Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

The Chosen Liberator

Senior Member
Joined
Jun 21, 2025
Posts
123
Reaction score
66
Habari zenu wakuu - Nitatoa ufafanuzi kama kichwa kinavyoeleza, Hizi hoja zote ni matokeo ya uchambuzi wangu wa kina wa biblia:

NInakubaliana na fumbo la utatu wa Mungu - Baba, Mwana na Roho lakini katika mtizamo wa kimajukumu na siyo Mamlaka.

Tuweke theology pembeni kisha tujadili neno lenyewe, Kwanini nasema Utatu ni wa majukumu na siyo mamlaka ? [Kama christians wengi wadaivyo kwamba YHWH, Yesu na RohoMtakatifu wana uwezo sawa kimamlaka], Sababu zangu ni:


1. Mungu ni Mmoja, Nafsi Moja — Sio Nafsi Tatu.
“Sikia, Ee Israeli, BWANA Mungu wetu, BWANA ni mmoja.”
(Kumbukumbu 6:4)
“Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu hapana Mungu.”
(Isaya 45:5)
Mungu ni nafsi moja tu, anasema “Mimi,” si “sisi.” Hakuna viini vitatu vya Mungu.


2. Yesu ni Mungu kwa Sababu ni Mwana wa Mungu — ila si Mkuu Kama Baba.
-"Kwani kijana wa miaka 35 si mtu mzima aliyekomaa sawa tu na baba yake-Je hilo linampa nafasi ya kuwa sawa na baba yake? Bado atabaki mtoto anayepaswa kutii simple.
“Naye Neno alikuwa Mungu... naye akawa mwili...” - Yaani Yesu pia alikua ni Mungu kamili kwasababu alirithi uungu ule kwa baba yake na akaja kupitia mwili.
(Yohana 1:1,14)
“Katika yeye unakaa utimilifu wote wa uungu...” - unakaa utimilifu wa uungu - Si kwamba yeye ndiye Mungu mkuu.
(Wakolosai 2:9)
“Baba peke yake ndiwe Mungu wa kweli...”
(Yohana 17:3)
Yesu ana uungu, lakini anamtambua Baba kuwa Mkuu kuliko yeye.


3. Yesu si Baba — Wanatenda Majukumu Tofauti
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)
“Sishuki kutoka mbinguni kufanya mapenzi yangu, bali ya Yule aliyenituma.”
(Yohana 6:38)
Yesu anatenda kazi ya Baba, si Baba mwenyewe.


4. Roho Mtakatifu si Nafsi ya Mungu, Bali ni Nguvu ya Mungu.
“Roho Mtakatifu atakujilia juu...”
(Luka 1:35)
“Mtapokea nguvu, Roho Mtakatifu atakapowajilia...”
(Matendo 1:8)
“Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” - Hutuombea kwa nani ikiwa watu wanaclaim Roho ni YHWH.
(Warumi 8:26)
Roho ni nguvu ya YHWH, si nafsi huru.



5. Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza — YHWH Hana Chanzo wala hazaliwi.
“Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.”
(Wakolosai 1:15)
“Mimi nalitoka kwa Mungu...”
(Yohana 8:42)
Yesu ni mwanzo wa ufunuo wa Mungu; Baba hana mwanzo.


6. Yesu Anafanya Kazi Maalum — Uumbaji na Ufunuo.
“Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa...”
(Wakolosai 1:16)
“Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana.”
(Wakolosai 1:15) - Amebeba sifa zote za YHWH asiyeonekana.
Yesu ni mtendaji mkuu wa Mungu, si chanzo kikuu.


7. Yesu Alijinyenyekesha — Hakujijaribu Kuwa Mkuu Kuliko Baba.
“Alijinyenyekeza mwenyewe, akawa mtii hata mauti...”
(Wafilipi 2:6-8)
Alijua kuwa ana sifa zote za Uungu lakini alimuachia Baba mamlaka ya mwisho.



8. Yesu Hakupewa Ujuzi wa Mwisho — Baba Pekee Anajua kila kitu.
“Siku ile au saa ile hakuna ajuaye, hata malaika, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
(Marko 13:32) - Hata Mwana mwenyewe haijui siku ya mwisho bali Baba.
Majukumu tofauti - mamlaka tofauti.


9. Roho Mtakatifu ni Nguvu ya YHWH Inayotumika na Baba mwenyewe, Mwana, na Sisi kama tukikiri kwa moyo wa dhati tunashare pia.
“Pokeeni Roho Mtakatifu.”
(Yohana 20:22)
“Nitaimimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili...”
(Matendo 2:17)
“Roho wake akaaye ndani yenu...”
(Warumi 8:11)
Roho hutenda kazi ndani ya Mungu na sisi.



10. Mungu Mmoja, Nafsi Moja, Anayetenda Ndani ya Wote.
“Mungu mmoja, aliye Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote, na ndani ya yote.”
(Waefeso 4:6).
Mungu ni mmoja, na anatenda kazi zote tatu:
I. Baba kama chanzo na mkuu.
II. Kumtuma Mwana kama mtendaji na mfunuo.
III. Kuachilia Roho kama nguvu inayotenda ndani ya sisi na ulimwengu


11. Yesu ni Mungu Kamili — Anatenda kama Mungu, Lakini Hadai Usawa na Baba kwasababu Baba ni Baba.
“Umesamehewa dhambi zako.”
(Luka 5:20)
“Wewe u Mwana wa Mungu.”
(Marko 3:11)
“Mungu alikuwa katika Kristo akiupatanisha ulimwengu...”
(2 Wakorintho 5:19)

