Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Hivi ili iitwe siku ni lazima yapite masaa 72? Unaposikia ziara ya Rais flani siku mbili anakuja leo anaondoka kesho huwa yamefika masaa 48?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi naongelea hizi ambazo zinasema atakaa kaburini siku tatu mchana na usiku.

Mathew 12:38-40

38Then some of the Pharisees and teachers of the law said to him, "Teacher, we want to see a miraculous sign from you."39He answered, "A wicked and adulterous generation asks for a miraculous sign! But none will be given it except the sign of the prophet Jonah.40For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth.
 
Huo utaratibu wa kuhesabu siku kuanzia saa 6 usiku ulianzishwa na Warumi ,haukuwepo wakati wa Yesu
Wewe Nyaigela wewee!
Kwahiyo unataka kusema Bwana Yesu hajawakuta Warumi wakitawala?
Gavana wa Kirumi wa Jimbo la Judea aliyemhukumu Yesu kwa treason alikuwa ni nani kama si Mrumi Ponsio Pilato?
 
Kwa kawaida siku kwa wa yahudi ilikuwa na masaa 12 sio 24 hivyo alikufa ijumaa saa tisa mpaka saa 12 ijumaa ilikuwa siku ya kwanza jumamosi saa 12 iliisha siku ya pili na tayari ilianza jumapili yaani siku ya 3 kwa hesabu hizo Yesu alifufuka siku ya Tatu jumapili

Sent from my iPhone using JamiiForums

Kiongozi umepitia tena hii hoja yako? kama umepitia tena unaona ndio jibu sahihi au umeleta mada mpya yenye kuleta maswali?

twende sawa saa 9 ijumaa mpaka saa 12 jion ya ijumaa ni siku ya kwanza
haya saa 12 jioni ya ijumaa mpaka 12 asubuhi ya jumamosi ni siku ya pili
saa 12 asubuhi ya jumamosi mpaka 12 jioni ni siku ya tatu
haya yesu kafufuka jumapili asubuhi yani kwa jibu lako ni siku ya nne! hata mimi sijui mambo ya biblia ila umenidanganya
 
Kwa maoni yangu ni kuwa Bishara hiyo ya Yesu ilikusudia kuonesha kwamba YEYE YESU HATOUWAWA bali ATAINGIZWA KATIKA MOYO WA NCHI AKIWA BADO ANAO UHAI WAKE KAMA AMBAYO YONA ALIINGIA KWENYE TUMBO LA NYANGUMI AKIWA NA UHAI WAKE

Na hiyo Ndiyo hali pekee inayoweze kuwa fananisha YESU na YONA kwenye hayo matukio yao mawili, vinginevyo hatuwezi kupata ufanano wowote wa matukio hayo mawili.
mkuu nikiongezea kidogo hapa, kwanz akwenye biblia hakuna mfumo wa kuhesabu siku kwa masaa 24, kama tufanyavyo sasa walichokua wanahesabu ni siku yaani jua lichomozapo na kuzama, hivyo Yesu alikufa mchana wa ijumaa saa tisa akashinda mchana wa jumamosi na jumapili asubuhi akafufuka maana yake ni siku ya tatu hivyo asemacho mtoa hoja ni hoja dhaifu kwa msomaji mzuri wa maandiko.
 
Wewe Nyaigela wewee!
Kwahiyo unataka kusema Bwana Yesu hajawakuta Warumi wakitawala?
Gavana wa Kirumi wa Jimbo la Judea aliyemhukumu Yesu kwa treason alikuwa ni nani kama si Mrumi Ponsio Pilato?
Mkuu hujanielewa pamoja na utukutu wangu. Nilichokisema huu utaratibu wa kuhesabu masaa kuanzia saa sita usiku haukuwepo wakati Yesu akisulibiwa. Ulikuja baadaye.
 
mkuu nikiongezea kidogo hapa, kwanz akwenye biblia hakuna mfumo wa kuhesabu siku kwa masaa 24, kama tufanyavyo sasa walichokua wanahesabu ni siku yaani jua lichomozapo na kuzama, hivyo Yesu alikufa mchana wa ijumaa saa tisa akashinda mchana wa jumamosi na jumapili asubuhi akafufuka maana yake ni siku ya tatu hivyo asemacho mtoa hoja ni hoja dhaifu kwa msomaji mzuri wa maandiko.
Mkuu kama kalugha ka kikoloni kanapanda ,hebu jaribu kusoma Mathayo 12:38-40 . Utaona kabisa Yesu akisema Mausiku matatu na maMchana matatu , kwa hesabu zako hapo hatupati huo muda

38Then some of the Pharisees and teachers of the law said to him, "Teacher, we want to see a miraculous sign from you."39He answered, "A wicked and adulterous generation asks for a miraculous sign! But none will be given it except the sign of the prophet Jonah.40For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth.
 
