Utatuzi wa Changamoto Kupata PF3 wakati wa ajali

Utatuzi wa Changamoto Kupata PF3 wakati wa ajali

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2020
Posts
3,443
Reaction score
4,006
Wana jamvi,

Ni miongo kadhaa sasa kwa mjibu wa sheria kila anayepata ajali ili apokelewe na kutibiwa na hospitali/zahanati au vituo vya afya ni sharti mgonjwa awe na Fomu iliyotolewa na kituo cha polisi alikoenda au kupelekwa kabla.

Utaratibu huu umesababisha madhara makubwa ikiwemo vifo kutokana na kuchelewa kufika hospitalini au kukataliwa hospitalini kutokana na hofu ya kutibu mtu aliyehusika na matendo ya jinai kama ujambazi nk. Huu utaratibu unavunja haki za msingi za binadamu kuwa na haki ya kuishi.

Kwa maoni yangu, napendekeza kwa serikali kutengeneza utaratibu wa kwamba pindi polisi wakipata taarifa za ajali barabarani, nyumbani, ofisini au popote ambapo kuna majeruhi au vyovyote, basi jeshi la polisi liwape wanaohusika na masuala ya ajali kwenda na PF3 kwenye eneo la tukio ambako baada ya kufika afanye tathiminni haraka na kutoa hiyo hati ya matibabu ya kipolisi kuwahi kuokoa maisha kuliko ilivyo kwa sasa.

Mchango wenu wadau tafadhali
 
Hoja ya kutotibu mtu kwa sababu ni jambazi au ameumia katika tukio la jinai au uhalifu ni UDHAIFU MKUBWA SANA WA KIFIKRA, hakuna sheria yoyote inayosema Jambazi akiumia aachwe afe.

Ali anatakiwa kutibiwa ili akipona afikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma.
 
Paragraph yako ya mwisho haieleweki vyema. Iweke vizuri kwanza.

Hata hivyo sio mara moja au 2 kumekuwa na kelele kuhusu huo mtindo wa polisi kutoa pf3, na ikatokea mapendekezo kuwa kuwe na dawati la polisi kwenye hospitali au vituo vya afya kwa ajili ya kutoa pf3. Hoja hiyo iliingia hadi bungeni, kwa bahati mbaya ilipelekwa na upinzani, hivyo haikupata msukumo maana huko bungeni hoja haipiti kwa ubora, bali kwa ushabiki wa kisiasa, na ilionekana ikipita itakuwa sifa za upinzani. Na polisi kama polisi bado wako kwenye muundo wa kikoloni, wao hawatungi sheria, bali husubiri sheria zitungwe na wanasiasa waliopo madarakani, na wao kufuata tu kama robots.

Mapendekezo, nashauri majeruhi yoyote akifika hospitalini aendelee na matibabu, kisha kuwe na mawasiliano maalum kati ya hospitali ama vituo vya afya na vituo vya polisi vilivyo karibu, kuwa akifika mtu anayepaswa kupata matibabu, aendelee na matibabu ila polisi wataarifiwe wafike hospitali kutoa pf3 muda huo huo, au ndani ya masaa 15. Na kama mtindo huu utakuwa mgumu kiutekelezaji, basi kuwe na form maalum ijazwe na kupigwa muhuri wa hospitali kwa ajili ya kwenda kituo cha polisi kupata pf3, na hii iwe ndani ya masaa 15 pia.

Na kama kuna uwezekano kwa kila hospitali kuwe na dawati la polisi la kutoa pf3. Na kwenye dawati hilo awepo polisi kama wanavyokuwa kwenye nyumba za viongozi ama mabenk nk. Ama itolewe elimu maalum kwa madkatari iwapo polisi hayupo basi wao watoe pf3 kwa muongozo wa polisi kama ilivyo polisi jamii,lakini ndani ya 15hrs kama polisi kama hawapo, taarifa hiyo iwe imefika polisi, hata kwa njia ya e-mail, WhatsApp, sms nk.
 
Back
Top Bottom