Utawajengea wakwe zako nyumba?

Utawajengea wakwe zako nyumba?

Kama wanakaa nyumba duni na wewe unauwezo kwa nini usiwajengee?
Kama unaweza kuwasaidia watu ambao hata huna uhusiano nao kwa nini iwe tatizo kuwasaidia wakwe zako?
Wewe wajengee tena Nyumba nzuri tu kulingana na uwezo wako
☑️🙏🙏🙏
 
Kwa wengine ni kama mwiko kuwajengea wakwe nyumba.

Lakini mimi sioni kama kuna ubaya wo wote ule kufanya hivyo, hasa kama hali ya kifedha inaruhusu. Kutaonekana na kasoro tu ikiwa utawajengea wakwe huku wazazi wako wa kukuzaa hujawatendea hilo.

Kimsingi, wakwe zako ni wazazi wako, na wa kwako ni wa mkeo vile vile!

Kama wewe na mkeo ni mwili mmoja, inamaanisha hata na wazazi wenu ni wenu sote.

Wewe una mtazamo gani? Utawajengea wakwe zako nyumba?
Fresh TU kama binti yao tumemkuta bikira
 
Fresh TU kama binti yao tumemkuta bikira
Vigezo na masharti kuzingatiwa, lazima Binti awe bikra. Sio wahuni wamemgalagaza vya kutosha halafu unakuja wewe unajifanya una mahaba mengi unajenga ukweni
 
Hilo Suala Linaambatana Na Uwezo Kubwa Kuliko Yote Hakuna Ubaya Wowote
Jenga Faster Faster
 
Nitajenga kwenye uwanja wangu nawahamishia hapo, siku yakiisha nao wameisha kila mtu akale alikopeleka mboga. Maisha yenyewe sasa hivi tunaishi kimachale machale tu hakuna kufumba macho yote.

[emoji23][emoji23]
 
Na nilishagasema nyumba nitakayokwenda kutoa posa halafu wakwe waniletee ngendembwe za kutaka mahari yao kias walichokitaja kiwe fixed isipungue hata mia, nikiwa nimemuelewa vizuri binti yao hiyo mahari nitalipa na hapo ndo nitakuwa nimemalizana na ukweni.
 
Sio jambo baya!
Lakini Mimi nani nijengee mkwe nyumba wakati shemeji zangu wapo wanajenga heshima bar?
 
Kwa wengine ni kama mwiko kuwajengea wakwe nyumba.

Lakini mimi sioni kama kuna ubaya wo wote ule kufanya hivyo, hasa kama hali ya kifedha inaruhusu. Kutaonekana na kasoro tu ikiwa utawajengea wakwe huku wazazi wako wa kukuzaa hujawatendea hilo.

Kimsingi, wakwe zako ni wazazi wako, na wa kwako ni wa mkeo vile vile!

Kama wewe na mkeo ni mwili mmoja, inamaanisha hata na wazazi wenu ni wenu sote.

Wewe una mtazamo gani? Utawajengea wakwe zako nyumba?
Wanadai mahali kwa fujo siwajengei
 
Back
Top Bottom