Utawala wa sheria kimataifa (Rules-based order(RBO) umefika katika ukomo wake

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Muundo au Mfumo wa muingiliano wa dunia baada ya kuisha kwa vita vya pili vya dunia ulijulikana kama Rules-Based Order(RBO), katika mfumo huu viongozi wa dunia walikubaliana kuachana na ule unyang'au wa wakati uliotangulia wa kutumia mabavu ya vita kujiimarisha na ushindani wa kipumbavu wa mataifa usio na faida kwa dunia.

Pia walikubaliana kushirikiana katika kuimarisha masuala mbalimbali katika ngazi ya kidunia ikiwemo biashara, uchumi, afya, demokrasia, haki za msingi za binadamu n.k

Katika kipindi cha hivi karibuni ni kama mfumo huo umevurigika kabisa na unaelekea ukingoni.

Marekani inajikitia kuweka tariffs za kibiashara kupambana na China na raia wake wengi wanataka hivyo, raia wake wengi na wanasiasa hawataki mashirikiano na wanavishambulia kwa wazi vyombo vya kimataifa kama WHO au ICC

Urusi na Putin wanavamia na wanatishia kuvamia mataifa jirani yao kwa minajili kutanua mipaka yao na sphere of influence kivita bila kuwajibishwa kwa namna yoyote ile. Putin anafikia hatua ya kukiri na kujivuna hadharani kufanya majaribio ya silaha kwa raia wa Ukraine bila kuhofia consequences zozote zile.

Netanyahu anatekeleza vita vya mauaji ya maelfu ya raia Palestina bila kuwajibishwa kwa namna yoyote ile. Hajali kinachoitwa proportionate force kudili na Hamas.

China anatishia kila siku kuivamia Taiwan na visiwa vingine vingi katika eneo la bahari wakidai ni mpaka wao , wanaharibu biashara ya kimataifa kwa bidhaa za ubora duni, devaluation na vikwazo chungu nzima vya kibiashara.

Africa imegeuzwa soko kubwa la silaha, dampo la bidhaa na wawekazaji uchwara na matapeli kutoka mataifa makubwa.

Waarabu wanatumia mafuta kama silaha ya kujifanyia mambo ya hovyo ndani na nje ya nchi zao bila consequences.

Mabadiliko yanahitajika, vinginevyo mafanikio yote yaliyofikiwa chini ya rule based order yatasambaratika na kupotea.
 
Putin ameuliza mnasema mataifa yote yafuate rule based order. What rules?
Nani na wapi walikaa kutunga hizo rules? Kwa faida ya nani?
Huenda Putin hakuwepo wakati UN inaundwa na makubaliano mengine mengi ya kimataifa kati ya mataifa mbalimbali yaliyofuatia yaliyolenga kuleta utulivu na maendeleo kwa dunia ila anaweza kusoma Historia kufahamu.
 
Utulivu gani umeletwa na UN ?
 
U.S ndio kinara wa kuharibu utawala wa sheria, kwa sababu yeye hataki kuwa chini ya sheria hizo!

Mfano wakati ncho zikijiunga na mahakama ya kimataifa ya jinai ICJ, Marekani sio mwanachama na imepiga marufuku raia wake kushitakiwa kwenye mahakama hiyo!

Lakini wakati huo huo analazimisha mataifa mengine yatekeleze hukumu za ICJ!

Mifano ni mingi!
 
Bidhaa duni za kichina ?wewe unatengeneza bidhaa gani bora ili kuzitoa bidhaa duni za kichina sokoni ?
Nimeacha kusoma hapo hapo kwenye utumbo wake, eti bidhaa duni. Huyu jamaa mjuaji kwelikweli. Kwani kuna aliyelazimishwa kununua hizo bidhaa duni kutoka China?
 
U.S ndio kinara wa kuharibu utawala wa sheria, kwa sababu yeye hataki kuwa chini ya sheria hizo!

Mfano wakati ncho zikijiunga na mahakama ya kimataifa ya jinai ICJ, Marekani sio mwanachama na imepiga marufuku raia wake kushitakiwa kwenye mahakama hiyo!

Lakini wakati huo huo analazimisha mataifa mengine yatekeleze hukumu za ICJ!

Mifano ni mingi!
Hapa kuna hoja lakini ni ukweli pia mahakama za Marekani na Ulaya ziko huru sana kushughulikia mtu yeyote.
 
Huenda Putin hakuwepo wakati UN inaundwa na makubaliano mengine mengi ya kimataifa kati ya mataifa mbalimbali yaliyofuatia yaliyolenga kuleta utulivu na maendeleo kwa dunia ila anaweza kusoma Historia kufahamu.
Put in mnamuonea sana kiukweli kama taifa moja kuvamia jengine ni uvunjifu wa hio inayoitwa RBO basi hao wanao jiona wasimamizi wa hio RBO ndio wanaongoza kwa kuvunja nato walivamia Yugoslavia hawakuishia hapa wakaenda Afghanistan Libya Iraq hawakuishia hapa wanalinda madikteta hawakuishia hapa wanatesa watu Venezuela naungana na Mi mi duniani hakuna hio sheria
 
Muundo au Mfumo wa muingiliano wa dunia baada ya kuisha kwa vita vya pili vya dunia ulijulikana kama Rules-Based Order(RBO), katika mfumo huu viongozi wa dunia walikubaliana kuachana na ule unyang'au wa wakati uliotangulia wa kutumia mabavu ya vita kujiimarisha na ushindani wa kipumbavu wa mataifa usio na faida kwa dunia.

Pia walikubaliana kushirikiana katika kuimarisha masuala mbalimbali katika ngazi ya kidunia ikiwemo biashara, uchumi, afya, demokrasia, haki za msingi za binadamu n.k

Katika kipindi cha hivi karibuni ni kama mfumo huo umevurigika kabisa na unaelekea ukingoni.

Marekani inajikitia kuweka tariffs za kibiashara kupambana na China na raia wake wengi wanataka hivyo, raia wake wengi na wanasiasa hawataki mashirikiano na wanavishambulia kwa wazi vyombo vya kimataifa kama WHO au ICC

Urusi na Putin wanavamia na wanatishia kuvamia mataifa jirani yao kwa minajili kutanua mipaka yao na sphere of influence kivita bila kuwajibishwa kwa namna yoyote ile. Putin anafikia hatua ya kukiri na kujivuna hadharani kufanya majaribio ya silaha kwa raia wa Ukraine bila kuhofia consequences zozote zile.

Netanyahu anatekeleza vita vya mauaji ya maelfu ya raia Palestina bila kuwajibishwa kwa namna yoyote ile. Hajali kinachoitwa proportionate force kudili na Hamas.

China anatishia kila siku kuivamia Taiwan na visiwa vingine vingi katika eneo la bahari wakidai ni mpaka wao , wanaharibu biashara ya kimataifa kwa bidhaa za ubora duni, devaluation na vikwazo chungu nzima vya kibiashara.

Africa imegeuzwa soko kubwa la silaha, dampo la bidhaa na wawekazaji uchwara na matapeli kutoka mataifa makubwa.

Waarabu wanatumia mafuta kama silaha ya kujifanyia mambo ya hovyo ndani na nje ya nchi zao bila consequences.

Mabadiliko yanahitajika, vinginevyo mafanikio yote yaliyofikiwa chini ya rule based order yatasambaratika na kupotea.
Utawala wa sheria haujawahikuwepo kwe mataifa makubwa ila sheria zipo kwa mataifa madogo
 
Back
Top Bottom