Utatu kati ya serikali, elimu na uchumi
Serikali.
Ili serikali iweze kukuza uchumi ni lazima kufanya kwanza maboresho katika mifumo yake ya elimu, kwa kuweka miundo mbinu wezeshi kumwezesha mwanafunzi kujifunza mfano majengo ya maabara na ya utafiti yawe hata kuanzia shule za msingi watoto wajifunze wakiwa na nyenzo muhimu wakisaidiwa na tehema, kwa Sasa tehema inafundishwa kama soma lakini nyenzo muhimu kama kompyuta kuwasaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo zinahitajika sana maana kumbukumbu kwa njia ya vitendo hujengwa kwa kiasi kikubwa, kulingana na mabadiliko ya teknolojia vitu vingi vya kuhusu uvumbuzi vimewekwa kwenye mitandao kwahiyo ili kwenda na kasi hii ya ukuaji wa teknolojia lazima serikali ihakikieshe wanafunzi wanapati mafunzo na nyenzo muhimu kama kompyuta.
Kama tunavyojua sayansi imekuwa muhimili muhimu kusaidia kuboresha utendaji na uzalishaji bora katika kila idara kama vile viwandani, uvuvi, kilimo, afya n.k katika kutoa vifaa vya kusaidia urahisishaji wa kazi na uzalishaji pia na ubora zaidi wa kazi basi kutokana na faida hizi na umuhimu mkubwa wa hii sayansi maana serikali inatumia fedha nyingi kunuunua na kuagiza hivi vifaa vya kiteknolojia kutoka nchi za nje au hata kununua teknolojia na kuwaleta wataalamu wake, ifike wakati kuwa na sehemu za kusaidia kukuza wazo (incubation centre) hii kuanzia kwenye shule za msingi licha ya kuwa na hiyo incubation centre pia kuwa na mazingira zaidi wezeshi mfano kuwa na klabu za vikundi mbalimbali kwa ajili ya kukuza na kuwahamasisha wavumbuzi mbalimbali.
swala la kujifunza ni kwamba nchi zilizo endelea ziliweka fedha kwenye tafiti na ubunifu uliowezesha kuja na vitu vingi vya kiteknolojia vikivyosaidia kukua kwa uchumi wao hadi leo wanazidi kuwekeza huko maana ndo nyenzo muhimu kwenye kufanya kasi ya maendeleo ya viwanda, kuboresha huduma za afya na kijamii kusaidia uchumi kwa ujumla kukua kwa pato la nchi kwa kuuza hiyo teknolojia au vitu wanavyozalishwa kutokana na hiyo teknolojia.
Elimu
Hapa tunahitaji mfumo mpya wa elimu na mitaala mipya ambayo itaendana na mfumo wa maisha wa sasa mfano kibiti boys wanautaratibu wa kubalishana wanafunzi na serikali ya Cuba japo mmoja au wawili waje kwetu na wawili waende kwao lakini yule mwanafunzi alivyokuja huku kibiti hakumaliza na sisi sababu alisema sisi tuna mifumo migumu sana badala ya kupata ile dhana ya msingi tuna jifunza mambo ya nyuma ambayo sasa hivi hayatumiki kama vile wakati wao wanasema wanajifunza kuanzia pale walipoishia wenzao kwenye teknolojia wanapata ile dhana ya msingi (basic concepts) ya hicho kitu kisha inasaidia kufikiri na kuendelea ile dhana kwa mapana zaidi ndio maana inakuwa rahisi sana kwao kuja na bunifu mpya
Walimu au wakufunzi yawapasa wawe wabunifu ili kuwafanya wanafunzi kupenda somo husika kigenzo cha mwalimu kuwa mkali haimfanyi mwanafunzi alipende somo bali tu itamjengea woga wa mwalimu na somo ndo maana hata kama mwalimu akitoa mazoezi mwanafunzi hata kama hawezi itamlazimu anakili kwa wenzake ili tu kuepusha kuadhibiwa na mwalimu vivyohivyo kwenye swala la ufaulu wanafuzi wengi wanaogopa kufeli sababu ya kutojengewa misingi hadi kufanya udanyanyifu wa mitihani
Siku zote ukimjengea mtu mazingira ya kupenda kitu, tabia ile hujijenga hata kama hapo mwanzo alikuwa hakipendi mfano watu wengi husema hesabu aus masomo ya sayansi ni magumu si kweli hakuna kitu kigumu dunia kukiwa na juhudi na jitihada pamoja na mazingira mazuri ya kujifunza hakuna ugumu wowote ila tu uelewa utakuwa tofauti kulingana na kila mtu alivyo umbwa au kuazaliwa.
