The Chosen Liberator
Senior Member
- Jun 21, 2025
- 123
- 66
- Thread starter
- #21
Yaah ukimuona yeye ni sawa na umemuona Mungu kwa maana ya Nguvu na Matendo.Mnataka baba gani zaidi.
Yohana 14:7-9
[7]Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
Kwani kiuhalisia hakuna binadamu anaweza akamuona Mungu wa pekee wa kweli "YHWH"
1 Timotheo 6:16
"Yeye peke yake asiyeweza kufa, akaaye katika nuru isiyoweza kukaribiwa; ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona."
Yesu alikufa lakini pia Yesu alionwa na binadamu - Kumbuka Mungu wa pekee wa kweli hafi.
Ukimuona Yesu umemuona Mungu sababu amebeba sifa zote za uungu na anaweza kusamehe dhambi.[8]Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
[9]Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
Yesu ni mwakilishi.