Utawala wa Kizayuni wakili kupata pigo kubwa ndani ya masaa 24

Utawala wa Kizayuni wakili kupata pigo kubwa ndani ya masaa 24

LINGWAMBA

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2023
Posts
484
Reaction score
1,214
Vyanzo vya Kizayuni, baada ya kipindi kirefu cha kudhibiti na kuficha habari kuhusiana na vifo na majeruhi wake vitani, hatimaye vimekiri kuuawa askari jeshi wake 75 katika saa 24 zilizopita.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kanali 12 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni ikimnukuu mchambuzi wa masuala ya kijeshi Barham Meir, imetangaza kuwa, magari 25 ya kivita ya Israel yameharibiwa katika Ukanda wa Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita.

Mtandao huo wa Kizayuni umeeleza kuwa askari jeshi 75 wa utawala huo pia wameangamizwa katika kipindi hicho, jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya utawala huo.

Kuhusiana na jambo hilo ripota wa Al-Alam huko Palestina aliripoti Jumapili kuwa kikosi cha Al-Qassam tawi la kijeshi la Hamas kilitoa taarifa Jumapili asubuhi ya tarehe 12 Disemba na kusisitiza kuwa kimelenga kundi la askari wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kufanikiwa kuwaangamiza wanajeshi na maafisa 60 wa Israel.

Ripota huyo amesema kuwa, kama habari hiyo itathibitishwa, itakuwa ni kama kutokea mapinduzi kamili katika utawala huo ghasibu kwa sababu kuuawa kwa idadi hiyo ya askari wa Kizayuni kunaweza kumsababishia Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu, mgogoro mkubwa wa ndani.

Duru za habari zinasema kuwa, takwimu rasmi za majeruhi na vifo vya utawala wa Kizayuni ni kubwa zaidi kuliko idadi inayotangazwa kuhusu suala hilo na hii inatokana na siasa za kudhibiti na kuchuja habari zinazotangazwa na vyanzo pekee vya kijeshi.
 
Hiyo ndiyo vita hakunaga taarifa sahihi, hata hiyo idadi ya wapalestina waliouliwa ni ya kupikwa tu ili kutafuta huruma ya jamii ya kimataifa. Wao waendelee tu kuuana . Ukimwengu unawatazama tu,mwisho wa siku mshindi atapatikana.
 
Hilo jeshi SI ndio lenye namba nzuri nzuri kitakwimu Kwa ubora duniani?
20230604_005828.jpg
 
Back
Top Bottom