Huwezi tofautisha watu na mfumo sababu,mfumo unatengenezwa na watu.Mkuu bhasi tatizo ni watu wenyewe na sio mfumo.
China inakuwa kwa sababu system ipo imara kudhibiti mianya ya rushwa na ufisadi pasipo kusahau kuwa watu wake wanafanya kazi na wanapewa support katika uvumbuzi wao..
Hivyo hata Tanzania tukiondoa mifumo ya kutowawajibisha viongozi na kulea lea ufisadi pasipo kusahau, kutengeneza mazingira wezeshi ya kibiashara, uwekezaji, kazi na teknolojia kwa wananchi wazawa. Nadhani tutafika mbali tu
kuhusu democratic state nadhani Ghana yaweza kuwa ideal na bado ni chumi inayokua kwa kasi Africa wakiwa na demokrasia yao.. "mfumo upo vizuri"
kingine usidate na Figures za pato la taifa tu ukasema Nigeria ni uchumi mkubwa bila kutumia Vigezo vingine kama Human development index , ambayo inapima huo ukubwa kama unaakisi maisha ya wananchi kwa kiasi kikubwa
usishangae Mauritius, Botswana na hata Ghana wakaizidi Nigeria ambayo uchumi wake unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mafuta ambayo yanafaidisha wanaijeria wachache na makampuni ya kigeni... Huku wananchi wa chini wakiendelea kuinjoi power cuts
kwa hiyo tuendelee na style ya trial and errors kujaribisha watu ili tuupate huo mfumo imara wa kidemokrasia?
Huku tukiendelea kurudi nyuma tuki jitahidi tume mark time.
Ghana ina rais mzuri huyu Nana Akufor-Ado lkn nyuma huko nao walikuwa vilaza wamepigwa sana kwenye Cocoa,huyu rais wa sasa ndiye anaye watetea wakulima wake wa Cocoa zidi ya dhuluma ya Uswiss na naujua umahiri wake.Vip huyu akiondoka tutapata kama yule au kwa nini tusimwachie yeye aendelee sababu tushamwona anafaa?
Hii habari siku isema mimi bali BBC,kama sikosei miaka kama mitatu walisema Nigeria iliipiku SA kiuchumi,lkn ukitizama yanayo endelea sasa hivi naijeria,watarudi kulekule rushwa na ufisadi imetamalaki,nchi haina amani so mda si mrefu wanarudi kulekule (wana mark time).
Botswana najua wamecheza vizuri sana kwenye mikataba ya madini,lkn vp nao huyo aliyekuwepo akiondoka je watasonga mbele au watarudi kule kule,sababu hata Nijeria ilikuwa vizuri ila kwa sasa hivi viashiria hivi vya Rushwa,Ufisadi na ukosefu wa amani baadhi ya maeneo nao wanaanza kurudi nyuma.
China huyu Rais wao baada ya kumuona,ameiwezesha inchi kufika level kubwa kiuchumi,wameamua kumuachia aendelee na leo wapo mbali.Kwa nini na sisi tusikopi na kupaste mfumo wa China ili marais wetu wanao fanya vizuri waendelee na team yake.
Kagame yule kaituliza nchi na leo hii Rwanda pamoja na vita yao ya nyuma wamepiga hatua kubwa kimaendeleo,sijajua atakaye kuja atafanya vizuri kama Kagame plus nao wana ukabila siku akipatika mwendawazimu wanaweza rudi kwenye vita.