Utawala wa Samia: Siku 100 za Matumaini na zilizobaki za giza

Utawala wa Samia: Siku 100 za Matumaini na zilizobaki za giza

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kuna fikra miongoni mwa wananchi kuwa siku 100 za mwanzo za utawala rais Samia alikuwa akisikiliza ushauri wa wazee hasa raisi Kikwete ndiyo maana kulikuwa na uvumilivu wa kisiasa ndani ya kipindi hicho kifupi, uonevu ulipungua, kesi za kubambikiza zikafutwa n. k

Wananchi wanasema kuwa baada ya miezi hiyo mitatu kuna uwezekano mkubwa kuwa kundi lisilokubaliana na utawala wa Kikwete, na lenye chuki binafsi naye ambalo ni masalia ya mwendazake limefanikiwa kumbadilisha Samia na hivyo kundeleza siasa za ubabe, uonevu, uongouongo.
Wananchi wanadhani kuwa kundi hilo la mwendazake lina longterm goal ya kurudi madarakani na kuendeleza agenda yao, lakini lina lengo la kujilinda kutokana na udhalimu walioutenda kipindi cha mwendazake na kadhalika lina lengo la kulinda positions zao

Wananchi wanadhani kuwa Kundi la mwendazake, limefanikiwa kukamata mpini wa ushawishi kwa rais Samia ndiyo maana Samia amepiga U-Turn na sasa hivi serikali yake imekuwa insensitive kwa hisia za wananchi, imekuwa dhalimu na onevu.

Labda Samia hajui, lakini ukweli ni kwamba Siku zake 100 wananchi walizipokea kwa furaha kubwa lakini siku hizi Uungwaji wake mkono miongoni mwa wananchi unapungua siku baada ya siku, Nenda kasikilize wananchi wanamvyomrate Samia, kwa kweli amepoteza uungwaji mkono kwa kiwango cha kutisha!

Samia ana kazi kubwa mbele yake, lakini ukweli ni kuwa uungwaji wake mkono mbele ya wananchi baada ya siku 100 za utawala wake ni mdogo sana. Sasa ni uamuzi wake, Je aendelee kuwa insensitive au arudi ktk mode aliyokuwa nayo alivyoingia madarakani
 
Ma mkubwa amekosa independent "philosophy na ideology" yake ya kuendeshea nchi iko njia panda.........muelekeo (vision) hana kukurashi ni lazima.
 
Ma mkubwa amekosa independent "philosophy na ideology" yake ya kuendeshea nchi iko njia panda.........muelekeo (vision) hana kukurashi ni lazima.
Inasemekana kuwa akina Diwani na Majaliwa wanamuingiza chaka.

Inasemekana wanajaribu kumuweka mbali na JK wakati angeweza kupata ushauri mzuri sana wa kuongoza nchi kutoka kwa mzee wa Msoga

Bi mkubwa amegeuka katili, muongo, insensitive etc.

Wananchi wanaona anawazingua tu
 
Una uhakika bwashee!
 
Kosa kubwa alilo lifanya Rais Samia ni kumuondoa Dr. Philipo Mpango Wizara ya Fedha na Mipango (Mtaalam aliye bobea katika sekta hiyo), na kumuweka Mwanasiasa mbobezi na mjanja mjanja kama Mwigulu Nchemba!

Tatizo lilianzia hapa! Huyu Mwigulu Nchemba, pasipo kufanya utafiti wowote ule wa kitaalam, akayachukua mawazo ya akina Zungu, na kutuletea hizi Tozo zisizo na uhalisia.

Ukija kwenye demokrasia, amekubali kirahisi kujazwa upepo na washauri wake, na hivyo kuamini kama wapinzani ni watu wabaya, magaidi, watu wa chokochoko! nk. Na hivyo dawa yao pekee ni kuwashughulikia tu.

Ameshasahau ya kwamba yeye pia ni MAMA, ukiondoa huo Urais slio nao. Kwa hiyo alitakiwa awaoneshee upendo kwa kiasi fulani hawa wapinzani waliotengwa na kunyanyaswa kwa miaka mitano na mtangulizi wake.
 
Ile hotuba yake wakati wa uapisho wake na anachofanya leo ni vitu viwili tofauti, inaonesha aliandikiwa akawa anasoma tu vitu ambavyo hakujua utekelezaji wake utakuwaje, leo kawaacha wasioelewa mambo wamuongoze kutupeleka watanzania kwenye lindi la umasikini tena kwa haraka zaidi.
 
Mimi sitaki kumsikia huyo mtu akitajwa kabisaaaaa..
Wamama wenzie huku mitaani kote hawamtaki.
Huwezi amini magu alipendwa kuliko wengi wanavyodhani.
 
Sasa kama ulizoea siasa za kizandiki utampendaje Samia?
Mimi sitaki kumsikia huyo mtu akitajwa kabisaaaaa..
Wamama wenzie huku mitaani kote hawamtaki.
Huwezi amini magu alipendwa kuliko wengi wanavyodhani.
 
Ile hotuba yake wakati wa uapisho wake na anachofanya leo ni vitu viwili tofauti, inaonesha aliandikiwa akawa anasoma tu vitu ambavyo hakujua utekelezaji wake utakuwaje, leo kawaacha wasioelewa mambo wamuongoze kutupeleka watanzania kwenye lindi la umasikini tena kwa haraka zaidi.
Amekupelekaje kwenye lindi la umasikini?

weka ushahidi?
 
Sijui asingekuwa siasani sijui angekuwa anafanya kazi gani.Maana amekaa kama muimba mziki wa.mwambao.
 
Back
Top Bottom