SoC03 Utawala Bora ahueni kwa jamii
Stories of Change - 2023 Competition
Joined
May 31, 2023
Posts
5
Reaction score
6
Utawala Bora ni namna ya kutumia madaraka ya umma katika kutawala rasilimali kwa njia zilizo sahihi ili kukuza uchumi wa nchi.utawala Bora hujumuisha ukweli uwazi uwajibikaji na ushirikishwaji katika utoaji wa maamuzi.

Ili nchi au taifa lolote liweze kupata maendeleo utawala Bora unahitajika. Utawala Bora unajengwa na viongozi Makini wanaothamini raia wao na wasiokuwa na uchu wa madaraka (tamaa ya uongozi). Hii ni kwa sababu Mara nyingi viongozi wenye uchu wa madaraka huangalia maslahi yao bila kujali changamoto zinazolikabili taifa na raia kwa ujumla. Viongozi Hawa huhujumu uchumi kwa kutumia fedha za serikali kinyume na Sheria kwa maslahi yao binafsi , fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo Kama vile ujenzi wa madarasa, hospitali, barabara n.k.

Baadhi ya viongozi wanapopewa fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo sio waaminifu badala yake hutumia kiasi katika fedha hiyo kufanya shughuli bila ufanisi ili waweze kupata chochote kitu katika fedha hiyo Jambo ambalo linazorotesha maendeleo ya nchi na raia kwa ujumla. Kwa mfano Kama ujenzi wa daraja au barabara imara unahitaji kiasi cha shilingi milioni Mia moja ( 100,000,000 Tsh), ili iweze kukamilika na kuonekana ya viwango vya juu kabisa, viongozi wenye tamaa huigawa fedha hii na kununua vifaa vya ujenzi visivyo na kiwango stahiki ilimradi tu wapate kiasi katika fedha hiyo kwa ajili ya shughuli zao, Jambo ambalo hupelekea ujenzi usio imara ambao hautachukua muda mrefu kwa barabara au daraja iliyotengenezwa kuharibika, na kugharimu kiasi kingine cha fedha ambacho kingeweza kutumika kwa ajili ya shughuli zingine za kimaendeleo kutumika Tena kwa ajili ya matengenezo. Hali hii huzorotesha kabisa maendeleo ya nchi na jamii kwa ujumla.

Utawala Bora huwapa raia nafasi ya kueleza changamoto zao. Hii hufanyika kwa njia ya mikutano ya hadhara ambapo viongozi hukutana na wananchi na kujadili pamoja nao changamoto zinazowakabili na kusikiliza mapendekezo yao kwamba Nini kifanyike ili kutatua changamoto hizo. Hii husaidia kuimarisha mahusiano Kati ya wananchi na viongozi wao pia hukuza ushirikiano katika kusimamia rasilimali na kutekeleza maendeleo ya nchi.

Vilevile kiongozi Bora husimamia usawa katika taifa lake. Katika serikali yoyote yenye utawala Bora raia wote ni sawa kwamba hakuna mtu yeyote awe kiongozi au raia wa kawaida aliye juu ya Sheria. Mtu yeyote atakayefanya makosa ataadhibiwa kulingana na Sheria bila kujali dini, jinsia, rangi, Wala kabila. Hii husaidia kukuza ushirikiano baina ya wananchi na viongozi wao katika kusimamia haki za binadamu na katika kutekeleza shughuli za kiuchumi zitakazochangia katika maendeleo ya taifa.

Kiongozi Bora hupinga suala la rushwa katika taifa na jamii yake. Hii ni kwa sababu rushwa imekuwa tatizo kubwa Sana katika jamii ya Sasa ambapo imekuwa kipaumbele katika masuala mbalimbali. Kwa mfano katika suala Zima la ajira, inampasa mtu kutoa rushwa ili aweze kupata ajira, Jambo ambalo linawaumiza watu wasio na uwezo kifedha na wale wasioweza kutoa rushwa ili kupata ajira. Pia katika suala la elimu, hasa elimu ya vyuo vikuu ambapo matokeo ya wanafunzi yapo mikononi mwa wakufunzi wao, baadhi ya wanafunzi hulazimishwa kutoa rushwa ya ngono ili waweze kupewa matokeo mazuri, vinginevyo wapewe matokeo mabaya yatakayopelekea kushindwa katika taaluma zao na hata chuo kwa ujumla.

Vilevile katika vituo vya afya rushwa imeshika Kasi kwa kiwango kikubwa ambapo wenye uwezo kifedha hupatiwa huduma Bora na ya haraka kwa sababu ya pesa zao huku wale wasio na uwezo kupata huduma zisizo bora kwa kucheleweshewa huduma na hata kukosa huduma kabisa. Katika mahakama pia haki inanunuliwa kwa pesa kwamba mwenye pesa ndiye mwenye haki hata Kama ndiye mwenye makosa. Hivyo serikali inahitaji viongozi watakaoweza kutokomeza kabisa suala Hilo la rushwa Ili wananchi wasio na uwezo waweze kusaidika.

Aidha viongozi wanapaswa kusimamia matumizi ya mapato ya nchi kwa kupanga bajeti yenye tija kwa taifa na jamii kwa ujumla. Hii itasaidia kuongeza uaminifu baina ya viongozi na wananchi pia kuwasaidia wananchi kulipa Kodi kwa moyo na kufanya kazi kwa bidii huku wakitegemea maendeleo makubwa kutokana na ya kazi ya mikono yao.

Hivyo Basi ili nchi au jamii yoyote iweze kuendelea inahitaji utawala Bora unaojengwa na viongozi waaminifu,wawajibikaji Wawazi na wakweli.
 
