Utawala bora na nidhamu ya chama cha CPC ni mifano ya kuigwa na Afrika kukabili masikini na ufisadi

Huwezi tofautisha watu na mfumo sababu,mfumo unatengenezwa na watu.


kwa hiyo tuendelee na style ya trial and errors kujaribisha watu ili tuupate huo mfumo imara wa kidemokrasia?
Huku tukiendelea kurudi nyuma tuki jitahidi tume mark time.

Ghana ina rais mzuri huyu Nana Akufor-Ado lkn nyuma huko nao walikuwa vilaza wamepigwa sana kwenye Cocoa,huyu rais wa sasa ndiye anaye watetea wakulima wake wa Cocoa zidi ya dhuluma ya Uswiss na naujua umahiri wake.Vip huyu akiondoka tutapata kama yule au kwa nini tusimwachie yeye aendelee sababu tushamwona anafaa?

Hii habari siku isema mimi bali BBC,kama sikosei miaka kama mitatu walisema Nigeria iliipiku SA kiuchumi,lkn ukitizama yanayo endelea sasa hivi naijeria,watarudi kulekule rushwa na ufisadi imetamalaki,nchi haina amani so mda si mrefu wanarudi kulekule (wana mark time).

Botswana najua wamecheza vizuri sana kwenye mikataba ya madini,lkn vp nao huyo aliyekuwepo akiondoka je watasonga mbele au watarudi kule kule,sababu hata Nijeria ilikuwa vizuri ila kwa sasa hivi viashiria hivi vya Rushwa,Ufisadi na ukosefu wa amani baadhi ya maeneo nao wanaanza kurudi nyuma.

China huyu Rais wao baada ya kumuona,ameiwezesha inchi kufika level kubwa kiuchumi,wameamua kumuachia aendelee na leo wapo mbali.Kwa nini na sisi tusikopi na kupaste mfumo wa China ili marais wetu wanao fanya vizuri waendelee na team yake.

Kagame yule kaituliza nchi na leo hii Rwanda pamoja na vita yao ya nyuma wamepiga hatua kubwa kimaendeleo,sijajua atakaye kuja atafanya vizuri kama Kagame plus nao wana ukabila siku akipatika mwendawazimu wanaweza rudi kwenye vita.
 

Rwanda ina mambo mengi na hiyo stability inamtegemea kwa kiasi kikubwa Kagame..kwa hiyo ni issue ingine

Kuhusu Nigeria labda hujanielewa. Nigeria ina uchumi mkubwa Africa kwa namba tu yaani pato la taifa lao (GDP) ndo liliangaliwa bila kuangalia hilo pata linagawanyikaje au linamfaidishaje mtu wa chini au taifa kiujumla. hivyo BBC hawajakosea ndio maana ili kuupima uchumi vizuri zaidi lazma utumie vipimo kama HDI ambayo inapima mambo kama elimu, afya, vifo nk ndio unakuta hata katika top ten, Nigeria haipo


Kuhusu Ghana, Jerry Rowlings ndio aliiokoa hiyo nchi na kuweka msingi ambao unawapa wananchi power zaidi kuliko viongozi hivyo, kujenga system ambayo italinda maslahi ya nchi pasipo kuangalia kiongozi..ndio maana alipoachia madaraka ndio tukapata hadi huyo rais unaemhusudu.. vipi kama angeamua kukaa madarakani, angefikaje

Issue ni moja, binadamu tunafariki na pia unaweza kujenga mji tripol kwa miaka zaidu ya hamsini na ukabomolewa ndani ya siku moja

hivyo, huoni kama ni vizuri zaidi kuwepo mfumo unaojengwa na kuendeshwa na watu lakini ukitoa power zaidi kwa watu au mfumo kuwawajibisha viongozi ili wasienende kinyume na matakwa ya nchi..

fikiria USA ingekuwaje kama Trump angepewa madaraka walionayo viongozi wa Africa..je kama angekuwa mbaya zaidi ya hapo je, asingebomoa vitu vilivyojengwa kwa karne nyingi...
si uliona kilichotokea

kwa nini tusiende na mfumo huu ukiangalia na viongozi wenyewe tulionao ambao ukiwapa nafasi hawachezei bahati
 
Hizo tawala ni za watu wao ndio maana wamewaacha. Angalia sera zao za kiuchumi zote ni za kimagharibi hivyo hawana shida. Shida itatokea ikiwa masilahi ya kimagharibi yataguswa .. ndio utaona

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Tuletee ripoti ya CAG wa China tuone CCP ilipata hati gani na wapinzani walipataje ili tulinganishe kwanza
 
Tuletee ripoti ya CAG wa China tuone CCP ilipata hati gani na wapinzani walipataje ili tulinganishe kwanza
Ripoti ya CAG china sijaiona ila mambo yao yana enda vizuri na yanaonekana kwa macho hutumii nguvu kubwa kuona maendeleo ya China na vile vile mpaka unaona wahujumu uchumi na wabadhilifu wana nyongwa lazima ukaguzi ulifanyika.

Ila niambie ni uongo vyama vyetu vya siasa vya upinzani vyenye wafuasi wengi havipati hati chafu kutoka kwenye ripoti ya CAG?

Na kwa bahati mbaya hawatoi maelezo ya kueleweka zaidi ya kumung'unya maneno.

So uaminifu wa kupewa vitu vikubwa unaanza na kuonyesha uaminifu kwenye vitu vidogo ulivyopewa.
 
Mnatupigia kelele wakati mnacho kiongea hamkijui, anaye onesha mwelekeo wa mwananchi kuijenga nchi yake ni rais na serikali yake aliyo iunda na kikubwa ni sera ya taifa,

mtawalaumu watanzania wakati wao wala sio chanzo cha tatizo bali tatizo ni sera ambazo zinamfanya mwananchi hata akilima hana pa kuuza mazao yake na mbali na hilo anakumbana na msururu wa tozo sasa sijui anakuwaje mzalendo hapo ndio huwa siwaelewi nyie watoa mawazo.
 
Naona unaongea contradictions. Tafuta kwanza CAG report yao ukiweza kuipata ndio tuje tuongee transparency. Hivi unadhani wangekuwa matajiri kama unavyodai, wangekuja kuchoma mahindi kariakoo?

Tatizo liko kwenye kupima kwa "kuona kwa macho". Hebu achana na hizo mambo halafu tafuta facts kwanza ndio uje tuongee...
 
Mkuu hiyo ripoti si itakuwa imeandikwa kichina?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…