Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2018
Posts
8,013
Reaction score
14,263
Je Yesu alikufa siku tatu kama alivyojitabiria au siku tatu (masaa 72) hazikufika au hakumaanisha siku tatu kamili? ( siku tatu za Yesu zilikuwa za masaa 72?)
Mathayo 12: 40 '' Kwa maana kama vile Yona+ alivyokuwa katika tumbo la yule samaki mkubwa siku tatu mchana na usiku, ndivyo Mwana wa binadamu+ atakavyokuwa katika moyo wa dunia+ siku tatu mchana na usiku'' (Mathew 12:40For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth.)
Kumbuka hili ni jibu la Yesu wakati akitaka kuwathibitishia mafarisayo na walimu waliotaka ishara kutoka kwake Mathayo12.38 Ndipo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema: “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” . Hivyo akatumia mfano wa Yohana kwa kuwaambia atakaa chini ya moyo wa ardhi kama alivyokaa Yona kwa siku tatu. Kwa hiyo hii ilibaki mioyoni mwao kama kipimo cha ukweli wake. Angefufuka kabla siku hizo tatu hazijafika mafarisayo wasingemuelewa. Wangemuita muongo na hakutoka kwa Mungu.

Kuna waalimu hufundisha kuwa Yesu alisulubiwa Ijumaa na wanaiita Ijumaa kuu ( Good Friday) na akafufuka Jumapili asubuhi na mapema.Je kuna ukweli hapo? Tukiamini kwamba Yesu alikufa Ijumaa mchana na akazikwa jioni kabla ya Sabato na kufufuka Jumapili asubuhi sana, Je siku Tatu zilitimia?
Kwa hesabu hizi alilala ijumaa usiku, akashinda jumamosi mchana na jumamosi usiku.
Je hizo ni siku tatu mchana na usiku kwa maana ya three days and three nights.

Wajuzi wa mambo tuelimishane hii ipoje
 
Kwa maoni yangu ni kuwa Bishara hiyo ya Yesu ilikusudia kuonesha kwamba YEYE YESU HATOUWAWA bali ATAINGIZWA KATIKA MOYO WA NCHI AKIWA BADO ANAO UHAI WAKE KAMA AMBAYO YONA ALIINGIA KWENYE TUMBO LA NYANGUMI AKIWA NA UHAI WAKE

Na hiyo Ndiyo hali pekee inayoweze kuwa fananisha YESU na YONA kwenye hayo matukio yao mawili, vinginevyo hatuwezi kupata ufanano wowote wa matukio hayo mawili.
 
Mkuu tatizo lipo kwenye hizo siku kuwa hazifiki tatu kwa maana ya masaa 72
 
Ikumbukwe kwamba wayahudi walikusudia Kumsulubisha YESU (kumuua juu ya Msalaba) ili kuithibitishia Jamii kuwa YESU sio ukweli bali ni Mlaaniwa, hivyo kwa maneno Haya ya YESU ambayo umeyanukuu yanatoa jibu kuwa Njama za Nitaka nife juu ya Msalaba hazita tumia badala yake NITAINGIA KATIKA MOYO WA NCHI NIKIWA HAI NA KUTOKA NIKIWA HAI KAMA ILIVYOTOKEA KWA YONA.
 
Ukiesabu masaa, ata masaa 48 hayafiki, mfano kutoka ijumaa saa sita mpaka jmos saa sita ni 24hrs, kutoka jmos saa sita iyi mpaka jpl asubui ni karibu 18hrs, sasa apo nin haswa unataka, japo nnavyo ona ni kama walihesabu siku bila kuzingatia masaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikumbukwe kwamba wayahudi walikusudia Kumsulubisha YESU (kumuua juu ya Msalaba) ili kuithibitishia Jamii kuwa YESU sio ukweli bali ni Mlaaniwa, hivyo kwa maneno Haya ya YESU ambayo umeyanukuu yanatoa jibu kuwa Njama za Nitaka nife juu ya Msalaba hazita tumia badala yake NITAINGIA KATIKA MOYO WA NCHI NIKIWA HAI NA KUTOKA NIKIWA HAI KAMA ILIVYOTOKEA KWA YONA.
duuh!
 