Ubunifu wa walimu na wakufunzi mfano kwa mimi shule ya msingi mwalimu wa sayansi alikuwa anakuja na michoro na zile skeletoni darasani anakuja kufundishwa kwa upendo na kutuambia jinsi viungo na mifumo ya mwili inavyofanya kazi, kupanda maharage kwenye kopo lenye pamba na kuona ukuaji wake ilitujengea uelewa wa ukuaji wa mmea.
Mfano mwingine ni wakati tukiwa sekondari mwalimu wetu wa somo la hesabu alikuwa akitoa zawadi kwa waliokuwa wanajitoa kujibu maswali na kutoa majaribio ya ushindani na kutangaza zawadi kwa mshindi wa kwanza hii ilifanya wengi tulipende somo lake na kukuza ufaulu.
Mfano mwingine ni wakati niko kidato cha sita pamoja na chuo kikuu baadhi ya walimu na wakufunzi walitumia mtindo wa kwamba kabla hajafundisha mada mpya anatuambia jina la hiyo mada alafu anatuambia tukaisome tuje tujadiliane kwenye makundi alafu kwenye kipindi chake tuwasilishe kila kundi tulicho fanya akitaka kila mtu ashiriki kila hatua alafu yeye ndo aje afundishe na ajazie vitu vingine kwakweli hii ilitufanya tusome vitabu na kutafuta kwenye mtandao vitu mbalimbali kuhusu mada husika, hii mtindo ulitufungua akili nakutufanya watu wenye kujituma wenye kutujengea ujasiri, ilikuza ufaulu, kupenda somo na kulielewa somo zaidi.
Uchumi
Mfano nchi zilizoendelea kama China miradi ya kujenga barabara ya kisasa wanakuja nayo wanafunzi kutoka vyuo na pia mfano kwenye mifumo ya ufugaji wa kisasa na kilimo ni bunifu za wanafunzi wa vyuo, kama vile marekani pia na nchi zilizoendelea mfano mtu kama bill gate alitumia robo tatu ya mda wake akiwa chuo kujifunza zaidi kuhusu software ambayo alikuja na bunifu yake ya microsoft ambayo ilimfanya kuja kuwa tajiri wa kwanza duniani na mpaka kuliingizia taifa fedha nyingi, pia mark zuckerberg aliweza kuazisha facebook akiwa chuoni pia hawa watu mpaka sasa hivi wanaliingizia taifa fedha nyingi wanachangia ukuaji wa uchumi kwa asilimia kubwa.
Kama inavyonekana kwa uhalisia kwenye nchi zilizo endelea udhabiti wa utawala bora wa serikali na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika elimu ndio ulio leta mapinduzi makubwa ya kiuchumi katika nchi zao, kukiwa na siasa safi, mifumo bora ya utawala wa sheria na haki, uwajibishwa watu au viongozi katika nafasi zao, uzalendo, kujituma kila mtu katika nafasi yake na kuchukia rushwa kutasaidia nchi kusonga mbele.
Kwahiyo huu utawala wao bora na mifumo bora ya elimu yao umezalisha watu sahihi na watu muhimu walikuja kusimama na kuwajibika katika nafasi zao kusaidia kuzalisha watu waliokuja na miradi, bunifu na mikakati iliyosaidia kukuza teknolojia yao iliyopelekea mapinduzi ya viwanda, kilimo na mifugo hali iliyofanya kukua kwa pato la taifa lao.

Upvote
1