Ijumaa Saa 9 Alasiri mpaka saa 5:59:59:99 usiku ni siku moja na usiku mmoja,
Jumamosi Saa 6:00:00:00 usiku mpaka saa 5:59:59:99 usiku ni siku ya pili na usiku wa pili,
Jupili Saa 6:00:00:00 usiku mpaka wakati anafufuka Alfajiri ya jumapili ni siku ya tatu na usiku wa tatu, maandiko hayakutaja masaa yalitaja siku na usiku

Hivo maandiko na maneno ya Yesu yalikua sahihi siku tatu mchana na usiku .
 
Mkuu kama kalugha ka kikoloni kanapanda ,hebu jaribu kusoma Mathayo 12:38-40 . Utaona kabisa Yesu akisema Mausiku matatu na maMchana matatu , kwa hesabu zako hapo hatupati huo muda

38Then some of the Pharisees and teachers of the law said to him, "Teacher, we want to see a miraculous sign from you."39He answered, "A wicked and adulterous generation asks for a miraculous sign! But none will be given it except the sign of the prophet Jonah.40For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth.
pamoja na hilo mzee hoja yangu ipo wazi kabisa so rudia comment yangu vizuri kuelewa uamue mwenyewe
 
Kumbuka hapa jamaa walikuwa hawana imani naye na hivyo anataka kuwaaminisha ( kwa kuwapa ishara ambayo itakapotokea wamwamini) kwa ishara ya kukaa kaburini kama Yona alivyokaa tumboni mwa samaki
Soma vizuri zile aya za biblia zinasema, Siku tatu mchana na usiku ( three days and three nights)
Mathayo 12:38-40 Ndipo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema: “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.”+ 39 Akajibu, akawaambia: “Kizazi kiovu na chenye uzinzi+ kinaendelea kutafuta ishara, lakini hakuna ishara kitakachopewa isipokuwa ishara ya nabii Yona.+ 40 Kwa maana kama vile Yona+ alivyokuwa katika tumbo la yule samaki mkubwa siku tatu mchana na usiku, ndivyo Mwana wa binadamu+ atakavyokuwa katika moyo wa dunia+ siku tatu mchana na usiku.[/I][/U][/B]
Kwa tafsiri yako ya siku 3 Mchana na usiku bado tunarudi pale pale MAKADIRIO.
Yesu alikufa saa 9 alasiri (mchana) akapitisha jumamosi (asubuhi na usiku) Jumapili asubuhi walivyoenda wakakuta kafufuka!, So bado siku 3 zinakamilika unless unataka neglect siku ya kwanza kisa nusu siku lakini saa 9 alasiri mpaka 12 jioni bado kulikuwa ni muda wa jua so ni mchana!.
Luka 23:44-47
Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.
Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.
Alipokwisha kusema hayo alikata roho. Yule akida alipoona yaliyotukia, alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki.

Tunaona asubuhi wakakuta kafufuka.
Luka:24.1-3
Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu.
 
Mambo ya dini waachie wabobezi wakujuze. Maana tunachofanya kwa Sasa Ni adhimisho tu. Mfano: kwenu mtu akizikwa mnasema matanga siku tatu au nne. Huwa mnahesabu VP?

Kama uliwahi kusafiri nje ya nchi unajua hata Kama umefika saa tano usiku wanahesbu siku Mona.....

Cha msingi tambua alikufa na siku ya tatu alifufuka Kama maandika yasemavyo.

Pia sabatho ilikua Ni siku ya Jumamosi lakini kutokana na umuhimu wa ufufuko wa Kristu Jumapili (ambayo ndio siku ya tatu) ilifanywa kuwa ndio siku ya Bwana
 
Hizo krismas na pasaka ni sherehe za kipagani tu ,hazipo kibiblia , kwani wewe umeziona zimeandikwa kwenye Biblia hadi useme zina utata?
Wayahudi walimuua Yesu? Wayahudi hawakuwa na huo uwezo wa kumuua Mungu mkuu

Yohana10:17-18
''Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu''

Alaaaaaaaaa Kumbe hizo ni sikukuu za Kipagani??? kwa hiyo wanaosherehekea hizo sikukuu ni wapagani??. Anyway nashukuru kwa uthibitisho huo.

[ohana10:17-18]
Halafu Tena anamlalamikia Mungu kumwacha???
Marko 15:34-37 Neno: Bibilia Takatifu.
Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi, Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Itakuwa hakuwa Yesu!
 
