Kwa tafsiri yako ya siku 3 Mchana na usiku bado tunarudi pale pale MAKADIRIO.
Yesu alikufa saa 9 alasiri (mchana) akapitisha jumamosi (asubuhi na usiku) Jumapili asubuhi walivyoenda wakakuta kafufuka!, So bado siku 3 zinakamilika unless unataka neglect siku ya kwanza kisa nusu siku lakini saa 9 alasiri mpaka 12 jioni bado kulikuwa ni muda wa jua so ni mchana!.
Luka 23:44-47
Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.
Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.
Alipokwisha kusema hayo alikata roho. Yule akida alipoona yaliyotukia, alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki.
Tunaona asubuhi wakakuta kafufuka.
Luka:24.1-3
Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu.