Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Habari zenu wakuu - Nitatoa ufafanuzi kama kichwa kinavyoeleza, Hizi hoja zote ni matokeo ya uchambuzi wangu wa kina wa biblia:

NInakubaliana na fumbo la utatu wa Mungu - Baba, Mwana na Roho lakini katika mtizamo wa kimajukumu na siyo Mamlaka.

Tuweke theology pembeni kisha tujadili neno lenyewe, Kwanini nasema Utatu ni wa majukumu na siyo mamlaka ? [Kama christians wengi wadaivyo kwamba YHWH, Yesu na RohoMtakatifu wana uwezo sawa kimamlaka], Sababu zangu ni:

1. Mungu ni Mmoja, Nafsi Moja — Sio Nafsi Tatu.
“Sikia, Ee Israeli, BWANA Mungu wetu, BWANA ni mmoja.”
(Kumbukumbu 6:4)
“Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu hapana Mungu.”
(Isaya 45:5)
Mungu ni nafsi moja tu, anasema “Mimi,” si “sisi.” Hakuna viini vitatu vya Mungu.

2. Yesu ni Mungu kwa Sababu ni Mwana wa Mungu — ila si Mkuu Kama Baba.
-"Kwani kijana wa miaka 35 si mtu mzima aliyekomaa sawa tu na baba yake-Je hilo linampa nafasi ya kuwa sawa na baba yake? Bado atabaki mtoto anayepaswa kutii simple.
“Naye Neno alikuwa Mungu... naye akawa mwili...” - Yaani Yesu pia alikua ni Mungu kamili kwasababu alirithi uungu ule kwa baba yake na akaja kupitia mwili.
(Yohana 1:1,14)
“Katika yeye unakaa utimilifu wote wa uungu...” - unakaa utimilifu wa uungu - Si kwamba yeye ndiye Mungu mkuu.
(Wakolosai 2:9)
“Baba peke yake ndiwe Mungu wa kweli...”
(Yohana 17:3)
Yesu ana uungu, lakini anamtambua Baba kuwa Mkuu kuliko yeye.

3. Yesu si Baba — Wanatenda Majukumu Tofauti
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)
“Sishuki kutoka mbinguni kufanya mapenzi yangu, bali ya Yule aliyenituma.”
(Yohana 6:38)
Yesu anatenda kazi ya Baba, si Baba mwenyewe.

4. Roho Mtakatifu si Nafsi ya Mungu, Bali ni Nguvu ya Mungu.
“Roho Mtakatifu atakujilia juu...”
(Luka 1:35)
“Mtapokea nguvu, Roho Mtakatifu atakapowajilia...”
(Matendo 1:8)
“Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” - Hutuombea kwa nani ikiwa watu wanaclaim Roho ni YHWH.
(Warumi 8:26)
Roho ni nguvu ya YHWH, si nafsi huru.

5. Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza — YHWH Hana Chanzo wala hazaliwi.
“Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.”
(Wakolosai 1:15)
“Mimi nalitoka kwa Mungu...”
(Yohana 8:42)
Yesu ni mwanzo wa ufunuo wa Mungu; Baba hana mwanzo.

6. Yesu Anafanya Kazi Maalum — Uumbaji na Ufunuo.
“Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa...”
(Wakolosai 1:16)
“Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana.”
(Wakolosai 1:15) - Amebeba sifa zote za YHWH asiyeonekana.
Yesu ni mtendaji mkuu wa Mungu, si chanzo kikuu.

7. Yesu Alijinyenyekesha — Hakujijaribu Kuwa Mkuu Kuliko Baba.
“Alijinyenyekeza mwenyewe, akawa mtii hata mauti...”
(Wafilipi 2:6-8)
Alijua kuwa ana sifa zote za Uungu lakini alimuachia Baba mamlaka ya mwisho.

8. Yesu Hakupewa Ujuzi wa Mwisho — Baba Pekee Anajua kila kitu.
“Siku ile au saa ile hakuna ajuaye, hata malaika, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
(Marko 13:32) - Hata Mwana mwenyewe haijui siku ya mwisho bali Baba.
Majukumu tofauti - mamlaka tofauti.

9. Roho Mtakatifu ni Nguvu ya YHWH Inayotumika na Baba mwenyewe, Mwana, na Sisi kama tukikiri kwa moyo wa dhati tunashare pia.
“Pokeeni Roho Mtakatifu.”
(Yohana 20:22)
“Nitaimimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili...”
(Matendo 2:17)
“Roho wake akaaye ndani yenu...”
(Warumi 8:11)
Roho hutenda kazi ndani ya Mungu na sisi.

10. Mungu Mmoja, Nafsi Moja, Anayetenda Ndani ya Wote.
“Mungu mmoja, aliye Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote, na ndani ya yote.”
(Waefeso 4:6).
Mungu ni mmoja, na anatenda kazi zote tatu:
I. Baba kama chanzo na mkuu.
II. Kumtuma Mwana kama mtendaji na mfunuo.
III. Kuachilia Roho kama nguvu inayotenda ndani ya sisi na ulimwengu

11. Yesu ni Mungu Kamili — Anatenda kama Mungu, Lakini Hadai Usawa na Baba kwasababu Baba ni Baba.
“Umesamehewa dhambi zako.”
(Luka 5:20)
“Wewe u Mwana wa Mungu.”
(Marko 3:11)
“Mungu alikuwa katika Kristo akiupatanisha ulimwengu...”
(2 Wakorintho 5:19)

Yesu anasamehe, anatoa pepo, anapatanisha — ni kazi za Mungu ila;
“Yeye kwa asili alikuwa Mungu, lakini hakudhani kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho...”
(Wafilipi 2:6) - Alijinyenyekesha, hakutaka kuwa sawa na Mungu mkuu.
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)

✅ Yesu ni Mungu, lakini hachukui nafasi ya Baba.
✅ Alinyenyekea, akatenda kwa mamlaka ya Baba.
✅Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza - Mungu hazaliwi na Hana chanzo, Kama angezaliwa ilitakiwa biblia ijibu alizaliwa toka kwa nani?
✅Mwana wa Mungu = Mungu [Genetically].
Lakini Baba ni mkuu kuliko yeye.
✅Roho ni nguvu ya Mungu, inayoshirikiwa na wote — Baba, Mwana, na sisi.
✅Huu ndio Utatu wa Majukumu — si uungu wa nafsi tatu, bali kazi tatu za Mungu mmoja aliye juu ya yote.

🧠 Tufungue mjadala:
Unakubaliana au unapinga? Tufanye hoja kwa hoja - siyo hisia na mihemko kwa heshima ya maandiko ili tupate kuujua ukweli.
📖 Biblia iwe mbele, Theology nyuma.
Nyinyi mungu hana mtoto katika sisi wanadamu.
Mungu si mchezo msifanye simpo mambo.
 
(Isaiah 9:6-7)

Yesu anaitwa, "BABA" wa milele.

Yesu ndiye MUNGU baba huyo huyo,ndiye MUNGU Roho mtakatifu, ndiye MUNGU Mwana.

Mungu mmoja, nafsi moja.
Nakuombea neema ya Mungu ipate kukuangazia katika kuijua kweli yote in Jesus name - Amen.
 
Trinity = Devil's doctrine to confuse the very elect.
No where in the scriptures you will find any of the Apostles including Jesus Christ himself teach of the trinity.

God is one.
His soul is one.
There is none other reigning beside him.

Jesus is the Father.
Flesh & Blood born by Marry was called son.
Holy Spirit is the spirit of God when inside of a man.

Father & Holy Spirit are the titles of God. Son is not God (for God is spirit) but spirit in Son was God.

Father, Son & Holy Spirit share the same name YHWSH (in Hebrew), Jesus in English, Yesu in Swahili.
Don't explain this emotionally.
Explain this while refering to bibble quotes.

2 TIMOTHY 4: 3-4.
For the time is coming when people will not endure sound teaching, but having itching ears they will accumulate for themselves teachers to suit their own passions, and will turn away from listening to the truth and wander off into myths.
 
Napenda kuchangia kama ifuatavyo.
Kwanza inabidi tujue Mungu ni Roho hivyo roho haina umbo linaloweza kuonekana kwa Binadamu zaidi sana Mungu hua anajifunua kwa umbo ambalo anaona ataweza kuonekana kwa macho ya binadamu
Jinsi Mungu alivyo jifunua kwa wanadamu haya ni baadhi ya matukio kwenye biblia
1.kichaka kilichowaka moto kutoka 3:2-6
2.Mtu wa nne kwenye moto daniel 3:25
3.isaya& daniel walimuona Mungu kwenye maono ndoto
Daniel 7:9 ,isaya isaya 6:1
4.Mungu alifanyika mwili katika yesu kristo
Yohana 1:14

Baada ya kuona jinsi Mungu alijifunua kwa binadamu katika nyakati tofauti tofauti hapa tuna kuja kuhitimisha kua Mungu ni mmoja,
kumbukumbu la torati 6: 4 "Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja"
 
Mungu ni muumba au chanzo cha kila kitu, Mungu ni mmoja, Mweza wa yote aliye ndani ya yote na katika yote.

Mungu yupo - lakini kukulazimisha kujua kama ninavyojua wakati haumini chochote ni kazi bure - Nitakua ninaingilia uhuru wako wa kufikiri. Zaidi ninakuombea Neema ya Mungu ikuangazie 🙏🏿
Asa uhatakiwa kutoa hoja, hata ya maandiko yako unayoyaamini...na sio kusema hearsays na speculations...mbona mwenzio amefafanua kea hoja za iamni yake na tumemsoma vizuri tuu
 
Napenda kuchangia kama ifuatavyo.
Kwanza inabidi tujue Mungu ni Roho hivyo roho haina umbo linaloweza kuonekana kwa Binadamu zaidi sana Mungu hua anajifunua kwa umbo ambalo anaona ataweza kuonekana kwa macho ya binadamu
Jinsi Mungu alivyo jifunua kwa wanadamu haya ni baadhi ya matukio kwenye biblia
1.kichaka kilichowaka moto kutoka 3:2-6
2.Mtu wa nne kwenye moto daniel 3:25
3.isaya& daniel walimuona Mungu kwenye maono ndoto
Daniel 7:9 ,isaya isaya 6:1
4.Mungu alifanyika mwili katika yesu kristo
Yohana 1:14

Baada ya kuona jinsi Mungu alijifunua kwa binadamu katika nyakati tofauti tofauti hapa tuna kuja kuhitimisha kua Mungu ni mmoja,
kumbukumbu la torati 6: 4 "Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja"
Ndo huyu alifanyika kwa mwili wa binadamu aliowaumba mwenyewe na wakampa kipigo mpaka kufa??!(Mnasema Mungu hafi).
Hapa ndo maana nakubali hoja za waIslam kwamba jamaa alikuwa mtume tu kama mitume wengine ingawa kwangu mimi hizo hadithi za Wayahudi na Waarabu hazinihusu kama muAfrika.
 
Acha nami nichangie ninachokiamini:

- 2 Wakorintho 13:14 – Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu na uwe nanyi nyote.

Wanaoukataa Utatu mara nyingi hufanya hivyo kwa sababu ya upungufu wa ufunuo au elimu sahihi ya Maandiko.

Mungu ni mmoja tu, ila nafsi ziko 3, sio miungu wa3 ila NAFSI kwa maana ya MUNGU Baba, Mwana naye Roho mtakatifu!
 
Kwa hivyo, Watu wengine wanaukataa Utatu Mtakatifu kwa sababu kuu zifuatazo:

1. Ni ngumu kuelewa kwa akili ya kibinadamu
Mafundisho ya Mungu mmoja katika nafsi tatu yanaonekana kama yanaenda kinyume na mantiki ya kawaida, hivyo wengine hulikataa kwa kuwa hawalielewi.

2. Hawalionyeshi moja kwa moja katika Biblia neno “Utatu”
Ingawa Biblia hufundisha dhahiri kuhusu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kuwa Mungu, neno “Utatu” halipo kama neno moja. Hii huwafanya baadhi waone ni fundisho la kibinadamu.

3. Uelewa usio sahihi wa maandiko
Wengine huchukua mistari kama “Baba ni mkuu kuniliko” (Yohana 14:28) na kufikiri Yesu si Mungu, pasipo kuelewa kuwa Yesu alisema hayo akiwa katika hali ya unyenyekevu kama mwanadamu.

4. Imani au madhehebu yaliyowafundisha tofauti
Kuna madhehebu kama Mashahidi wa Yehova na wengine wanaoamini kuwa Yesu ni kiumbe aliyeumbwa na si Mungu, hivyo hukataa fundisho la Utatu.

5. Upinzani wa makusudi dhidi ya Ukristo wa jadi
Baadhi ya watu hukataa mafundisho ya msingi ya Ukristo kwa sababu ya misingi ya upinzani wa kiitikadi au kisiasa dhidi ya Kanisa au Ukristo wa kitamaduni.

Lakini ukweli wa Utatu upo katika Biblia:
- Mathayo 28:19 – ...mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
 
Yaani haiwezekani mtu akawa mama na wakati huohuo akawa baba huo ni ujinga wa kujilazimisha
 
Na ukikutana na mtu anayeamini kuwa kwa sababu Kumbukumbu la Torati 6:4 inasema "Bwana Mungu wetu ni mmoja" haina maana ya kuwa hakuna Utatu,

Ni kweli kabisa kuwa Mungu ni mmoja, kama maandiko yanavyosema. Hata sisi tunaoamini Utatu hatuamini miungu watatu, bali Mungu mmoja aliye katika nafsi tatu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Maandiko mengi yanaonyesha jinsi Mungu huyu mmoja alivyojifunua kwa njia tatu tofauti, lakini bado akabaki kuwa Mungu mmoja.

Mfano:
-Yesu alibatizwa – Luka 3:21-22: Yesu (Mwana) yupo, Roho Mtakatifu anashuka kama hua, na sauti ya Baba inasikika. Nafsi zote tatu zinaonekana kwa wakati mmoja.
- Mathayo 28:19 – “...mbatizeni kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu” – sio majina, bali jina Moja likiwa na mamlaka ya nafsi tatu.
Hivyo;
Mungu ni mmoja kwa asili, lakini alijifunua kwa wanadamu katika nafsi tatu kwa ajili ya kazi tofauti: Baba kama Muumba, Mwana kama Mkombozi, na Roho Mtakatifu kama Msaidizi. Hii haipingani na Kumbukumbu 6:4, bali inaithibitisha kwa kina! Ni nayo tu..

Amen🙏🏽
 
Yaani haiwezekani mtu akawa mama na wakati huohuo akawa baba huo ni ujinga wa kujilazimisha
Soma polepole, weka positive mind kwanza! hakuna aliyeandika hii maana unayoiwaza kwa maandishi, ukisoma haraka haraka huwezi kuelewa kabisa nakuhakikishia! Mtabishana hapa karne na karne ila hutookota kitu😊
 
Heri wapatanishi maana hao wataitwa Wana wa Mungu...😎

Kwenye Bible wana wa Mungu n wengi sana..
Hata wewe ukikuta watu wanagombana ukawapatanisha according to bible,,,unaitwa mwana wa Mungu😃
 
enedelea mpaka 40-44.

hapa Yesu anaonyesha dhamira halisi ya kutoitaja siku hiyo,kumbuka atakayetakiwa kuja ni yeye huyo huyo anayejizungumzia kama mfumanizi.

ingekosa maana kabisa kuitaja siku husika,maana watu wangejiandaa wakati wanaikaribia.
HAPO KIDOGO INAKUJA UKAKASI, UKISEMA HIVO UNAMAANISIA YAKUWA ALIONGOPA SI NDIO....?
 
Kwa hivyo, Watu wengine wanaukataa Utatu Mtakatifu kwa sababu kuu zifuatazo:

1. Ni ngumu kuelewa kwa akili ya kibinadamu
Mafundisho ya Mungu mmoja katika nafsi tatu yanaonekana kama yanaenda kinyume na mantiki ya kawaida, hivyo wengine hulikataa kwa kuwa hawalielewi.
WW UMELIELEWA KWA AKILI YA KIUNGU EE...?
 
(Isaiah 9:6-7)

Yesu anaitwa, "BABA" wa milele.

Yesu ndiye MUNGU baba huyo huyo,ndiye MUNGU Roho mtakatifu, ndiye MUNGU Mwana.

Mungu mmoja, nafsi moja.
Muislamu akisikia umemfafanua Yesu jinsi hii unywea na kujikunyata utamsikia anakuambia hiyo injili ya hivyo umeitoa wapi ? Waislam wanapenda ile injili potovu ya Mungu mmoja nafsi 3 maana ndiyo wanaweza kuicharenji ...MAKANISA NA MADHEHEBU YAME HALIBU SANA INJILI HADI UISLAMU UMEPATA UPENYO WA KUDANGANYA WATU, KWA WAKRISTO WASIO NA UFAHAMU NA AKILI KUPOTOSHA KUWA MUNGU NI NAFSI 3...

BAADHI YA MAMBO YALIYO POTOSHWA VIBAYA SANA NDANI YA UKRISTO NI HAYA👉

1)Yesu alipokufa alienda kuzimu na siku ya 3 kufufuka.

