora katiba" msibiri kutimiza hiyo ndoto yenu ya 2015, ndipo mtuletee "katiba bora!".

Hiki unachotaka kushauri ni kutupigia tuu makelele ya mlango, the ball is set, kipenga kitapulizwa na magoli yataingia!.

Hii ni sehemu ya kulipia gharama ya kufanya kulichopaswa kufanywa, and this is the price Chadema na sisi wengine wote, must pay!.

Pasco.

Hii nchi iko na raia wa kiwango cha chini wengi mno akiwemo Pasco.
 
Mkuu Shingwe,
Mchakato huu ni process, ulianzia Bungeni, Chadema kikiwa ni chama kikuu cha Upinzani, kuna kitu hapa Chadema kilipaswa kufanya tangu mwanzo, hakikufanya na haya sasa ndio matokeo!.

Jee kitu ambacho Chadema walipaswa kufanya ni nini?, kwa nini hawakufanya?, na badala yake walifanya nini?.
Soma hapa Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!
Pasco

Kila siku tunasema CDM hawana maana.... hawana dira... hawana mikakati yoyote ya kile wanachoamua na kusimamia...

Hebu mkuu angalia taifa linavyoingia gharama kubwa kufanya kitu ambacho hakina maslahi yoyote wala jipya lolote kwa taifa...

Hebu ona wajumbe wote nguvu zao zipo kwenye muundo wa serikali na muungano.. Kwa jinsi wajumbe wa CCM walivyo wengi ni nadra kupata kitu tofauti na cha awali....

CCM wanataka serikali mbili na itapita.. Sehemu kubwa ya katiba itakayopitishwa itabeba maslahi ya CCM ni viongozi wazembe wa CDM walioshindwa kufikiri impact hii mbeleni ndo sasa wanahaha eti watasusia mchakato mzima then hasara haijulikani atafidia nani...

ni hasara na laana kubwa kuwa na viongozi wa namna yao wasiojua mahitaji ya taifa ni nin,, yaje lini na kwa njia gani..

Huko awali tulipata kusema unaweza ukawa na katiba mpya lakini isiwe suluhisho la uchumi au matatizo yetu.. kama watekelezaji wa katiba ni walewale watungaji ni walewale waliozoea kuishi kwa mazoea huwezi ukapata jipya katika utendaji hata kama kutakuwa na mambo mapya kwenye katiba....

Kwa ufupi wamechemka bora CCM tuliokiri toka Awali katiba haikuwa kipaumbele chetu..
 
Wasapu ndo nini? Shule kitu mhimu sana. Kila wakati unakuja na ushuzi mtupu kama mwendawazimu mwenye makengeza Mbowe

ametumia kiswahili mkuu
kwa msaada zaidi kwako wasapu(whatsapp) ni mfumo au huduma ya kutuma na kupokea ujumbe mfupi wa maandishi,picha za mnato,picha za video,sauti iliyorekodiwa na nyimbo bila gharama yoyote ila tu unatakiwa kuwa na na huduma ya intaneti katika simu yako..
 
Ukiangalia mapendekezo ya kanuni za Bunge la Katiba utaona zinakubaliana kabisa na madaraka ya Bunge hilo kwa mujibu wa Kifungu cha 25 cha Sheria ya Mapitio ya Katiba.
 
Ukiangalia mapendekezo ya kanuni za Bunge la Katiba utaona zinakubaliana kabisa na madaraka ya Bunge hilo kwa mujibu wa Kifungu cha 25 cha Sheria ya Mapitio ya Katiba.
Nikweli,

Nadhani njia kuu ya wazalendo hapa ni kupigania mabadiliko ya sheria kifungu hicho cha 25 ili waweze kushinikiza tena mabadiliko ya kanuni zote zenye utata.
 
Pasco,

Upataji wa katiba ni mchakato, hakuna taifa lililowahi kubadilisha katiba yake ndani ya miaka mitano baada ya kuitunga,

Mfano Tanganyika ilichukua miaka sita kupata katiba kutoka kwa Waingereza ijapokuwa halikuwa koloni lake, Kenya iliwachukua miaka 15 kupata katiba tangu mchakato wake uanza, Tanzania mapambano ya kudai katiba yalianza tangu kuundwa kwa Azimio la Zanzibar 1992, na leo ndio tunataka kuipata.