Yesu anasamehe, anatoa pepo, anapatanisha — ni kazi za Mungu ila;
“Yeye kwa asili alikuwa Mungu, lakini hakudhani kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho...”
(Wafilipi 2:6) - Alijinyenyekesha, hakutaka kuwa sawa na Mungu mkuu.
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)


✅ Yesu ni Mungu, lakini hachukui nafasi ya Baba.
✅ Alinyenyekea, akatenda kwa mamlaka ya Baba.
✅Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza - Mungu hazaliwi na Hana chanzo, Kama angezaliwa ilitakiwa biblia ijibu alizaliwa toka kwa nani?
✅Mwana wa Mungu = Mungu [Genetically].
Lakini Baba ni mkuu kuliko yeye.
✅Roho ni nguvu ya Mungu, inayoshirikiwa na wote — Baba, Mwana, na sisi.
✅Huu ndio Utatu wa Majukumu — si uungu wa nafsi tatu, bali kazi tatu za Mungu mmoja aliye juu ya yote.


🧠 Tufungue mjadala:
Unakubaliana au unapinga? Tufanye hoja kwa hoja - siyo hisia na mihemko kwa heshima ya maandiko ili tupate kuujua ukweli.
📖 Biblia iwe mbele, Theology nyuma.
 
Ngoja wasaudia wa kibongo waje,
Watakwambia huyo ni Issa bin Mariam,mtoto wa Yussuf the carpenter.
Hana umungu wowote🤣🤣
 
Mkuu kwa maelezo yako - Mungu wako wawili?

Kama huyo mmoja wenzako hawawezi kumthibitisha - hao wawili je utaweza?

Haya prove uwepo wao lakini uanze na kutoa maana ya Mungu kwanza.
Mungu ni muumba au chanzo cha kila kitu, Mungu ni mmoja, Mweza wa yote aliye ndani ya yote na katika yote.

Mungu yupo - lakini kukulazimisha kujua kama ninavyojua wakati haumini chochote ni kazi bure - Nitakua ninaingilia uhuru wako wa kufikiri. Zaidi ninakuombea Neema ya Mungu ikuangazie 🙏🏿
 
Kauli zako tu zinaonyesha kuna miungu watatu.

Kama Munhu ni mmoja tuu.
Hana mshirika hana ushirika hajagawanyika.
Majukumu yake anayafanya mwenyewe.
Huyo huyo akiwa baba huyo huyo akiwa mwana na huyo huyo kama roho.

Yesu ndie yehova wa agano la kale.
Roho mtakatifu ndie roho wa Mungu.
Ni Mungu mwenyewe
 
Tito 2:13
[13]tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;


Yesu ndie mungu mkuu hakuna mwingine
 
Mungu ni muumba au chanzo cha kila kitu, Mungu ni mmoja, Mweza wa yote aliye ndani ya yote na katika yote.

Mungu yupo - lakini kukulazimisha kujua kama ninavyojua wakati haumini chochote ni kazi bure - Nitakua ninaingilia uhuru wako wa kufikiri. Zaidi ninakuombea Neema ya Mungu ikuangazie 🙏🏿
Hapa ulikua unamjibu nani? Maana sicho nilichohitaji kufafanuliwa.
 
Unatumia nguvu mno....sio tu mimi sielewi inaonekana hata wewe pia HUELEWI...na sio wewe tu hata kadinali mkuu pale vatikani HAELEWI...😅

eniwei wewe UMEMJUAJE MUNGU ama UNAMJUAJE MUNGU?
 
Biblia inamuita Yesu ni Mungu mkuu
Ukisema sio Mungu mkuu unatuchanganya.

Baba
ROHO
Yesu
Kila kimoja hapo juu kinasi SIFA ya uungu sawa na chenzake.
 
Isaya 9:6
[6]Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele, Mfalme wa amani.


Mnataka mjue nini zaidi huyo mtoto ndie baba
Emmanuel ni yule Mungu mkuu pamoja nasi
 
Yohana 1:1
[1]Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Yesu ni mwili wa munguuu ambao ndio aliuvaa akaumba ulimwengu.

Yohana 1:3
[3]Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
 
Tito 2:13
[13]tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;


Yesu ndie mungu mkuu hakuna mwingine
Sawa naomba pia ufafanuzi wako kupitia kifungu hiki;

"Lakini kuhusu siku hiyo au saa hiyo hakuna ajuaye, wala malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake." — Marko 13:32
 
Mnataka baba gani zaidi.

Yohana 14:7-9
[7]Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.

[8]Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.

[9]Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
 
Yohana 1:1
[1]Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Yesu ni mwili wa munguuu ambao ndio aliuvaa akaumba ulimwengu.

Yohana 1:3
[3]Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Alikua Mungu ndiyo "Mungu kwa maana baba yake ni Mungu hivyo yeye hawezi kuwa binadamu" lakini sio Mungu mkuu kama baba yake.

Thats why akasema Uzima wa ukweli ndiyo huu wakujue Mungu wa pekee wa kweli na Yesu kristo aliyemtuma.

Kwa kifungu hiki Mungu wa pekee wa kweli ni nani? na Yesu aliyetumwa ni nani?
 
M
Sawa naomba pia ufafanuzi wako kupitia kifungu hiki;

"Lakini kuhusu siku hiyo au saa hiyo hakuna ajuaye, wala malaika wa mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake." — Marko 13:32
Mwana ni mwili aliouvaa Mungu akiwa duniani.
Uliozaliwq na mwanamke.
Na ndio maana biblia inasema mungu ana wana wengi.

Na ndio maana alipokata roho mwili ukalia baba baba mbona umeniachaaa.
Kwa sababu mungu asingeonja laana ya kifo ila mwili aliouvaa wa sadaka.

Ule mwili ulishamaliza kazi
Mungu akarudi kwenye hali yake ya roho
 
Back
Top Bottom