2)Yesu ajui siku ya kihama kwa sababu alisema "mwana ajui ila baba) ..hapa wakajenga hoja ya nafsi ya pili ....kumbe ni tofauti, hii kauli ni kinyume na kutokujua siku ya kihama.

3)Yesu alisulibiwa kwa sababu ya dhambi ya asili ....hapa napo kuna upotovu mbaya sana unao wapa Waislam nguvu ya kupotosha, kwa sababu hii dhana inadunisha thamani ya kifo cha yesu... na kuifanya iwe duni sana, kama mtu akijua sababu sahihi ya Yesu kusulibiwa ...ni kweli Yesu alisulibiwa kwa sababu ya dhambi zetu ila siyo dhambi ya asili.

4)Kuna dhambi ya asili 👉 huu ni uongo na kutokuelewa maandiko ...kuna tofauti ya dhambi kuingia ulimwenguni na mtu kupata dhambi ....adamu na hawa awakupata dhambi wala awakuhesabiwa dhambi kwa kosa la kula tunda (hapa inatakiwa kujua dhambi ni nini kwanza ) adamu na hawa walikuwa awajui mema wala mabaya walipo kula tunda ...ila baada ya kula tunda ndiyo walifunguliwa wakajua mema na mabaya na huko kujua mema na mabaya ndiyo kuingia kwa DHAMBI DUNIANI.

5)666 ni papa au freemason au kiumbe fulani kijacho kwenye nyakati fulani za ulimwengu 👉 huu ni upumbavu mwingine wa kutokujua kabisa maandiko na kukosa hekima ya kupambanua mambo kwa akili.

KWA KUIPOTOA INJILI NAMNA HII AIWEZEKANI MTU KUPATA WOKOVU, NDIYO MAANA MIMI NAWAONA WALOKOLE WOTE NI WAPUMBAVU MAANA INJILI WANAYO IFUATA NA KUDAI WOKOVU YENYEWE NI INJILI YA SHETANI KUTOKA KUZIMU
FaizaFoxy Malaria 2 Mufti kuku The Infinity Jagina Bwana Utam selem Covax Joe Milla Seran ngoswe hamis77 DR Mambo Jambo
 
Habari zenu wakuu - Nitatoa ufafanuzi kama kichwa kinavyoeleza, Hizi hoja zote ni matokeo ya uchambuzi wangu wa kina wa biblia:

NInakubaliana na fumbo la utatu wa Mungu - Baba, Mwana na Roho lakini katika mtizamo wa kimajukumu na siyo Mamlaka.

Tuweke theology pembeni kisha tujadili neno lenyewe, Kwanini nasema Utatu ni wa majukumu na siyo mamlaka ? [Kama christians wengi wadaivyo kwamba YHWH, Yesu na RohoMtakatifu wana uwezo sawa kimamlaka], Sababu zangu ni:

1. Mungu ni Mmoja, Nafsi Moja — Sio Nafsi Tatu.
“Sikia, Ee Israeli, BWANA Mungu wetu, BWANA ni mmoja.”
(Kumbukumbu 6:4)
“Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu hapana Mungu.”
(Isaya 45:5)
Mungu ni nafsi moja tu, anasema “Mimi,” si “sisi.” Hakuna viini vitatu vya Mungu.

2. Yesu ni Mungu kwa Sababu ni Mwana wa Mungu — ila si Mkuu Kama Baba.
-"Kwani kijana wa miaka 35 si mtu mzima aliyekomaa sawa tu na baba yake-Je hilo linampa nafasi ya kuwa sawa na baba yake? Bado atabaki mtoto anayepaswa kutii simple.
“Naye Neno alikuwa Mungu... naye akawa mwili...” - Yaani Yesu pia alikua ni Mungu kamili kwasababu alirithi uungu ule kwa baba yake na akaja kupitia mwili.
(Yohana 1:1,14)
“Katika yeye unakaa utimilifu wote wa uungu...” - unakaa utimilifu wa uungu - Si kwamba yeye ndiye Mungu mkuu.
(Wakolosai 2:9)
“Baba peke yake ndiwe Mungu wa kweli...”
(Yohana 17:3)
Yesu ana uungu, lakini anamtambua Baba kuwa Mkuu kuliko yeye.