Kuuacha mchakato huu uendelee ilihali unafinyanga matakwa ya uum ni uhaini, kikundi kidogo (ccm) kinalisaliti taifa halafu unapendekeza tuache ipite tukitaraji mpaka Chadema iingie madarakani????? Isiposhida 2015 inamaana taifa litaendelea kutopea kwenye lindi la uzandiki huu???

Noooooo hapa kinachofuata ni kuvu ya umma na sio nguvu ya siasa,

Msongo wako wa mawazo unasababishwa na tabia yako ya hofu ya usiyoyajua (fear of unknown), mimi ninatumaini mjadala wa katiba utafanikiwa sana tu, ila ile tabia ya umimi inayojengeka kwa wanasiasa mara nyingi husema ''hoja yetu ni bora kuliko ya wapinzani'' au kuamini kwamba wao ndio wanaajenda ya wananchi , kutishia kususa iwapo hoja yao haitapita. Siasa sio uanaharakati, katika historia hata Kina Mwl.JK.Nyerere walidai mambo bungeni kwa uchahe wao kwahoja ambazo hata wabunge wazungu walishawishika na kuwaunga mkono.........................siasa za matamko hazishindi kamwe kwani lazima uheshimu maoni ya wengi, cha msingi ni kutoa hoja zenye mashiko kitaifa ili uungwe mkono.

Sio wabunge woote wa CCM wanaunga mkono serikali mbili hili lazima lieleweke, na kwa bahati nzuri baadhi wamekiri kwenye media kutofautiana na Chama, na sio dhambi.........na kwenye hili uongozi wa CCM haujawaona ni wasaliti wala wahaini ni jambo la kupongeza CCM kwani kwa baadhi ya vyama mwanachama hatakiwi kuwa na mtazamo tofauti.

Umejaribu sana kueleza jinsi sharia ya marekebisho ya katiba mpya inavyolipa bunge nguvu ya kutunga katiba mbadala, hilo ni suala la tafsiri ndio maana lina kupa msongo wa mawazo, Pia lazima ikumbukwe kwamba CCM ina wabunge wengi sana wanaounga mkono rasimu, na pia sio wabunge wote wa CDM wanaunga mkono rasimu 100%

Chadema wakiingia bungeni kwa kauli kwamba '' sisi chadema tunaka a,b, c,d.........'' lazima mjadala uharibike vilevile na CCM.

Kuna mambo yapaswa ujifunze kwenye umuhimu wa kuwa na katiba bora ukilinganisha na ubora wa katiba za vyama va siasa (ukizingatia demokrasia,usawa nk)

Lazma
 
Nilivyokuwa nafahamu mimi (may be wrongly) Bunge la Katiba ni Supreme Council ambayo haifungwi na mipaka yoyote katika kuhoji na hata kurekebisha chochote kadiri itakavyoonekana inafaa. Tatizo ni "uhuni" wa CCM, otherwise ndivyo ilivyotakiwa kuwa.

Nimevunjika moyo sana kwa mambo mengi kidogo , kwani mwanzoni nilitengemea bunge maalumu la katiba linakwenda pale kufanya kazi ya wananchi wa tanganyika waliopoteza uhalisia wao kwa kipindi kirefu. Sasa hali ninayoiona pale ni kitu tofauti kabisa kumbe watu wamekusanywa waende pale ili mwisho wasiku wapige kura za ndio kama ambavyo wabunge wa bunge la bajeti wanavyopitisha mambo ambayo baadaye yanaigharimu nchi. Sasa changamoto ni je tutafanyaje ili tusipate katiba ya CHAMA TAWALA? Maana waliokwenda wamekwenda kwa ajili ya kufuta au kukataa maoni yaliyotolewa na wananchi ambao wamewachangua ili wawawakilishe. Lakini jambo lingine ambalo naliona KAMA TAYARI UTARATIBU UNAONYESHA KUWA BUNGE LA KATIBA LINAYO MAMLAKA KUFUTA /KUONDOA MAONI YA MWANANCHI NA KUWEKA WANAVYOONA WAO KWANINI TUMETUMIA PESA NYINGI KUKUSANYA MAONI LINGEUNDWA BUNGE HILI LIKATENGENEZA KATIBA ILI KUOKOA GHARAMA.:shock:
 
vipi biashara yako ya vitabu na udhamini wa u.s aid unaendeleaje?.naona mbowe boss wako amepata zali la kushuglikia posho iongezwe japo ifikie laki 6 akulipe na wewe houseboy wake.
Hivi Tanzania bado kuna watu wenye akili mbovu kama zako?... Wewe ni houseboi wa nani?
 
