Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Wapo baadhi ya watu ambao hupenda kujua mambo yanayokuhusu au mambo asiyoyajua; na anatamani kuyajua ila hapaswi kuyajua kwa wakati huo.
Sasa ikiwa wewe ndiye unaulizwa kuhusu jambo au taarifa fulani unayoijua ila hupaswi kuisema kwa huyo anayekuuliza kwasababu ni SIRI; Je utamdanganya kwa kumpa majibu au taarifa ya uongo?
Nimeuliza swali hili kwasababu kuna watu wengi sana ili kuficha siri zao huamua kusema uongo. Mfano mtu ni mgonjwa ila hataki watu wajue, anaamua kusema kuwa yeye ni mzima tu..
Au mwingine ni mke wa mtu amepigwa na mmewe akavimba jicho akiulizwa anasema alijigonga mahali. Je hii ni sawa?
Kwa mtu kusema uongo ili kutunza siri?