Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Tunahitimisha zile nyuzi zetu za mwezi wa Mungu , Kwenye utawala wa awamu ya 5 , Bwana Paulo Makonda aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , alijipa cheo cha Kitengo cha kudhibiti Madawa ya kulevya kabla ya kudhibitiwa, huku akiutangazia umma kwamba ataweka hadharani Majina ya Waingizaji na wauzaji wa madawa ya kulevya Nchini Tanzania .
Katika kampeni yake hiyo alishirikiana kikamilifu na Simon Sirro aliyekuwa RPC wa DSM , Makonda aliungwa mkono na Vyombo vyote vya Habari vya Tanzania , ikiwemo Clouds Media aliyotuhumiwa kuivamia kwa Bunduki usiku wa manane , huku vyombo hivyo vikirusha live upuuzi wake ule bila hata kuhariri .
Waliotajwa kuhusika na Biashara hiyo bila Ushahidi wowote ni Yusufu Manji , aliyedaiwa kuwa pamoja na kuuza unga pia anabwia , Idd Azan , Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima , Wema Sepetu , Riziwan Kikwete , Nyandu Tozi , Mwanamuziki TID , Freeman Mbowe na wengine wengi tu , Miongoni mwa waliokamatwa ni Josephat Gwajima , TID , NYANDU TOZI na Yusufu Manji , Japo kesi iliyovutia Wengi ilimhusu Mfadhili wa Yanga Yusufu Manji , ambaye mpaka sasa vipimo vyake vya mkojo havijulikani majibu yake ,
Hata hivyo Yusufu Manji aliyekuwa na matatizo ya Moyo na huku akitibiwa Marekani na Muhimbili madaktari wake waliithibitishia Mahakama kwamba kwa afya aliyonayo isingewezekana Kutumia Madawa ya kulevya , Kwa niaba ya Jopo la Madaktari hao Profesa Janabi alileta nyaraka Mahakamani zilizothibisha kwamba kwa Tatizo la Moyo alilokuwa nalo Bwana Manji asingeweza kula Unga , na kama angefanya hivyo angekufa , Mahakama ilipokea vielelezo hivyo kama ushahidi .
Kesi za akina Gwajima , TID , Nyandu Tozi , Wema Sepetu na wengine hazikufahamika zilikoishia , Na wala haikuwahi kufahamika kwanini Mbowe na Riziwan Kikwete hawakukamatwa wala kushitakiwa hadi leo , Mbowe alidaiwa kuitumia Club Bilicanas kuuzia Unga huo , huku haikujulikana kama Riziwani yeye alikuwa anauzia Chalinze au kwingine .
Mwisho tunatoa wito kwa Viongozi wa kuteuliwa kuacha kuchafua watu kwa sababu zao binafsi , huwezi kuwataja watu kwenye tuhuma nzito namna hiyo halafu ukashindwa kuwafikisha Mahakamani , Nani atawasafisha ?
Kwa kumalizia japo si kwa umuhimu tunawashukuru wadau wate wa JF waliotufuatilia kwenye makala zetu kabambe za Mwezi wa Mungu , tunaamini kwamba makala hizi zimewafunza Jambo , Siku zote tutambue kwamba Madaraka ni dhamana ya muda mfupi tu tujitahidi kuyatumia kwa haki .
NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO .