Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Muundo au Mfumo wa muingiliano wa dunia baada ya kuisha kwa vita vya pili vya dunia ulijulikana kama Rules-Based Order(RBO), katika mfumo huu viongozi wa dunia walikubaliana kuachana na ule unyang'au wa wakati uliotangulia wa kutumia mabavu ya vita kujiimarisha na ushindani wa kipumbavu wa mataifa usio na faida kwa dunia.
Pia walikubaliana kushirikiana katika kuimarisha masuala mbalimbali katika ngazi ya kidunia ikiwemo biashara, uchumi, afya, demokrasia, haki za msingi za binadamu n.k
Katika kipindi cha hivi karibuni ni kama mfumo huo umevurigika kabisa na unaelekea ukingoni.
Marekani inajikitia kuweka tariffs za kibiashara kupambana na China na raia wake wengi wanataka hivyo, raia wake wengi na wanasiasa hawataki mashirikiano na wanavishambulia kwa wazi vyombo vya kimataifa kama WHO au ICC
Urusi na Putin wanavamia na wanatishia kuvamia mataifa jirani yao kwa minajili kutanua mipaka yao na sphere of influence kivita bila kuwajibishwa kwa namna yoyote ile. Putin anafikia hatua ya kukiri na kujivuna hadharani kufanya majaribio ya silaha kwa raia wa Ukraine bila kuhofia consequences zozote zile.
Netanyahu anatekeleza vita vya mauaji ya maelfu ya raia Palestina bila kuwajibishwa kwa namna yoyote ile. Hajali kinachoitwa proportionate force kudili na Hamas.
China anatishia kila siku kuivamia Taiwan na visiwa vingine vingi katika eneo la bahari wakidai ni mpaka wao , wanaharibu biashara ya kimataifa kwa bidhaa za ubora duni, devaluation na vikwazo chungu nzima vya kibiashara.
Africa imegeuzwa soko kubwa la silaha, dampo la bidhaa na wawekazaji uchwara na matapeli kutoka mataifa makubwa.
Waarabu wanatumia mafuta kama silaha ya kujifanyia mambo ya hovyo ndani na nje ya nchi zao bila consequences.
Mabadiliko yanahitajika, vinginevyo mafanikio yote yaliyofikiwa chini ya rule based order yatasambaratika na kupotea.