Uungu haurithiwi! Yesu Kristo alikuwa ni Mungu kwa asili!
Mfano kwa asili Mtoto wa MTU ni MTU! Mtoto wa SIMBA ni SIMBA,nk
Umeeleza vizuri tu kuwa Yesu Kristo ni Mungu lakini siyo Mungu Mkuu!
Kwa hiyo kwa habari ya Uungu,Yesu Kristo ni Mungu kama Baba alivyo!,(na hiki ndicho Wayahudi walichotaka kumpigia mawe,aliposema Yeye ni Mwana wa Mungu,walimwona ni mtu kama wao kwa nini ajilinganishe na Mungu?)
Yohana5:16-18
Yohana10:30-36
Ila kwa habari ya Ukuu,Mungu Baba ni Mkuu kuliko Mwana.
Kwa hiyo Baba na Mwana ni Nafsi mbili za Mungu.
Baba ni Nafsi na Mwana ni Nafsi ya Mungu kwa sababu ametokana na Mungu.
Ukiweka na Roho Mtakatifu aliyetoka kwa Baba,ni Nafsi nyingine ya Mungu,(Yohana14:16-18)
Kwa Baba,Neno na Roho Mtakatifu ni Nafsi tatu za Mungu Mmoja.
Anza kujifunzia:
Adamu na Hawa walikuwa Wawili lakini MWILI MMOJA,au Mtu Mmoja aitwaye Adamu,(Mwanzo2:21-24;5:1-3)
Katika ulimwengu wa roho Mme na Mke ni Nafsi mbili lakini ni Mmoja-Mme kichwa na Mke Mwili)!