Utaratibu wa Wayahudi ktk kuhesabu siku enzi zile, haukuwa sawa na huu wa kwetu - mfumo wa saa 24.
Siku ya Ijumaa ilianza siku ya Alhamis jioni baada ya jua kushuka - siku ya kwanza
Siku ya Jumamosi ilianza siku ya Ijumaa jioni baada ya jua kushuka - siku ya pili
Siku ya Jumapili ilianza siku ya Jumamosi jioni baada ya jua kushuka - siku ya tatu.
 
N kweli mkuu walikuwa wanahesabu kwa utaratibu kwamba jua likizama siku inaisha na nyingine inaanza.Kwa hiyo kama alizikwa Ijumaa jioni na kufufuka jumapili asubuhi siku tatu hazifiki
 
"Mathayo 12: 40 '' Kwa maana kama vile Yona+ alivyokuwa katika tumbo la yule samaki mkubwa siku tatu mchana na usiku, ndivyo Mwana wa binadamu+ atakavyokuwa katika moyo wa dunia+ siku tatu mchana na usiku".

Kama kwa hesabu ya wayahudi siku huanza jioni maana yake mchana wa ijumaa unafutwa kwa kuwa yesu hajaingia kaburini: Siku ya kwanza imeanza jumamosi na tunapata usiku na mchana wake. Siku ya pili inaanza jumapili jioni na tunapata usiku mmoja na kukosekana mchana wa Jumapili.

Au jaalia ijumaa mchana iwe mchana na jumamosi iwe usiku: Hapo tunapata mchana wa ijumaa na jumamosi na usiku wa jumamosi na jumapili: Mchana wa jumapili na usiku wa jumatatu unakosekana.
Bado andiko la Biblia halitusaidiee kuona ishara ikitimia kama kwa Yona.

SIKU TATU MCHANA NA USIKU HAZIPO:

Tafakuri:
Either aliyoyasema Mwana hayakutokana na Baba. Yaani hayakuwa ni ufunuo!
Ushahidi 1: Katika Qur'an Mwenyezi Mungu anasema: Hawakumsulubisha wala hawakumuua! Surat Nisaa (4:157)
Ushahidi 2: Kuna mtu mmoja alipewa msalaba wa Yesu aubebe na hakuna andiko linaonyesha ule msalaba aadaye alirudishiwa Yesu.

Nachelea usema kuwa ule haukuwa mpango wa Mungu. Kwani Mungu husikia maombi ya muombaji. Na mtume wake hasemi jambo likawa kinyume!! Siku tatu zipo wapi????
 
Utaratibu wa Wayahudi ktk kuhesabu siku enzi zile, haukuwa sawa na huu wa kwetu - mfumo wa saa 24.
Siku ya Ijumaa ilianza siku ya Alhamis jioni baada ya jua kushuka - siku ya kwanza
Siku ya Jumamosi ilianza siku ya Ijumaa jioni baada ya jua kushuka - siku ya pili
Siku ya Jumapili ilianza siku ya Jumamosi jioni baada ya jua kushuka - siku ya tatu.
Hapa kwa ufupi ulitakiwa useme hivi "Siku hubadilika baada ya kuzama jua"

Huo ndio usawa.

Nipo .....
 
Kwa kawaida siku kwa wa yahudi ilikuwa na masaa 12 sio 24 hivyo alikufa ijumaa saa tisa mpaka saa 12 ijumaa ilikuwa siku ya kwanza jumamosi saa 12 iliisha siku ya pili na tayari ilianza jumapili yaani siku ya 3 kwa hesabu hizo Yesu alifufuka siku ya Tatu jumapili

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mtazamo wangu maana wanasema siku ya 3 akafufuka

Ijumaa inaisha saa 6 usiku...kwa iyo ilikuwa bado siku ya kwanza
Jumamosi inaisha saa 6 usiku kwa iyo ilikuwa kama siku ya pili
Jumapili ambayo ni siku ya tatu kabala ya saa6 usiku akafufuka

Mtazamo ni huo

If it isn’t perfect ,it’s not good enough
 
Mkuu tatizo lipo kwenye hizo siku kuwa hazifiki tatu kwa maana ya masaa 72
Kuna baadhi ya vitu havifanyiwi hesabu kwa kutumia namba kamili, ndio maana kukawa na somo la MAKADIRIO!..
Mojawapo ni hilo, toka Ijumaa mpaka Jumapili ni siku tatu kikawaida. Sawa na birthday yako (ukizaliwa leo tarehe 16 saa 4 Usiku ina maana utakuwa unaiadhimisha ikifika tarehe 16 saa 4 usiku?)
 
Back
Top Bottom