SoC02 Utawala Bora katika kujenga nchi na kuchochea uzalendo bora

SoC02 Utawala Bora katika kujenga nchi na kuchochea uzalendo bora

Stories of Change - 2022 Competition

C87

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
6
Reaction score
1
UTAWALA BORA KATIKA KUJENGA NCHI NA KUCHOCHEA UZALENDO BORA

Utawala bora ni mchakato wa kuongoza nchi kwa kuzingatia suala la Demokrasia na utu wa wazawa katika nchi,utawala bora ni dhana kubwa ya kuwaleta viongozi wanaongoza na raia mahali pamoja ili kulijenga Taifa lenye maendeleo.

Mambo Muhimu katika utawala bora.

1.Uwajibikaji

2.Usikivu na uelewa

3.Demokrasia dhidi ya vyama vingi

4.Uwazi na ukweli

5.Uhuru katika vyombo vya habari katika yale wanayo yaandika.

6.Kutengeneza miundo mbinu (Barabara,Reli,Maji,Shule nk)

7.kupinga suala la rushwa na ufisadi.

8.Utawala bora ni pamoja na kuilinda na kuipigania amani yetu na kuilinda ndani ya nchi na hata katika mipaka ya nchi yetu.

9.Utawala bora ni pamoja na kuwa wazalendo katika yale yanayo husu Taifa letu bila kujali itikadi za vyama vyetu na siasa zetu.

1.Uwajibikaji
Uwajibikaji ni kufanya yale yote yanayopaswa kufanywa kwa kusimamia kweli,mfano ilani mbalimbali katika vyama vya siasa,zinapaswa kutekeleza dhidi ya utawala bora kwa wananchi wake

Viongozi wanapaswa kuwa wajibikaji kwa kuwafikia wananchi katika maeneo yao na kutatua kero zao mbalimbali,dhana ya uwajibikaji ni kuwafikia wananchi kila wakati na sio tu,kipindi cha kwenda kuomba kura katika chaguzi mbalimbali.

2.Usikivu na uelewa
Usikivu na uelewa ni mambo ambayo yanaendana pamoja,usikivu unahitaji kujishusha na kusikia kile kinachotolewa na mwingine na hili ni muhimu sana katika utawala bora,uelewa maana yake ni kusikia na kukubali kupokea pasipo na shaka,yale yanayotolewa na wananchi au na wawakilishi wa Wananchi.Mfano kwenye mikutano kadhaa ya hadhara,katika kata,Wilaya,Mkoa,Tarafa ,au hata katika Bunge.

3. Demokrasia dhidi ya vyama vingi
Nchi yeyote ambayo ni waumini wa utawala bora ni muhimu sana kuzingatia demokrasia katika nchi ili kuwaleta wananchi mahali pamoja,Mataifa mengi ya Afrika yameamka katika suala zima la kuhakikisha utawala bora unazingatia mfumo wa vyama vingi,hapa kwetu Tanzania mfumo huu wa vyama vingi ulianza rasmi 1992,katika mwezi wa saba na hatimaye uchaguzi wa kwanza ukafanyika 1995.

4. Uwazi na ukweli
Uwazi na ukweli katika utawala bora ni mambo ambayo yanaendana ili kujenga nchi iliyo bora kwa wananchi wake, suala la mapato, matumizi ni muhimu pia katika mustakabali wa kujenga nchi iliyostawi kwa maendeleo ya vizazi vyetu vya sasa na vya baadaye.

5. Uhuru wa vyombo vya habari katika yale wanayo yaandika au kuripoti katika runinga au redio
Vyombo vya habari vinapaswa kupewa uhuru katika yale wanaoyaandika au kuripoti kupitia televisheni au redio,uhuru wa vyombo vya habari hautakiwi kupendelea upande fulani,kalamu ya mwandishi au mdomo wa mwandishi inatakiwa/ unatakiwa kuwa na hekima na macho katika kuchochea Taifa lenye maendeleo na tija,vyombo vya habari pia havitakiwi kutumiwa na Maifa ya nje ambayo hayalitakii mema Taifa letu au Nchi zetu za Afrika.

Waandishi na vyombo vya habari wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuchochea demokrasia yetu.

6. Kutengeneza miundo mbinu (Barabara, Maji, Reli, Shule, umem)
Utawala bora ni pamoja na kuwatengenezea wananchi Miundo mbinu bora mfano,barabara zilizo bora,kuwapelekea maji yaliyo safi katika maeneo yao,kujenga shule kwa ajili ya kuwaletea wananchi elimu bora katika maeneo mbalimbali katika nchi,umeme katika maeneo ya mijini na vijijini pia.