Kaka mtukutu.
Unapoanzisha mjadala jaribu kufungua macho na ubongo upate pia kujifunza upande usioujua. Kuna vitu havihitaji nguvu nyingi kuvitetea. Ubainifu wake kwa wengineo ni maneno machache tu na uchokonozi wa kifikra ili kuzindua!
 
endelea mkuu nakusikiliza
 
Je Yesu alikufa siku tatu kama alivyojitabiria au siku tatu (masaa 72) hazikufika au hakumaanisha siku tatu kamili? ( siku tatu za Yesu zilikuwa za masaa 72?)
Mathayo 12: 40 '' Kwa maana kama vile Yona+ alivyokuwa katika tumbo la yule samaki mkubwa siku tatu mchana na usiku, ndivyo Mwana wa binadamu+ atakavyokuwa katika moyo wa dunia+ siku tatu mchana na usiku'' (Mathew 12:40For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth.)
Kumbuka hili ni jibu la Yesu wakati akitaka kuwathibitishia mafarisayo na walimu waliotaka ishara kutoka kwake Mathayo12.38 Ndipo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema: “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” . Hivyo akatumia mfano wa Yohana kwa kuwaambia atakaa chini ya moyo wa ardhi kama alivyokaa Yona kwa siku tatu. Kwa hiyo hii ilibaki mioyoni mwao kama kipimo cha ukweli wake. Angefufuka kabla siku hizo tatu hazijafika mafarisayo wasingemuelewa. Wangemuita muongo na hakutoka kwa Mungu.

Kuna waalimu hufundisha kuwa Yesu alisulubiwa Ijumaa na wanaiita Ijumaa kuu ( Good Friday) na akafufuka Jumapili asubuhi na mapema.Je kuna ukweli hapo? Tukiamini kwamba Yesu alikufa Ijumaa mchana na akazikwa jioni kabla ya Sabato na kufufuka Jumapili asubuhi sana, Je siku Tatu zilitimia?
Kwa hesabu hizi alilala ijumaa usiku, akashinda jumamosi mchana na jumamosi usiku.
Je hizo ni siku tatu mchana na usiku kwa maana ya three days and three nights.

Wajuzi wa mambo tuelimishane hii ipoje
Kwa kweli hizi hesabu za makanisani zinapingana na hesabu zilizoandikwa hii ni hatari kwa afya ya mwanadamu
 
Siku zinazozungumzwa ni za matukio, na co cku kamili za kibinadamu yaani masaa 72,,
-siku ya kwanza kafara ya ukombozi ilitolewa kwa kifo cha Yesu Kristo (Ijumaa)
-siku ya pili, Yesu alipumzika kaburini(Jumamosi )
-siku ya tatu alifufukA(Jumapili )

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu maandiko yanasema USIKU na MCHANA kwa mda wa siku 3, kama hakuna USIKU 3. na MCHANA 3 hicho unachoamini ni uongo
 
mkuu nikiongezea kidogo hapa, kwanz akwenye biblia hakuna mfumo wa kuhesabu siku kwa masaa 24, kama tufanyavyo sasa walichokua wanahesabu ni siku yaani jua lichomozapo na kuzama, hivyo Yesu alikufa mchana wa ijumaa saa tisa akashinda mchana wa jumamosi na jumapili asubuhi akafufuka maana yake ni siku ya tatu hivyo asemacho mtoa hoja ni hoja dhaifu kwa msomaji mzuri wa maandiko.
Maandiko yanataka USIKU 3 na MCHANA 3 , ili siku 3 zikamilike, nnje ya hapo hakuna siku tatu msilazimishe mambo
 
Kwa kawaida siku kwa wa yahudi ilikuwa na masaa 12 sio 24 hivyo alikufa ijumaa saa tisa mpaka saa 12 ijumaa ilikuwa siku ya kwanza jumamosi saa 12 iliisha siku ya pili na tayari ilianza jumapili yaani siku ya 3 kwa hesabu hizo Yesu alifufuka siku ya Tatu jumapili

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu hizo siku tatu za kiyahudi za Masaa kuminambili kila moja Turejee kitabu gani?
 
N kweli mkuu walikuwa wanahesabu kwa utaratibu kwamba jua likizama siku inaisha na nyingine inaanza.Kwa hiyo kama alizikwa Ijumaa jioni na kufufuka jumapili asubuhi siku tatu hazifiki
usiwe mzito kuelewa walikuwa wanahesabu siku sio masaa
 
Back
Top Bottom