3. Yesu si Baba — Wanatenda Majukumu Tofauti
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)
“Sishuki kutoka mbinguni kufanya mapenzi yangu, bali ya Yule aliyenituma.”
(Yohana 6:38)
Yesu anatenda kazi ya Baba, si Baba mwenyewe.

4. Roho Mtakatifu si Nafsi ya Mungu, Bali ni Nguvu ya Mungu.
“Roho Mtakatifu atakujilia juu...”
(Luka 1:35)
“Mtapokea nguvu, Roho Mtakatifu atakapowajilia...”
(Matendo 1:8)
“Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” - Hutuombea kwa nani ikiwa watu wanaclaim Roho ni YHWH.
(Warumi 8:26)
Roho ni nguvu ya YHWH, si nafsi huru.

5. Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza — YHWH Hana Chanzo wala hazaliwi.
“Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.”
(Wakolosai 1:15)
“Mimi nalitoka kwa Mungu...”
(Yohana 8:42)
Yesu ni mwanzo wa ufunuo wa Mungu; Baba hana mwanzo.

6. Yesu Anafanya Kazi Maalum — Uumbaji na Ufunuo.
“Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa...”
(Wakolosai 1:16)
“Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana.”
(Wakolosai 1:15) - Amebeba sifa zote za YHWH asiyeonekana.
Yesu ni mtendaji mkuu wa Mungu, si chanzo kikuu.

7. Yesu Alijinyenyekesha — Hakujijaribu Kuwa Mkuu Kuliko Baba.
“Alijinyenyekeza mwenyewe, akawa mtii hata mauti...”
(Wafilipi 2:6-8)
Alijua kuwa ana sifa zote za Uungu lakini alimuachia Baba mamlaka ya mwisho.

8. Yesu Hakupewa Ujuzi wa Mwisho — Baba Pekee Anajua kila kitu.
“Siku ile au saa ile hakuna ajuaye, hata malaika, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
(Marko 13:32) - Hata Mwana mwenyewe haijui siku ya mwisho bali Baba.
Majukumu tofauti - mamlaka tofauti.

9. Roho Mtakatifu ni Nguvu ya YHWH Inayotumika na Baba mwenyewe, Mwana, na Sisi kama tukikiri kwa moyo wa dhati tunashare pia.
“Pokeeni Roho Mtakatifu.”
(Yohana 20:22)
“Nitaimimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili...”
(Matendo 2:17)
“Roho wake akaaye ndani yenu...”
(Warumi 8:11)
Roho hutenda kazi ndani ya Mungu na sisi.

10. Mungu Mmoja, Nafsi Moja, Anayetenda Ndani ya Wote.
“Mungu mmoja, aliye Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote, na ndani ya yote.”
(Waefeso 4:6).
Mungu ni mmoja, na anatenda kazi zote tatu:
I. Baba kama chanzo na mkuu.
II. Kumtuma Mwana kama mtendaji na mfunuo.
III. Kuachilia Roho kama nguvu inayotenda ndani ya sisi na ulimwengu

11. Yesu ni Mungu Kamili — Anatenda kama Mungu, Lakini Hadai Usawa na Baba kwasababu Baba ni Baba.
“Umesamehewa dhambi zako.”
(Luka 5:20)
“Wewe u Mwana wa Mungu.”
(Marko 3:11)
“Mungu alikuwa katika Kristo akiupatanisha ulimwengu...”
(2 Wakorintho 5:19)

Yesu anasamehe, anatoa pepo, anapatanisha — ni kazi za Mungu ila;
“Yeye kwa asili alikuwa Mungu, lakini hakudhani kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho...”
(Wafilipi 2:6) - Alijinyenyekesha, hakutaka kuwa sawa na Mungu mkuu.
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)

✅ Yesu ni Mungu, lakini hachukui nafasi ya Baba.
✅ Alinyenyekea, akatenda kwa mamlaka ya Baba.
✅Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza - Mungu hazaliwi na Hana chanzo, Kama angezaliwa ilitakiwa biblia ijibu alizaliwa toka kwa nani?
✅Mwana wa Mungu = Mungu [Genetically].
Lakini Baba ni mkuu kuliko yeye.
✅Roho ni nguvu ya Mungu, inayoshirikiwa na wote — Baba, Mwana, na sisi.
✅Huu ndio Utatu wa Majukumu — si uungu wa nafsi tatu, bali kazi tatu za Mungu mmoja aliye juu ya yote.