Katika miundo mbinu ni muhimu pia kuwajengea wananchi hospitali,zahanati na vituo mbalimbali vya afya kwa ajili ya kujali afya zao

7. Kupinga suala la rushwa na ufisadi
Katika utawala bora ni muhimu pia suala la kupinga suala la vitendo vibaya vya rushwa na ufisadi, Hayati Baba wa Taifa la Tanzania katika moja ya hotuba zake aliwahi kusema rushwa ni adui wa haki. Katika moja ya hotuba yake (1995) Mwalimu Nyerere aliwahi kusema waliamua kuweka adhabu ya viboko kwa watoa rushwa na wapokea rushwa, likiwemo suala la viboko 12 wakati wa kuingia na viboko 12 wakati wa kutoka (Hotuba ya Mwalimu Nyerere 1995.

Muasisi huyu wa Taifa la Tanzania aliendelea kupinga suala la rushwa hata katika Kikao cha almashauri huu ya Chama Cha Mapinduzi,kwa ajili ya kumpitisha mgombea ambaye angesimama wakati huo kukiwakilisha chama.

“Mchagueni, mpinga rushwa, Watanzania wamechoka na rushwa” (Hotuba ya Mwalimu Nyerere 1995)

8. Utawala bora ni pamoja kuilinda na kuipigania amani yetu na kuilinda ndani ya nchi na hata katika mipaka ya nchi yetu.

Kupitia katiba ya nchi ni muhimu kwa watawala kuhakikisha wanailinda katiba ya nchi kwa kuipigania amani ya nchi ili kuepuka suala la umwagaji damu,kwani kutokuilinda amani yetu ni kuruhusu machafuko katika nchi, tunaona mifano ya nchi kadhaa katika nchi za wenzetu, mfano Somalia, Sudan, Ethiopia jinsi ambavyo suala la upotevu wa amani katika hizo zilivyo gharimu amani katika Mataifa hayo na mengine,vyombo vya ulinzi na usalama pia Jeshi, Polisi, Magereza, uhamiaji, mahakama ni muhimu kusimamia sheria bila kuvunja katiba ya nchi juu ya kuilinda amani yetu.

9. Utawala bora ni pamoja na kuwa wazalendo katika yale yanayo husu Taifa letu bila kujali itikadi za vyama vyetu na siasa zetu.

Kama mambo muhimu yahusuyo Taifa ni muhimu kuwa Wazalendo mfano suala la kufana sasa safi ambazo hazina chuki,kufichua mambo mabaya ya kuhujumu Taifa na kuharibu amani katika nchi,suala la haki pia ni muhimu ili kukuza uzalendo wetu.

MAMBO YANAYOWEZA KUHARIBU UTAWALA BORA

1. Vita vya wenyewe kwa wenyewe

2. Siasa zenye chuki.

3. Ukabila

4. Utawala wa mabavu

5. Kutokuwepo kwa katiba yenye matakwa (Utoshelevu) juu ya Wananchi wake

Hitimisho: Suala la utawala bora lizingatiwe kila wakati na liwe ni jambo la kukumbushana kila wakati, katika majukwaa ya siasa au Matukio mbalimbali ya Kitaifa ili kuwakumbusha watu kuzingatia suala hili kuwa na umuhimu mkubwa ndani yao, Wasanii pia ni muhimu kutunga nyimbo mbalimbali kuwakumbusha Watawala na Wananchi namna ya kuzingatia utawala bora na mustakabali wa Taifa letu.


 
Upvote 3
Hongera kwa makala nzuri na yenye mtazamo chanya kwenye jamii.

Ningependa kupata mawazo yako kwenye makala juu ya kesho ya Africa.
SoC 2022 - Kesho ya Afrika ipo katika mtandao

Ikikupendeza tupe kura yako na maoni yako
Habari, kwa wageni wote jinsi ya kunipigia kura gusa kimshale hapa chini ya post chenye arama "^" chini ya chapisho.

Kama ukipata shida kwenye kupiga Kura Tafadhali nijulishe kwenye comment kwa maelekezo zaidi.

Tafadhali lakini pia usisahau Ku-like chapisho na kuacha maoni yako kuhusiana na chapisho hili
 
Back
Top Bottom