Upvote 2
Utawala Bora ni namna ya kutumia madaraka ya umma katika kutawala rasilimali kwa njia zilizo sahihi ili kukuza uchumi wa nchi.utawala Bora hujumuisha ukweli uwazi uwajibikaji na ushirikishwaji katika utoaji wa maamuzi.

Ili nchi au taifa lolote liweze kupata maendeleo utawala Bora unahitajika. Utawala Bora unajengwa na viongozi Makini wanaothamini raia wao na wasiokuwa na uchu wa madaraka (tamaa ya uongozi). Hii ni kwa sababu Mara nyingi viongozi wenye uchu wa madaraka huangalia maslahi yao bila kujali changamoto zinazolikabili taifa na raia kwa ujumla. Viongozi Hawa huhujumu uchumi kwa kutumia fedha za serikali kinyume na Sheria kwa maslahi yao binafsi , fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo Kama vile ujenzi wa madarasa, hospitali, barabara n.k.

Baadhi ya viongozi wanapopewa fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo sio waaminifu badala yake hutumia kiasi katika fedha hiyo kufanya shughuli bila ufanisi ili waweze kupata chochote kitu katika fedha hiyo Jambo ambalo linazorotesha maendeleo ya nchi na raia kwa ujumla. Kwa mfano Kama ujenzi wa daraja au barabara imara unahitaji kiasi Cha shilingi milioni Mia moja (100,000,000 Tsh), ili iweze kukamilika na kuonekana ya viwango vya juu kabisa, viongozi wenye tamaa huigawa fedha hii na kununua vifaa vya ujenzi visivyo na kiwango stahiki ilimradi tu wapate kiasi katika fedha hiyo kwa ajili ya shughuli zao, Jambo ambalo hupelekea ujenzi usio imara ambao hautachukua muda mrefu kwa barabara au daraja iliyotengenezwa kuharibika, na kugharimu kiasi kingine Cha fedha ambacho kingeweza kutumika kwa ajili ya shughuli zingine za kimaendeleo kutumika Tena kwa ajili ya matengenezo. Hali hii huzorotesha kabisa maendeleo ya nchi na jamii kwa ujumla.

Utawala Bora huwapa raia nafasi ya kueleza changamoto zao. Hii hufanyika kwa njia ya mikutano ya hadhara ambapo viongozi hukutana na wananchi na kujadili pamoja nao changamoto zinazowakabili na kusikiliza mapendekezo yao kwamba Nini kifanyike ili kutatua changamoto hizo. Hii husaidia kuimarisha mahusiano Kati ya wananchi na viongozi wao pia hukuza ushirikiano katika kusimamia rasilimali na kutekeleza maendeleo ya nchi.

Vilevile kiongozi Bora husimamia usawa katika taifa lake. Katika serikali yoyote yenye utawala Bora raia wote ni sawa kwamba hakuna mtu yeyote awe kiongozi au raia wa kawaida aliye juu ya Sheria. Mtu yeyote atakayefanya makosa ataadhibiwa kulingana na Sheria bila kujali dini, jinsia, rangi, Wala kabila. Hii husaidia kukuza ushirikiano baina ya wananchi na viongozi wao katika kusimamia haki za binadamu na katika kutekeleza shughuli za kiuchumi zitakazochangia katika maendeleo ya taifa.

Kiongozi Bora hupinga suala la rushwa katika taifa na jamii yake. Hii ni kwa sababu rushwa imekuwa tatizo kubwa Sana katika jamii ya Sasa ambapo imekuwa kipaumbele katika masuala mbalimbali. Kwa mfano katika suala Zima la ajira, inampasa mtu kutoa rushwa ili aweze kupata ajira, Jambo ambalo linawaumiza watu wasio na uwezo kifedha na wale wasioweza kutoa rushwa ili kupata ajira. Pia katika suala la elimu, hasa elimu ya vyuo vikuu ambapo matokeo ya wanafunzi yapo mikononi mwa wakufunzi wao, baadhi ya wanafunzi hulazimishwa kutoa rushwa ya ngono ili waweze kupewa matokeo mazuri, vinginevyo wapewe matokeo mabaya yatakayopelekea kushindwa katika taaluma zao na hata chuo kwa ujumla.

Vilevile katika vituo vya afya rushwa imeshika Kasi kwa kiwango kikubwa ambapo wenye uwezo kifedha hupatiwa huduma Bora na ya haraka kwa sababu ya pesa zao huku wale wasio na uwezo kupata huduma zisizo bora kwa kucheleweshewa huduma na hata kukosa huduma kabisa. Katika mahakama pia haki inanunuliwa kwa pesa kwamba mwenye pesa ndiye mwenye haki hata Kama ndiye mwenye makosa. Hivyo serikali inahitaji viongozi watakaoweza kutokomeza kabisa suala Hilo la rushwa Ili wananchi wasio na uwezo waweze kusaidika.

Aidha viongozi wanapaswa kusimamia matumizi ya mapato ya nchi kwa kupanga bajeti yenye tija kwa taifa na jamii kwa ujumla. Hii itasaidia kuongeza uaminifu baina ya viongozi na wananchi pia kuwasaidia wananchi kulipa Kodi kwa moyo na kufanya kazi kwa bidii huku wakitegemea maendeleo makubwa kutokana na ya kazi ya mikono yao.

Hivyo Basi ili nchi au jamii yoyote iweze kuendelea inahitaji utawala Bora unaojengwa na viongozi waaminifu, wawajibikaji Wawazi na wakweli.
 
Back
Top Bottom