Kila siku tunasema CDM hawana maana.... hawana dira... hawana mikakati yoyote ya kile wanachoamua na kusimamia...

Hebu mkuu angalia taifa linavyoingia gharama kubwa kufanya kitu ambacho hakina maslahi yoyote wala jipya lolote kwa taifa...

Hebu ona wajumbe wote nguvu zao zipo kwenye muundo wa serikali na muungano.. Kwa jinsi wajumbe wa CCM walivyo wengi ni nadra kupata kitu tofauti na cha awali....

CCM wanataka serikali mbili na itapita.. Sehemu kubwa ya katiba itakayopitishwa itabeba maslahi ya CCM ni viongozi wazembe wa CDM walioshindwa kufikiri impact hii mbeleni ndo sasa wanahaha eti watasusia mchakato mzima then hasara haijulikani atafidia nani...

ni hasara na laana kubwa kuwa na viongozi wa namna yao wasiojua mahitaji ya taifa ni nin,, yaje lini na kwa njia gani..

Huko awali tulipata kusema unaweza ukawa na katiba mpya lakini isiwe suluhisho la uchumi au matatizo yetu.. kama watekelezaji wa katiba ni walewale watungaji ni walewale waliozoea kuishi kwa mazoea huwezi ukapata jipya katika utendaji hata kama kutakuwa na mambo mapya kwenye katiba....
Kwa ufupi wamechemka bora CCM tuliokiri toka Awali katiba haikuwa kipaumbele chetu..
Wewe ni CCM? Mpuguso kuna CCM? Sasa Masaki na Oysterbay kuna nini?... Nahisi harufu ya Ulanzi wa Mpuguso..
 
Nimevunjika moyo sana kwa mambo mengi kidogo , kwani mwanzoni nilitengemea bunge maalumu la katiba linakwenda pale kufanya kazi ya wananchi wa tanganyika waliopoteza uhalisia wao kwa kipindi kirefu. Sasa hali ninayoiona pale ni kitu tofauti kabisa kumbe watu wamekusanywa waende pale ili mwisho wasiku wapige kura za ndio kama ambavyo wabunge wa bunge la bajeti wanavyopitisha mambo ambayo baadaye yanaigharimu nchi. Sasa changamoto ni je tutafanyaje ili tusipate katiba ya CHAMA TAWALA? Maana waliokwenda wamekwenda kwa ajili ya kufuta au kukataa maoni yaliyotolewa na wananchi ambao wamewachangua ili wawawakilishe. Lakini jambo lingine ambalo naliona KAMA TAYARI UTARATIBU UNAONYESHA KUWA BUNGE LA KATIBA LINAYO MAMLAKA KUFUTA /KUONDOA MAONI YA MWANANCHI NA KUWEKA WANAVYOONA WAO KWANINI TUMETUMIA PESA NYINGI KUKUSANYA MAONI LINGEUNDWA BUNGE HILI LIKATENGENEZA KATIBA ILI KUOKOA GHARAMA.:shock:

Umeuliza swali zuri sana mkuu
 
Najiuliza sana, hivi kwamfano kwenye hiyo Sheria ya mabadiliko ya katiba ambayo ilitungwa awali kabisa, wanasheria wetu mahiri na wazee wetu wote hawakuona kasoro hizo????

Kasoro waliziona na ndo maana wakapaaza sauti zao toka mwanzo lakini maccm wakawabeza kuwa wana njaa ya kwenda Ikulu kunywa juice na chai. Si unamkumbuka yule mnyama flani alivyo tembea kila mahali akiwabeza wapinzani?
Tujikite katika kuanza kuliandaa Taifa wajue kwamba hakuna kitakacho tokea kwenye hili Bunge. Upinzani ujiandae kuiweka hii kuwa agenda katika uchaguzi ujao.
 
kumbe mpuguso hakuna CCM? unachekesha!!!!
Na wewe vunajiita CCM? Hata bajaji huna? Wenye CCM ni watu wanaohesabika!... Hawazidi 200!... Tena wanafahamika.. Siyo wewe unayetoka kwenye familia za "kajamba nani!"... Ushirika, mpuguso mpaka kaporogwe hakuna mwana - CCM!!!...
 
Back
Top Bottom