🧠 Tufungue mjadala:
Unakubaliana au unapinga? Tufanye hoja kwa hoja - siyo hisia na mihemko kwa heshima ya maandiko ili tupate kuujua ukweli.
📖 Biblia iwe mbele, Theology nyuma.
Habari zenu wakuu - Nitatoa ufafanuzi kama kichwa kinavyoeleza, Hizi hoja zote ni matokeo ya uchambuzi wangu wa kina wa biblia:

NInakubaliana na fumbo la utatu wa Mungu - Baba, Mwana na Roho lakini katika mtizamo wa kimajukumu na siyo Mamlaka.

Tuweke theology pembeni kisha tujadili neno lenyewe, Kwanini nasema Utatu ni wa majukumu na siyo mamlaka ? [Kama christians wengi wadaivyo kwamba YHWH, Yesu na RohoMtakatifu wana uwezo sawa kimamlaka], Sababu zangu ni:

1. Mungu ni Mmoja, Nafsi Moja — Sio Nafsi Tatu.
“Sikia, Ee Israeli, BWANA Mungu wetu, BWANA ni mmoja.”
(Kumbukumbu 6:4)
“Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu hapana Mungu.”
(Isaya 45:5)
Mungu ni nafsi moja tu, anasema “Mimi,” si “sisi.” Hakuna viini vitatu vya Mungu.

2. Yesu ni Mungu kwa Sababu ni Mwana wa Mungu — ila si Mkuu Kama Baba.
-"Kwani kijana wa miaka 35 si mtu mzima aliyekomaa sawa tu na baba yake-Je hilo linampa nafasi ya kuwa sawa na baba yake? Bado atabaki mtoto anayepaswa kutii simple.
“Naye Neno alikuwa Mungu... naye akawa mwili...” - Yaani Yesu pia alikua ni Mungu kamili kwasababu alirithi uungu ule kwa baba yake na akaja kupitia mwili.
(Yohana 1:1,14)
“Katika yeye unakaa utimilifu wote wa uungu...” - unakaa utimilifu wa uungu - Si kwamba yeye ndiye Mungu mkuu.
(Wakolosai 2:9)
“Baba peke yake ndiwe Mungu wa kweli...”
(Yohana 17:3)
Yesu ana uungu, lakini anamtambua Baba kuwa Mkuu kuliko yeye.

3. Yesu si Baba — Wanatenda Majukumu Tofauti
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)
“Sishuki kutoka mbinguni kufanya mapenzi yangu, bali ya Yule aliyenituma.”
(Yohana 6:38)
Yesu anatenda kazi ya Baba, si Baba mwenyewe.

4. Roho Mtakatifu si Nafsi ya Mungu, Bali ni Nguvu ya Mungu.
“Roho Mtakatifu atakujilia juu...”
(Luka 1:35)
“Mtapokea nguvu, Roho Mtakatifu atakapowajilia...”
(Matendo 1:8)
“Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” - Hutuombea kwa nani ikiwa watu wanaclaim Roho ni YHWH.
(Warumi 8:26)
Roho ni nguvu ya YHWH, si nafsi huru.

5. Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza — YHWH Hana Chanzo wala hazaliwi.
“Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.”
(Wakolosai 1:15)
“Mimi nalitoka kwa Mungu...”
(Yohana 8:42)
Yesu ni mwanzo wa ufunuo wa Mungu; Baba hana mwanzo.

6. Yesu Anafanya Kazi Maalum — Uumbaji na Ufunuo.
“Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa...”
(Wakolosai 1:16)
“Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana.”
(Wakolosai 1:15) - Amebeba sifa zote za YHWH asiyeonekana.
Yesu ni mtendaji mkuu wa Mungu, si chanzo kikuu.

7. Yesu Alijinyenyekesha — Hakujijaribu Kuwa Mkuu Kuliko Baba.
“Alijinyenyekeza mwenyewe, akawa mtii hata mauti...”
(Wafilipi 2:6-8)
Alijua kuwa ana sifa zote za Uungu lakini alimuachia Baba mamlaka ya mwisho.

8. Yesu Hakupewa Ujuzi wa Mwisho — Baba Pekee Anajua kila kitu.
“Siku ile au saa ile hakuna ajuaye, hata malaika, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
(Marko 13:32) - Hata Mwana mwenyewe haijui siku ya mwisho bali Baba.
Majukumu tofauti - mamlaka tofauti.

9. Roho Mtakatifu ni Nguvu ya YHWH Inayotumika na Baba mwenyewe, Mwana, na Sisi kama tukikiri kwa moyo wa dhati tunashare pia.
“Pokeeni Roho Mtakatifu.”
(Yohana 20:22)
“Nitaimimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili...”
(Matendo 2:17)
“Roho wake akaaye ndani yenu...”
(Warumi 8:11)
Roho hutenda kazi ndani ya Mungu na sisi.

10. Mungu Mmoja, Nafsi Moja, Anayetenda Ndani ya Wote.
“Mungu mmoja, aliye Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote, na ndani ya yote.”
(Waefeso 4:6).
Mungu ni mmoja, na anatenda kazi zote tatu:
I. Baba kama chanzo na mkuu.
II. Kumtuma Mwana kama mtendaji na mfunuo.
III. Kuachilia Roho kama nguvu inayotenda ndani ya sisi na ulimwengu

11. Yesu ni Mungu Kamili — Anatenda kama Mungu, Lakini Hadai Usawa na Baba kwasababu Baba ni Baba.
“Umesamehewa dhambi zako.”
(Luka 5:20)
“Wewe u Mwana wa Mungu.”
(Marko 3:11)
“Mungu alikuwa katika Kristo akiupatanisha ulimwengu...”
(2 Wakorintho 5:19)

Yesu anasamehe, anatoa pepo, anapatanisha — ni kazi za Mungu ila;
“Yeye kwa asili alikuwa Mungu, lakini hakudhani kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho...”
(Wafilipi 2:6) - Alijinyenyekesha, hakutaka kuwa sawa na Mungu mkuu.
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)

✅ Yesu ni Mungu, lakini hachukui nafasi ya Baba.
✅ Alinyenyekea, akatenda kwa mamlaka ya Baba.
✅Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza - Mungu hazaliwi na Hana chanzo, Kama angezaliwa ilitakiwa biblia ijibu alizaliwa toka kwa nani?
✅Mwana wa Mungu = Mungu [Genetically].
Lakini Baba ni mkuu kuliko yeye.
✅Roho ni nguvu ya Mungu, inayoshirikiwa na wote — Baba, Mwana, na sisi.
✅Huu ndio Utatu wa Majukumu — si uungu wa nafsi tatu, bali kazi tatu za Mungu mmoja aliye juu ya yote.

🧠 Tufungue mjadala:
Unakubaliana au unapinga? Tufanye hoja kwa hoja - siyo hisia na mihemko kwa heshima ya maandiko ili tupate kuujua ukweli.
📖 Biblia iwe mbele, Theology nyuma.

ole wa walimu. Umeandika mengi ila blunders ni nyingi. una hatari sana ndugu.

“Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi."

— Yakobo 3:1 (Biblia Takatifu)
 
HAPO KIDOGO INAKUJA UKAKASI, UKISEMA HIVO UNAMAANISIA YAKUWA ALIONGOPA SI NDIO....?
Mwana ni mwili wake.... Baba ni Nafsi yake, sasa kaongopa vipi lile lilikuwa fumbo wanafunzi awakumwelewa wakaacha kumsumbua .....wakristo mnatakiwa kujua neno YESU ni mambo MAWILI
1)mwili = (mwana) (mwana wa adamu)
2)nafsi = (baba) (Mungu)
Ukijua hivi utajua Yesu alipo sema mwana ajui ila baba maana yake ni nini ? Pia utajua kwanini Yesu anasema baba ni mkuu kuliko mwana ...pia utajua kilicho kufa msalabani ni mwana siyo baba ...pia utajua kwa nini Yesu anamwambia yuke mtu msalabani kuwa 👉 leo hii utakuwa pamoja nami pema peponi ...je yesu aliye kufa na kufufuka siku ya 3 ni yupi na huyu anaye sema siku ileile atakuwa peponi ni yupi ? Hapo tuna waona Yesu wawili mmoja kafa yupo kaburini na mwingine akufa yupo peponi siku ile ile .....fafanuzi pale juu tukiitumia tunapata jibu ....mwili wa yesu ndiyo uliokufa na kwenda kaburini ila nafsi ya yesu ndiyo baba aiwezi kufa hiyo ilikuwa hai na peponi siku ile ile.
FaizaFoxy Malaria 2 Mufti kuku The Infinity Jagina Bwana Utam selem Covax Joe Milla Seran ngoswe DR Mambo Jambo hamis77
 
Back
Top Bottom